Kuikumbatia Morocco Tutaumia Baadae!!

Kuikumbatia Morocco Tutaumia Baadae!!

Kweli sisi tu wavivu kiasi hata cha kushindwa kulala, hatujui hata kitu cha kuomba? Morocco inakuja na mipesa yake, jamani nataka kurudi AU, naomba mnisaidie kushawishi wenzenu. Sisi tukasema sawa tutakusaidia, lakini kwa lipi? Morocco ikajibu lolote nyinyi ombeni! Katika maombi, tukaomba kujengewa msikiti na uwanja wa mpira. Haki ya Mungu!
Kumbuka mfano wa nyerere wa mtz mwenye almasi na tapeli mwenye kipande cha chupa.
 
ukiwa na fikra za kupinga kila kitu daima hutaona jema hata moja,mathalani kama ulifuatilia vizuri kilichokuwa kinazungumzwa jana wala leo hii usingekuwa na kwanini zako hizo,kingine sisi watanzania ebu tujifunze kufanya vitu kwa mipango endelevu na sio kwa ajili ya kuridhisha watu,bado nitatetea kuwa JPM jana alisema kuwa uwanja ,msikiti ni baadhi ya vitu vingi ambavyo wameongea na kukubaliana na mflame yule katika kuhakikisha mafaniko yanafikiwa.

Kingine kumbuka Mfalme huyu kaja hapa kwa malengo mawili aua matatu tofauti,moja kuomba kuungwa mkono,pili ni ziara rasmi ya kiserikali ,tatu amekuja kwa ajili ya kutalii ndio maana ataenda na ngorongoro kule.

Ukija katika ziara ya kiserikali ndio utaona kuwa wamesaini mikataba ya ushirikiano zaidi ya 22 na YOTE NI YA kimaendeleo hasa ikilenda diplomasia ya uchumi,theni hilo la kuunwa mkono ni sehemu tu ya ziada katika safari yake
Kuungwa mkono ndio sababu kuu iliyomleta mvamizi huyo,
 
Wewe unaingiza udini huna lolote. Morocco ni nchi ya kiislamu rais hakufanyakosa Waislamu wa Tanzania kusaidiwa na waislamu wenzao wa Morocco
Ni kazi ya raisi kuwaombea waamini misikiti na makanisa kutoka kwa wakoloni tuliowakataa?serikali si mnasema haina dini?
 
kuna mengi sana ambayo yamekubaliwa ktk MoU hii ambayo serikali imesaini na hawa Morroco lkn tatizo linaonekana ni kuwekwa kipengele cha kujengwa msikiti ndio kimekuwa kiroja,hebu tupunguze chuki toeni taarifa ya makubaliano yote iliyosainiwa.AMESEMA KWELI MZEE MWINYI.
LA uwanja na msikiti ndo limeonesha hakuna cha maana kwenye MOU na Morocco watafaidika na sisi kuliko sisi kwa wao.
 
Maadui wa Nyerere ndio wamekuwa marafiki wa Magufuli,madui wa Jk ndio wamekuwa marafiki wa Magufuli,tulikataa kutawaliwa na wazungu na sasa tunakwenda kutawaliwa na waafrika wenzetu, kwa sababu ya kuendekeza njaa zetu.
 
Van persie ni mchezaji mpira maarufu sana duniani ameoa morocco mwanamke anaitwa Bouchra. Morocco kuna wadada wazuri pia kwa sisi waoaji tunaweza kutumia fursa hii kupata ndoa(kijamii tunafaidika + msikiti + uwanja wa mpira). Pia kupitia mikataba na morocco tutafaidika kiuchumi na kisiasa.
Mkuu chukua tahadhari unapochangia mada maana kuna tafiti zimetoa matokeo hivi karibuni usije ukajumuishwa humo.
 
Wa Morocco si watu wazuri,shauri yenu,hata Ronaldo kakatazwa kwenda Morocco.
 
Mkuu chukua tahadhari unapochangia mada maana kuna tafiti zimetoa matokeo hivi karibuni usije ukajumuishwa humo.
*Hapo nimezungumzia ndoa
*Pia nimezungumzia msikiti
*Na ujenzi wa uwanja wa mpira

Kipi hapo kimekutatiza kadhi mkuu
Utafiti wa watanzania vichaa ni uchwara
 
Kila kitu mnalaumu! Hii ndiyo recipe ya watu maskini!
 
Huyu jamaa wakati akipiga kampeni za urais alisema kuwa yeye serikali yake haitakuwa OMBAOMBA kwa sababu aliiona hii nchi ni tajiri saaaana.Sasa Je huo utajiri wa MAMA TANZANIA umepotelea wapi, au baada ya kuingia madarakani amepofuka macho hayauoni tena huo utajiri aliokuwa akiuona wakati wa kampeni???.Ooooooooohh CCM ya maombaomba. k
Kumbe Mnawafukuza ombaomba mjini ili wawaachie nafasi ya nyie kuombaomba vizuri!!!!!! hahahahaaaaaaaaaa serijali ya viwanda kumbe serikali ya kuombaomba.
 
Ufalme wa Morrocco sio sawa na ufalme wa Uingereza. Mfalme wa Morroco anaweza kutoa maamuzi yakawa ni kama serikali lakini ni yake binafsi kwa madaraka aliyonayo. Katika imani ya Kiislam kuna kitu kinaitwa sadak Jaalia, yaani sadaka ambayo utaendelea kupata fadhila za Mwenyezi Mungu hata baada ya kifo chako, hivyo Mfalme ameamua kutoa hivyo akijua malipo atayapata kwa Mwenyezi Mungu, na ndivyo Waislam wanavyojitahidi kujenga misikiti, visima, shule nk (kwa wale wenye imani na uwezo), kwa hilo moja sidhani anategemea kupata return kama tunavyofikiria.

Makanisa yote haya makubwa ya Roman, na mengineyo ni misaada toka Rome, Uingereza na Marekani kuendeleza imani walizonazo. Kwa msaada wa kujengewa msikiti imekuwa nongwa, au kwa vile Papa na wengine huwa hawatangazwi?

Sasa hivi Tanzania ina uwanja mmoja tu ambao tunaweza kujivunia. Hivyo kama tumeweza kupata offer ya kujengewa uwanja mwingine, basi tutakuwa na viwanja viwili. Wito wangu, Rais Magufuli au serikali yake akija na mgeni mwingine tajiri pamoja na mengineyo endelea kuomba "msaada" wa kiwanja, na mwingine na mwingine, mwisho wa siku tutakuwa na viwanja kadhaa ambavyo tutakuja kuomba kuandaa mashindano ya kimataifa kama vile AFCON, mashindano ya Vikombe mbalimbali vya dunia (wakubwa na vijana), Olympic nk kwa kuwa tutakuwa tayari na miundombinu ya michezo. Mashindano kama haya yakiandaliwa kwa ustadi yataleta faida kubwa sana kiuchumi (utalii, mahoteli, huduma).

Sasa hivi tunayo matatizo mengi, yaani huduma za afya, mawasiliano, elimu na mengineyo lakini isitufanye tusiendelee na maeneo mengine kwa vile tu hatuna madawa, au shule. Vyote vifanyike tu. Tukifanya vibaya kwenye michezo kelele, sisi wenyewe tunailaumu serikali kwa viwanja vibovu sasa binadamu mfanyiwe nini?
 
Hoja dhaifu sana hizi,mbona tumerudisha uhusiano na ISARAEL wanakalia kwa mabavu ardhi ya watu lakini walikua kimya na wangeni walipongeza kwa kusema haina haja kuendelea na kinyongo
Tanzania ni nchi huru in uamuzi wa kufanya inachoona sahihi
Tumempa magufuli bendera atuongoze,tutampima akimaliza miaka yake mitano,hizi porojo zetu haziwezi kumyumbisha
 
Katika ulimwengu wa sasa NO FREE LUNCH, Hata mabilionea duniani hawawezi kukupa pesa bure tu pasipokujiuliza impact ya msaada anaokupa labda kwake yeye, jamii inayokuzunguka, majirani zako, na wadau wote kwa ujumla. Kwa hili kukubaliliwa kujengewa uwanja wa mpira na msikiti mkubwa are there the priorities of the nation??? Je zipo kwenye ilani ya chama. Watakonufaika na uwanja na msikiti ni wangapi.

Ni vijiji vingapi havina maji, huduma ya afya, elimu. Vipi swali NYETI la kujenga viwanda ambalo ndo makakati wa nchi kwa ujumla. Bado nina wasiwasi kuwa ahadi ya kufanya hayo hazikuombwa na mkuu wa kaya BALI ni kitu anachohitaji kufanya mfalme mtukufu mgeni katika ardhi yetu kwa agenda binafsi ya kurahisisha baadhi ya mambo amabayo tutajaona siku za usoni.
TUNAJIDANGANYA TU.

Henry Kissinger wakati Fulani alipata kuishauri serikali ya Marekani enzi hizo. Kwamba ukitaka kulikamata bara la Afrika nenda kamweke sawa Julius Nyerere na Tanzania. Ukimweka sawa Nyerere basi ni rahisi kwa mataifa mengine.

KUHUSU MOROCCO
Miaka 32 iliopita tuliwatangazia Morocco msimamo wetu kupinga mabavu yake huko Sahara Magharibi. Tuliwaambia pia waafrika wenzetu.Tuliutangazia ulimwengu wote. Msimamo wetu ulikuwa kuwaunga mkono Sahara Magharibi ili wajitawale.

Miaka 32 baadaye tumeikaribisha Morocco nchini kwa gego na fizi (Hongereni). Tumeketi mezani kuzungumza na Mfalme Mohammed VI (sina hiyana Naye).

Tumemwambia ushirikiano wetu ni diplomasia ya uchumi, demokrasia na mengineyo. Halafu tumemwambia atujengee nyumba ya Ibada na uwanja wa soka huko Dodoma. Vyote amekubali. Sina tatizo na maombi hayo. Tatizo ni kujidanganya kwetu bila soni.

Toka mwezi Januari mwaka huu kuna kampeni kubwa imeshika kasi Morocco irudishiwe uanachama wa AU. Julai 17 mwaka huu kule Kigali, Rwanda, Mfalme Mohammed VI aliandika barua kwenda kwa Mwenyekiti wa AU, Rais Idris Derb kwamba wapewe nafasi yao AU. Akaomba huruma ya wanachama wa AU(kuna mgawanyiko, na naamini pia utazihusisha Anglophone na Francophone).

Morocco imefanikiwa kushawishi baadhi ya wanachama kwa Afrika kaskazini na magharibi. Kwa upande wa nchi za SADC Ina maana Morocco wamefuata ushauri wa Henry Kissinger, ikamate Tanzania na mengine yatafuata. Naamini kwa SADC ni Tanzania na Afrika kusini tu. Wanachama wa EAC hawana ubavu huo ukiondoa Tanzania.

Sasa tumemtangazia "njaa" Mfalme. Tunamtegemea "kiuchumi" atufadhili. Hivi utakuwa na msimamo gani dhidi yake? Hivi Mfalme hawezi kusema aungwe mkono kwenye juhudi za kurejea AU? Halafu sharti lake ni kwamba Sahara Magharibi ibakie kuwa sehemu yake.

Tunajua Novemba wakuu wa Afrika wamekaribishwa Morocco. Naamini hakuna sababu ya kujidanganya wala kumung'unya maneno.

Tuseme kuwa tumebadili msimamo na tunaungana na Morocco. Ama baniani mbaya Kiatu chake dawa? Nimeambiwa ni suala la kibiashara ndicho tunachojali. Heee! Hakika hayo?? Tunajidanganya mno.

Tuseme ukweli tumekamatwa tayari. Nadhani pia siyo mbali sana ila siyo sasa, tutawakaribisha Israel, na pengine hata Makaburu wangekuwepo Afrika kusini tungewapa mwaliko.

Mimi yangu ni hayo tu. Na wazo hili ruksa kulibishia.

Wasaalamu. ©Markus Mpangala "Markus M.M


Mchango wetu katika ukombozi wa Afrika unatosha, hivyo si vibaya na sisi sasa tukapiga 'MPUNGA'!

NB: Acha Kenya, Uganda na Rwanda n.k. nao watupokee hili zigo wa wapigania uhuru wa Sahara magharibi!
 
Siku hizi Tz haina msimamo.
Hata Kabila alialikwa juzi.
 
Back
Top Bottom