Viongozi wa Yanga ninaheshimu sana kazi yenu maana hakika tunaona timu ilipo kwa sasa. Ila niwaombe sana mjaribu kutumia busara zenu katika hili suala la kuipa timu jina la mchezaji siku ya mechi.
Kwa maoni yangu ninaona linaweza kuharibu umoja na mshikamano kwa wachezaji kwani kunaweza kukaleta tabia za kuchekana, kudhihakiana na hata kuleta unyonge kwa mchezaji husika iwapo timu kufanya vibaya.
Timu inaposhinda hakika inakuwa ni fahari kubwa kwa mchezaji husika kama ilivyokuwa kwa Pacome juzi.
Mfano itokee kuna kamgogoro fulani baina ya mchezaji na wenzake halafu huyo mmoja ikatokea mechi kupewa jina lake inaweza kuharibu mechi kwasababu wapo watakaotaka kumkomoa ionekane heshima aliyopewa haikuwa na Baraka bali gundu kwao.
Hii ya juzi ya Pacome day imefanikiwa sana, lakini ingetokea Yanga kufungwa nina uhakika Pacome angejisikia vibaya zaidi kuliko wenzake na hata baadhi yao wangekuwa wanamdhihaki, pia angezidi kuwa mnyonge kutokana na kuchekwa na kudhihakiwa kwenye mitandao. Ikumbukwe hata suala la kupaka blitch kichwani lilipokelewa na wachezaji watatu tu kwenye timu yake.
Kwa afya ya umoja na amani kwa wachezaji wetu , nawaomba sana viongozi jambo hili liishie tu kwa Pacome na lisiendelee. Tafuteni namna nyingine ya kujenga morali katika timu.
Halafu ndugu yangu Engr Hersi Saidi NIKUSHAURI USIPOKEE KILA JAMBO ANALOLILETA ALI KAMWE. Nadhani unajua mihemko ya vijana ambao hawataki kuoa.