Kuikumbatia Morocco Tutaumia Baadae!!

Kuikumbatia Morocco Tutaumia Baadae!!

kuna mengi sana ambayo yamekubaliwa ktk MoU hii ambayo serikali imesaini na hawa Morroco lkn tatizo linaonekana ni kuwekwa kipengele cha kujengwa msikiti ndio kimekuwa kiroja,hebu tupunguze chuki toeni taarifa ya makubaliano yote iliyosainiwa.AMESEMA KWELI MZEE MWINYI.
 
Ombaomba anapo nyoosha mkoni na bakuli lake huwa hachagui noti ipi iliyopa ndani ya Wallet ya mtoaji...!!

Kitendo tulichofanya wala sio cha ombaomba. Omba omba huwa anaomba na kupewa bila kutegemea na yeye kutoa kitu. Tulichofanya kwa Morocco ni uchangudoa wa hali ya juu. Tumeombwa na sisi tukaomba ili tutoe - hiyo ndio kanuni ya uchangudoa!
 
Mkuu uko sahihi in some extent
Lakini turudi nyumna, kuna ile mikataba 17 aliyotia sahihi JK kati yetu na China, what's going on kama outcome ya ile mikataba. Tumebaki dumping area for everything from china from construction, manufacturing and importing fast moving consume goods. Tuweweza ku export nini china mpaka wakati huu??? Kumbukeni yule Mwarabu aliyeuziwa eneo kwenye hifadhi ya wanyama kule LOLIONDO mpaka akajenga uwanja wa ndege, do you know WHAT is going on there? Tisa kumi Dangote kafanya kazi kubwa sana ya uwekezaji kule mtwara, baada ya hapo akajenga PORT yake binafsi direct connected na kiwanda chake, do we know what's is going on there?? No maana nasema tusisherekee kupata vya bure ina changamoto zake siku za usoni. The country needs strategic partnership for WIN-WIN, pia tupunguze mwendokasi kufanya mikataba mingi kwa wakti mmoja, test 5 if successfull move foward, ziki bounce zote utafanyeje??//
Mkuu umenikumbusha yule mwarabu wa Loliondo gate. Mikataba ya Mwinyii leo ndiyo watanzania tunasuffer haswa.

Hii mikataba hii, lazima tutumie akili zaidi kuliko mwendokasi otherwise tutaumia sana
 
Hakuna nchi ambayo tunapoikumbatia hatutaumia kama unaijua itaje. Ukishakuwa nchi masikini ni kunyonywa tuu mpaka ufutike kwenye huu uso wa dunia
Tunaendekeza ujinga wetu na kujidai tunajua wakati hatujui.

Kaa chini na watanzania wenzako shirikisha akili zote mtoke na jibu moja zuri lililo jema na afya kwa taifa
 
Serikali ya CCM imekuwa ikiwaaminisha watanzania kuwa wakiichagua CUF italeta waarabu TANZANIA na hivyo UTUMWA utarudi. Hata Bunge la Katiba hiyo Propaganda imetumika kweli kweli! Hivi sasa tuna mgeni, mfalme wa WAKURYA kutoka MOROCCO, hajawahi kuwa mwarabu.
Mtatiro J
 
Mleta mada sijaelewa mantiki yake.Kwa hiyo Magufuri angekataa hiyo zawadi au?
 
Serikali ya CCM imekuwa ikiwaaminisha watanzania kuwa wakiichagua CUF italeta waarabu TANZANIA na hivyo UTUMWA utarudi. Hata Bunge la Katiba hiyo Propaganda imetumika kweli kweli! Hivi sasa tuna mgeni, mfalme wa WAKURYA kutoka MOROCCO, hajawahi kuwa mwarabu.
Mtatiro J

ccm imaongoza kwa siasa za majitaka
 
Suala la uchadema au chama chochote hapa linakujaje waungwana? Mtu katoa maoni yake na ukiyaangalia yana mantiki pia, wengine badala ya kujibu hoja kwa hoja zenye mantiki wanaanza kubeza wenzao kichamachama! Inasikitisha kwa kweli.
Hayana mantiki bali husuda na wivu
 
Katika ulimwengu wa sasa NO FREE LUNCH, Hata mabilionea duniani hawawezi kukupa pesa bure tu pasipokujiuliza impact ya msaada anaokupa labda kwake yeye, jamii inayokuzunguka, majirani zako, na wadau wote kwa ujumla. Kwa hili kukubaliliwa kujengewa uwanja wa mpira na msikiti mkubwa are there the priorities of the nation??? Je zipo kwenye ilani ya chama. Watakonufaika na uwanja na msikiti ni wangapi.

Ni vijiji vingapi havina maji, huduma ya afya, elimu. Vipi swali NYETI la kujenga viwanda ambalo ndo makakati wa nchi kwa ujumla. Bado nina wasiwasi kuwa ahadi ya kufanya hayo hazikuombwa na mkuu wa kaya BALI ni kitu anachohitaji kufanya mfalme mtukufu mgeni katika ardhi yetu kwa agenda binafsi ya kurahisisha baadhi ya mambo amabayo tutajaona siku za usoni.
TUNAJIDANGANYA TU.

Henry Kissinger wakati Fulani alipata kuishauri serikali ya Marekani enzi hizo. Kwamba ukitaka kulikamata bara la Afrika nenda kamweke sawa Julius Nyerere na Tanzania. Ukimweka sawa Nyerere basi ni rahisi kwa mataifa mengine.

KUHUSU MOROCCO
Miaka 32 iliopita tuliwatangazia Morocco msimamo wetu kupinga mabavu yake huko Sahara Magharibi. Tuliwaambia pia waafrika wenzetu.Tuliutangazia ulimwengu wote. Msimamo wetu ulikuwa kuwaunga mkono Sahara Magharibi ili wajitawale.

Miaka 32 baadaye tumeikaribisha Morocco nchini kwa gego na fizi (Hongereni). Tumeketi mezani kuzungumza na Mfalme Mohammed VI (sina hiyana Naye).

Tumemwambia ushirikiano wetu ni diplomasia ya uchumi, demokrasia na mengineyo. Halafu tumemwambia atujengee nyumba ya Ibada na uwanja wa soka huko Dodoma. Vyote amekubali. Sina tatizo na maombi hayo. Tatizo ni kujidanganya kwetu bila soni.

Toka mwezi Januari mwaka huu kuna kampeni kubwa imeshika kasi Morocco irudishiwe uanachama wa AU. Julai 17 mwaka huu kule Kigali, Rwanda, Mfalme Mohammed VI aliandika barua kwenda kwa Mwenyekiti wa AU, Rais Idris Derb kwamba wapewe nafasi yao AU. Akaomba huruma ya wanachama wa AU(kuna mgawanyiko, na naamini pia utazihusisha Anglophone na Francophone).

Morocco imefanikiwa kushawishi baadhi ya wanachama kwa Afrika kaskazini na magharibi. Kwa upande wa nchi za SADC Ina maana Morocco wamefuata ushauri wa Henry Kissinger, ikamate Tanzania na mengine yatafuata. Naamini kwa SADC ni Tanzania na Afrika kusini tu. Wanachama wa EAC hawana ubavu huo ukiondoa Tanzania.

Sasa tumemtangazia "njaa" Mfalme. Tunamtegemea "kiuchumi" atufadhili. Hivi utakuwa na msimamo gani dhidi yake? Hivi Mfalme hawezi kusema aungwe mkono kwenye juhudi za kurejea AU? Halafu sharti lake ni kwamba Sahara Magharibi ibakie kuwa sehemu yake.

Tunajua Novemba wakuu wa Afrika wamekaribishwa Morocco. Naamini hakuna sababu ya kujidanganya wala kumung'unya maneno.

Tuseme kuwa tumebadili msimamo na tunaungana na Morocco. Ama baniani mbaya Kiatu chake dawa? Nimeambiwa ni suala la kibiashara ndicho tunachojali. Heee! Hakika hayo?? Tunajidanganya mno.

Tuseme ukweli tumekamatwa tayari. Nadhani pia siyo mbali sana ila siyo sasa, tutawakaribisha Israel, na pengine hata Makaburu wangekuwepo Afrika kusini tungewapa mwaliko.

Mimi yangu ni hayo tu. Na wazo hili ruksa kulibishia.

Wasaalamu. ©Markus Mpangala "Markus M.M

Israel ana tatizo gani?
 
Vinchi vingi vinavyotaka kujitenga viongozi wake wana uroho wa madaraka.
 
mkuu umenena sawa ila unasahau kuwa ulimwengu wa sasa si wa kuangalia unataka nini,unaangalia unatoa nini,sahara magharibi wanakitu gani cha kuipa TZ ya sasa kuliko hao Morocco,hilo moja ,mbili Kumbuka jana imesainiwa mikataba aidi ya 22 ya ushirikiano katika sekta za kijamii,kiuchumi na kitamaduni pia na mengi imejikita katika suala zima la diplomasia ya kiuchumi sasa huoni hapo bado JPM anaendeleza harakati zake za ndoto ya viwanda?

Tisa kumi,huo uwanja ukijengwa huko Dodoma si wamorocco watao kuja kufanya kazi bali ni ndugu zetu watanzania wenye ujuzi huo wataajiriwa hivyo kupunguza ombwe la ajira kwa kiasi fulani
Huo uwanja ukiisha watafanya nn?Sahara itakuwa inakaliwa bado na Morocco kazi za kibarua ndo tumegeuza msimamo wetu wa muda wote?hata sisi tutaliwa tu kwa huo uwanja wao sio mafala.
 
mliandika humu umuhimu wa diplomasia ya kushirikiana na mataifa ya nje...mkamlaumu JPM hasafiri....sasa ameshawishi ushirikiano na mataifa mnakuja na nyimbo,ujinga ujinga....Huyu aliyefubaza akili ni nani?...kama ni Mbowe au Lowassa mimi ntawasaidia muondokane na minyororo ya ujinga.
Kamgeuka nyerere na waasisi wengine wa AU.moroko hawakufukuzwa walijitoa kwa AU kuunga mkono uhuru wa sahara.
 
Suala la uchadema au chama chochote hapa linakujaje waungwana? Mtu katoa maoni yake na ukiyaangalia yana mantiki pia, wengine badala ya kujibu hoja kwa hoja zenye mantiki wanaanza kubeza wenzao kichamachama! Inasikitisha kwa kweli.
Mkuu asikuumize kichwa huyo mama anavizia u dc ndo maana kila kitu cha serikali anasapoti
 
Uwanja na msikiti vimekuuma sana dah pole ila mwambie queen wa england nae aje kujenga lile kanisa la anglikan hahahaha sijui itakuwaje kuhusu ushoga nawaza tu lakini
 
Back
Top Bottom