VIDEO - Barcelona Yafanya Mauaji, Yaigaragaza Real Madrid 6-2
Thiery Henry akiifungia Barcelona goli la kwanza Sunday, May 03, 2009 4:48 AM
Barcelona imewafundisha soka watani wao wa jadi Real Madrid kwa kuwabugiza magoli 6-2 katika mechi ya ligi ya Hispania iliyochezwa kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu na kuweka historia mpya kwenye uwanja huo. VIDEO ya magoli yote ya mechi hiyo na matukio muhimu mwisho wa habari hii. Real Madrid haijawahi kufungwa magoli sita katika uwanja wake huo na timu yoyote katika ligi ya Hispania kwa miaka 58 sasa.
Barcelona imezidi kujiweka katika hali nzuri ya kutangazwa mabingwa wa Hispania wiki ijayo itakaposhuka dimbani kwenye uwanja wa Nou Camp baada ya kujikita kileleni kwa tofauti ya pointi saba na wanaowafuatia.
Madriad ndio waliotangukia kufungua mlango wa magoli katika mechi hiyo kwa goli safi la kichwa lililofungwa na Gonzalo Higuain katika dakika 13.
Goli hilo lilikuwa kama Real Madrid wamechokoza nyuki kwani mvua ya magoli ilianza kuwanyeshea kwa Thierry Henry kuisawazishia Barcelona dakika nne baadae kabla ya nahodha wa Barcelona Carles Puyol kuongeza goli la pili dakika tatu baadae.
Lionel Messi alizidi kuwanyamazisha wenyeji kwa kuongeza goli la tatu katika dakika ya 35 na kuifanya Barcelona iende mapumziko ikiwa mbele kwa goli 3-1.
Kipindi cha pili Madrid walikuja na nguvu mpya na kufanikiwa kufunga goli lao la pili katika dakika ya 55 kupitia kwa Ramos.
Goli hilo lilisababisha mvua ya magoli ianze tena kwa Thiery Henry tena kuifungia Barca goli la nne dakika mbili tu baada ya goli la Madrid.
Katika dakika ya 75, Messi alifunga goli lake la pili katika usiku wa leo na la tano kwa Barca baada ya kugongeana pasi za nguvu na xavi na kumalizia kwa goli kali la kiufundi.
Gerard Pique alihitimisha shughuli ya Barcelona kwenye uwanja wa Bernabeu kwa kuifungia Barcelona goli la sita dakika ya 83 baada ya kudondoshewa krosi safi na Samuel Eto'o.
![1900046.jpg](/proxy.php?image=http%3A%2F%2Fwww.nifahamishe.com%2FNewsImages%2F1900046.jpg&hash=0d6026d45f1bd55a597fe19486c82a59)