Kuileta Madrid Bongo ni kituko | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuileta Madrid Bongo ni kituko

Discussion in 'Sports' started by falesy, Oct 8, 2006.

 1. f

  falesy Senior Member

  #1
  Oct 8, 2006
  Joined: Mar 15, 2006
  Messages: 105
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ijulikane kwamba hakuna mtanzania asiyependa maendeleo ya michezo lakini kwa hili la Real Madrid siliiungi mkono hata chembe. sababu ziko nyingi lakini moja tu ya kiuchumi na kushuka kwa thamani ya sarafu yetu nitaiweka wazi.

  real Madrid ni timu kubwa yenye wachezaji wa ghalama kubwa na wenye kuhitaji ulinzi mkubwa na kubwa zaidi wanaoishi maisha ya kitajiri sana. mshahara tuchukulie wa mchezaji mmoja david Beckham ni pound 120,000/= kwa wiki thamani ya paundi hizo ni shilingi za kibongo milioni mia mbili na arobaini (240,000,000/=) sasa huyo ni mchezaji mmoja je unaweza kufikiria ghalama ya kawaida sana ya kuishi hapa bongo kwa bekham itakuwa sh ngapi kwa siku? haipungui milioni saba(7,000,000) sasa waje wachezaji labda 18 viongozi jumla 7 kwa ujumla wao wawe 25 pamoja na rais wa timu yao na kisha wakae siku mbili utaweza kufikiria thamani ya shilingi yetu itashuka kwa kiasi gani kwa maana dola zitatafutwa ili kuwakimu hawa jamaa na hapo hapo kumbuka hawaji kutumia dawa za huku, maji ya huku, oh pipi za huku vyote wanakuja navy hivyo hatutafaidi kwa kuwauzia hata pipi tu je safari hiyo ina manufaa gani kwa Tanzania.
  ningeshauri serikali iombe uwanja uzinduliwe katika miongoni mwa mechi za AFCAN ili kufikia malengo yetu kiuchumi. tupange mambo yetu ikifika wakati tuwataarifu CAF kwamba mechi moja sema ya SENEGAL itafanyikia uwanja mpya.
  mie ninavyoona Rais akae aangalie jinsi ya kujenga uchumi na si kuangalia Taifa Stars (sisemi aiache lahasha) tu.
  MUNGU ibariki TANZANIA
   
 2. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #2
  Oct 9, 2006
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  TAHARIRI

  Bajeti ya Real, ni bora Stars ikajinoa Hispania


  KWANZA, tuanze kwa kuipongeza timu yetu ya Tanzania kwa kufanya vema katika mchezo wake wa pili wa michuano ya kusaka nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika.

  Timu hiyo jana ilitoka sare ya bila kufungana na Msumbiji katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Machava mjini Maputo.

  Ulikuwa ni mchezo wa pili kwa Stars ambao matokeo hayo yameifanya ikae kileleni katika kundi lake la saba baada ya kukusanya pointi nne ikifuatiwa na Senegal yenye pointi tatu, sawa na Burkina Faso, ilhali Msumbiji imeambulia pointi moja hadi sasa.

  Timu hizo zinasaka nafasi moja ya kwenda Ghana mwaka 2008 katika fainali zitakazokuwa na mvuto wa aina yake.

  Mechi zijazo, Stars itakipiga na Senegal jijini Dakar, itafanyika Machi mwakani.

  Baadhi yetu tumeiona mechi ya jana kati ya Stars na Msumbiji. Kwa wataalamu wa soka watazungumza mengi, lakini ukweli ni kwamba maji yalikuwa shingoni.

  Tunashukuru tumepata matokeo ya sare yanayotupa nguvu na matumaini ya kujipanga upya kwenda Ghana kushiriki fainali hizo kwa mara ya pili. Ikumbukwe, kwa mara ya mwisho Stars kushiriki fainali hizo ni mwaka 1980 nchini Lagos, Nigeria.

  Kutokana na upungufu wa uzoefu ulioonekana, tungependa nasi tutoe machache kabla ya mchezo ujao dhidi ya Senegal, timu iliyopewa nafasi kubwa ya kufanya vema katika kundi hilo la saba.

  Mechi ni kama vile iko mbali, lakini ukweli ni kwamba iko jirani, na maandalizi yake bila shaka yanahitaji muda zaidi dhidi ya vigogo hao wa Afrika wenye uwezo pia wa kucheza fainali za Kombe la Dunia.

  Rais Jakaya Kikwete ameweka mambo hadharani kwamba Real Madrid itafanya ziara Tanzania Julai mwakani kwa ajili ya sherehe rasmi za kufungua Uwanja mpya wa Taifa, Dar es Salaam.

  Hakuna ubishi, fedha za kuileta timu hiyo ni nyingi. Ndiyo maana Rais wetu amesema wazi kuwa, kunahitajika wadhamini ili kuileta klabu hiyo maarufu Hispania na duniani.

  Sisi tunadhani, ni vema wafadhili hao wakaungana na wengine waliojitokeza kuiandaa Stars katika kambi ya kitaifa, yenye kila aina ya chembe ya uzalendo, ili timu yetu ifuzu kwenda Ghana.

  Suala la Madrid kuja nchini lina faida na baraka zake, lakini la kuiandaa zaidi Stars ni la muhimu zaidi kwa soka ya Tanzania katika kampeni yetu ya kwenda Ghana.

  Tunasema haya kutokana na ukweli kuwa, kitendo cha Stars kwenda Ghana, kuna umuhimu na hadhi kubwa kwa taifa kuliko ujio wa Real Madrid.

  Tutafarijika kama wadhamini wengine watajitokeza lakini tunachohitaji kwanza ni bajeti ya Stars ili ifuzu kwenda Ghana, kwani hakuna linaloshindikana.

  Bila shaka, wengine watafikia hatua ya kuunganisha msimamo huu na ule uliotolewa na baadhi ya wanasiasa wa upinzani kuhusu hili. Hata kama itakuwa hivyo, lakini ukweli unabaki kuwa, ni vema Stars ikapewa nafasi ya kwanza kuliko ujio wa Real Madrid nchini.

  Msingi wa msimamo wetu umejikita katika mizania ya umuhimu wa Stars kwenda Ghana na ujio wa Real Madrid.

  Tunasema, ni vema zaidi fedha za kuileta Real Madrid nchini zikatumika kutunisha mfuko wa kuitunza Stars, hata kwenda nje ya nchi ili tuweze kwenda Ghana.

  Itakuwa ni heri kuona Stars ikienda kupiga kambi hata kama ni nchini Hispania ili wachezaji wetu waweze kupata maarifa na mbinu zaidi.

  Tunaamini ikiwa hivyo, Stars itaweza kujifunza mengi na hata kucheza mechi za kirafiki na klabu za Real Madrid, Barcelona na nyinginezo.

   
 3. K

  Kulikoni JF-Expert Member

  #3
  Oct 9, 2006
  Joined: Aug 28, 2006
  Messages: 203
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nakubaliana na maoni ya TAHARIRI na Mh. Mbunge Halima. Ufwedha wa kuileta REal Marid ni bora utumike kuifua zaidi Stars.
   
 4. J

  JokaKuu Platinum Member

  #4
  Oct 9, 2006
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,107
  Trophy Points: 280
  kuna tatizo kidogo katika hilo pendekezo la hiyo tahariri.....

  ningekubaliana na pendekezo hilo, ikiwa timu yetu ingekuwa inajiandaa kwa mashindano yatakayofanyika ulaya, ambako kuna mazingira kama ya Madrid.

  tunakwenda kucheza dakar senegal hivyo hatuna budi kujua mazingira ya huko yako namna gani. zaidi, mechi itachezwa muda gani, na hali ya hewa itakuwa vipi.

  baada ya uchunguzi huo ndipo tunapaswa kwenda kupiga kambi ya mazoezi katika eneo lenye mazingira kama hayo. mara nyingi timu yetu imeshindwa kwasababu ndogo kama kukosa viatu vya kucheza katika tope na utelezi. kukosa jezi za kuvaa wakati wa mvua n.k. tungejisumbua kidogo, kwa kutumia hata maofisa wetu wa ubalozi, tungeweza kujiandaa vizuri kwa mechi za ugenini.  wamarekani waliweza kushinda nafasi ya pili katika marathon za olimpiki za athens kwasababu waliweza ku-simulate hali ya hewa ya ugiriki, pamoja na miinuko na tambarare, ya njia ya kukimbilia marathon, ndani ya gym marekani.

  watanzania wenzangu, michezo ni sayansi. kumpeleleza[scouting] mpizani wako ni kitu cha muhimu sana. ili kujihakikishia ushindi ni vizuri tukawajua wachezaji wa timu pinzani, na mbinu wanazotumia.

  Kama tunakwenda kucheza Senegal basi tunapaswa tukapige kambi ya siri, walau kwa wiki moja,Mali, Guinea,au Mauritania, nchi zinazopakana na Senegal. Hapo tunajihakikishia kwamba siku ya mpambano hali ya hewa haitatuathiri. vilevile tunapaswa kucheza mechi za kirafiki na timu zilizocheza na senegal na kuwapa taabu kidogo.
   
 5. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #5
  Oct 10, 2006
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Safari itadhaminiwa, Serikali haitoi hela. Watu wanachosema ni kuwa huyo mdhamini aidhamini Taifa stars na sio kuileta Real
   
 6. M

  Mwanagenzi JF-Expert Member

  #6
  Oct 10, 2006
  Joined: Sep 11, 2006
  Messages: 690
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Ina maana ziara ya JK hapo Real Madrid inaanza kuvutia "wawekezaji wa soka"?

  Angalia habari hii...

  Kocha wa Man United aiona Taifa Stars Maputo

  Na Angetile Osiah, Maputo
  KAMA wachezaji wa Taifa Stars wana ndoto ya kucheza soka barani Ulaya, basi watakuwa wameshaanza kujitafutia soko baada ya kocha msaidizi wa Manchester United, Carlos Queiroz kushuhudia wakati wakichuana na Msumbiji kwenye Uwanja wa Machava.

  Mbali na kocha huyo, ambaye pia aliwahi kuifundisha klabu ya Real Madrid, wachezaji wa Stars pia walipata fursa ya kuonyesha vipaji vyao mbele ya gwiji wa soka wa Ureno, Eusebio, ambaye pia alikuwepo uwanjani kushuhudia mechi hiyo ya Kundi la Saba la michuano ya Mataifa ya Afrika iliyoisha suluhu.

  Haikueleweka ni sababu gani zilizomfanya kocha huyo msaidizi wa Alex Ferguson kutua jijini Maputo kushuhudia pambano hilo, lakini Eusebio ni mtoto wa wazazi wa Msumbiji, ambaye alikulia nchini Ureno na kuchukua uraia wa taifa hilo wakati akingara duniani kwa kusakata soka.Queiroz , hata hivyo, ni Mreno, nchi ambayo ina uhusiano mkubwa na Msumbiji
  katika njanja zote.

  Wawili hao walikuwa wamekaa jukwaa la wageni wa heshima na hivyo waandishi hawakupata nafasi ya kuwahoji zaidi ya watangazaji wa redio waliokuwa karibu yao.Katika mahojiano yaliyofanywa na watangazaji hao, Queiroz alisifu mchezo wa kujihami ulioonyeshwa na Stars uliowanyima nafasi washambuliaji wakali wa Msumbiji, akiwemo Dario Montero,anayesakata soka nchini Ufaransa, kushindwa kutikisa nyavu.

  Mchezo wa kujihami uliwafanya wachezaji wa Stars kushindwa kuonyesha vipaji vyao kutokana na viungo kuamua kupiga pasi ndefu kwa washambuliaji Gaudence Mwaikimba na Said Maulid kila walipopata mpira, mipira ambayo ilipokonywa kirahisi na mabeki wa Msumbiji na kurudishwa golini mwa Stars.

  Pengine mchezaji ambaye anaweza kuwa alionyesha kiwangocha juu alikuwa kipa Ivo Mapunda, ambaye mbali na kuokoa mipira kadhaa, aliiokoa Stars na kipigo mwanzoni mwa kipindi cha pili alipotoka golini kwenda kupangua kiki ya chini ya winga hatari wa kushoto, Miro, ambaye alipewa pasi akiwa peke yake.
   
 7. J

  JokaKuu Platinum Member

  #7
  Oct 10, 2006
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,107
  Trophy Points: 280
  Mwanamagenzi,
  huyu kocha msaidizi wa Man United ni raia wa Ureno. Msumbiji ni koloni la zamani la Ureno. Kama angekuwa anatafuta vipaji/wachezaji wa Tanzania basi angekuja nchini kwetu, siyo Msumbiji.

  Halafu, kama Madrid wana-scout wachezaji wa Tanzania kwanini wamtume kocha msaidizi wa Man United?

  Mimi naona kuwepo kwa kocha Msaidizi wa Man United hapo uwanjani Maputo hakuna uhusiano wowote ule na ziara ya Kikwete Madrid.
   
 8. Z

  Zanaki JF-Expert Member

  #8
  Oct 10, 2006
  Joined: Sep 1, 2006
  Messages: 544
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mwanagenzi...Carlos Queiroz nae ni mzaliwa wa Msumbiji,alishafundisha timu ya taifa ya Afrika Kusini na alifukuzwa.
   
 9. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #9
  Oct 10, 2006
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,723
  Likes Received: 1,218
  Trophy Points: 280
  Licha ya kuwa mzaliwa wa huko Nchumbiji, pia hutembelea huko mara kadhaa na ana miradi ya soka.....
   
 10. C

  Comrade Mfate Member

  #10
  Oct 11, 2006
  Joined: Sep 26, 2006
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu hawa wabongo ukiwaambia Wadhamini kujenga uwanja mwingine watasuasua sasa kama watatokea watu kudhamini safari ya madrid its ok ilimradi isiwe hela ya serikali ambayo ni jasho la watanzania maskini pia kumbuka kuwa hawa mabigwa wa ulaya wakija watatoa hamasa kwa wabongo kujali michezo hasa Soka
   
 11. K

  Kulikoni JF-Expert Member

  #11
  Oct 12, 2006
  Joined: Aug 28, 2006
  Messages: 203
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tanzania now 28th in Africa

  http://www.thisday.co.tz/Sports/864.html

  THISDAY REPORTER
  Dar es Salaam

  TANZANIA has maintained a steady rise in the FIFA World rankings, moving seven steps to the 28th position in Africa on the monthly log.

  The country also moved 38 places in the world to equal its highest ranking in six years, according to the September assessment of the world soccer's governing body.

  The national soccer team's impressive performance in the 2008 African Cup of Nations qualifiers played a role in improving the country's status.

  Marcio Maximo's lads launched their campaign in the qualifiers with a 2-1 home win over Burkina Faso on September 2.

  On Sunday, they battled to barren draw with Mozambique in Maputo to dislodge Senegal from the top of Group Seven.

  Burkina Faso have dropped seven places to the 23rd position in the continental ranking, while Mozambique are now ranked 38th, six places down the table.

  Senegal, Taifa Stars' next opponents in the qualifiers, remain unruffled at the eighth berth despite going down 1-0 to Burkina Faso on Saturday.

  Senegal tie on three points with Burkina Faso, one point adrift of Taifa Stars, whose first ever appearance in the Nations Cup finals dates back to 1980 in Lagos, Nigeria.

  Bottom-placed Mozambique now bank on miracles to make it into the Ghana finals. They have only one point so far after two matches.

  Tanzania is also ranked second in East Africa, behind Uganda, but ahead of neighbours Kenya.

  Kenya have nothing to show for their efforts in the qualifiers. They tumbled 2-1 and 3-1 to Eritrea and Angola, respectively, in their first two matches.

  In East and Central Africa, Tanzania is now ranked third behind Ethiopia and Uganda, while Djibouti are glued at the bottom of the table.
   
 12. m

  mTz JF-Expert Member

  #12
  Oct 12, 2006
  Joined: Aug 20, 2006
  Messages: 283
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ah! hata majirani zetu wakenya tumewapiga bao!
   
 13. a

  alles JF-Expert Member

  #13
  Oct 15, 2006
  Joined: Oct 14, 2006
  Messages: 356
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii ndio raha ya kuwa na Kiongozi kilaza wa nchi, siku zote anafikiria mambo ya kumuongezea umaharufu badala ya kujenga nchi. Angeshuka Spain na kuomba Solar power or alternative power kwa ajili ya kukabiliana na tatizo la umeme nchini kwetu ingekuwa vizuri zaidi.Uchumi wa nchi yeye haumuhusu kabisa kwa sasa yuko busy na michezo.
   
 14. m

  masai New Member

  #14
  Oct 18, 2006
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  We kichwa unazni kuileta realmadrid ni kuwalipa mishahara selikari haita toa mbuni wala nini je vipi kama huyo beckam angekuwa mtanzania au cameroon wanapo kwenda kwao kwenye mechi za africa wanalipwa nini hau haujui na wao wachezaji wao wote wanalipwa ma pound. kichaa wale wakija uchumi wa bongo utakuwa kwa asilimia 0.0009 kwa kuwa habari zitauzwa, hoteli zitajitangaza kuna wazamini kama makampuni makubwa kama siemens wata zamini mpambano. we unazani mohamed ally alipo kwenda kupigana zaile uchumi wao ulikuwa kwa cm chache kapuko we  [/I]
   
 15. f

  falesy Senior Member

  #15
  Oct 19, 2006
  Joined: Mar 15, 2006
  Messages: 105
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
   
 16. Maxence Melo

  Maxence Melo JF Founder Staff Member

  #16
  Oct 20, 2006
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 2,606
  Likes Received: 1,704
  Trophy Points: 280
  LoL, visit JamboPhotos and you will Nkapa doing it right!
   
 17. COLE

  COLE Member

  #17
  Oct 23, 2006
  Joined: Oct 21, 2006
  Messages: 70
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 25
  wanajamboforum

  Binafsi yangu me nafikiri kuja kwa Real Madrid hapa Bongo ni changamoto kubwa kwa Watanzania hasa wanamichezo wato nchini, kama unavyojua Club Madrid imepiga hatua kubwa sana ni moja ya club kubwa na bora duniani, kuja kwao hapa Tz sio dhambi na sioni kama ni tatizo mimi nalichukulia kwa uzito mkubwa na kwamba wavile ni walimu amebobea kwa football na tukiwa wajanja tutajifunza mengi sana kwa muda mfupi, na watatuelewa sisi maana mimi kwa mawazo yangu madogo haya naamini sana kuwa tuna vijana wengi wanavipaji vya mpira wa miguu.Sasa tunaweza kupata soko sio la kwenda Hispani huko mjini Madrid bali popote pale duniani kucheza soka vijana wetu, kwakupitia hao Real Madrid kwani watakuja na waadishi wao wa habari.

  Tanzania sasa hivi tuna hotel nyingi za kimataifa tena bora ambazo tajiri yoyote duniani anaweza kuja na kulala bila shaka hata hao wachezaji millionea wanaweza kupata mahitaji yoye hapa nchini, na Hotels zetu zikafanya kazi na kupata faida kubwa bila wako kufungasha

  Pesa hazita tumika hata shilingi moja ya kodi ya Mtanzania

  baadae
   
 18. N

  Nego Member

  #18
  Oct 26, 2006
  Joined: Oct 25, 2006
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hi jamani hata tukiachia mbali uchumi, hivi si aibu Rais wetu kwenda Madrid kuomba hao jamaa waje Tanzania; siangemtuma hata waziri wake tu; au hata TFF?
  Na marekani nikamwona kwenye mambo ya Basketball.........anatafuta wawekezaji?! Huyu jk jamani hana washauri nini, au ndio matokeo ya kujizungushia wanamtandao badala ya wasaidizi makini; wanaojua wamewekwa pale kutoka na uwezo wao bali si nafasi yao katika mtandao?!

  ngoja tuone avyoelekea Japan ataibuka na nini...usishangae akarudi na mwaliko wa wana SUMO!
   
 19. H

  HKiboka Member

  #19
  Mar 7, 2007
  Joined: Feb 6, 2007
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna mambo mengi ambayo hufanywa kwa kukurupuka na serikali, sio hii ya JK pekee bali hata waliokuwepo kabla yake wote! Nisingependa kuelezea ni kwa jinsi gani kila mmoja alikurupuka,lakini tuliangalie hili suala la Real Madrid kuja Tanzania lina manufaa au ni hasara kwa walipa kodi hohe hahe ambao watoto wao wanakaa chini katika shule za sekondari!
  Ni ukweli usio pingika kuwa kuja kwa Madrid ni hasara kubwa kama ilivyo Rada na Ndege kama watakuja kwa masharti waliyotoa.Wanataka kuja watu themanini ambao watagharamikiwa kila kitu zikiwemo posho za wachezaji! Labda watu hawajui kuwa posho za wale jamaa si kama za Simba na Yanga, ni mamillioni kwa mchezaji mmoja kwa siku! Sasa mamilioni haya ni sawa na madawati mangapi?,vitabu vingapi? au Mishahara ya waalimu wangapi kwa mwaka ambayo Madrid watapewa siku kadhaa tu! Je, mechi za kufuzu kombe la mataifa hazitatosha kuutangaza wanja huu? je hatuwezi hata tukawalipa Suppersport wakautangaza uwanja huu japo kwa nusu saa pekee? Kwanini Madrid waje wachukue fedha zetu na wakati kuna uwezekano wa kuepusha hilo na tukaendelea kukuza mpira wetu hata kwa kuzidisha safari za Brazil na kwingineko?je mechi moja kati ya Stars na Madrid itabadilisha soka letu kuliko safari ya Brazil?
   
 20. Dua

  Dua JF-Expert Member

  #20
  Mar 9, 2007
  Joined: Nov 14, 2006
  Messages: 2,481
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Tanzania prepare for Madrid visit
  [​IMG]


  President Jakaya Kikwete visited Real Madrid last year


   
Loading...