Kuikumbatia Morocco Tutaumia Baadae!!

Kuikumbatia Morocco Tutaumia Baadae!!

Siku hizi ukiwa chadema 'ulofa na upumbavu' ndio sifa kuu,Chandimu mliandika humu umuhimu wa diplomasia ya kushirikiana na mataifa ya nje...mkamlaumu JPM hasafiri....sasa ameshawishi ushirikiano na mataifa mnakuja na nyimbo,ujinga ujinga....Huyu aliyefubaza akili ni nani?...kama ni Mbowe au Lowassa mimi ntawasaidia muondokane na minyororo ya ujinga.

Mlisema uyu anafata nyayi za Mwl. Nyerere,imekuaje leo anakiuka yale yaliohasisiwa na Nyerere?
 
Kwanini tuionee huruma Sahara Magharibi wakati Sisi "Tumeikamata" Zanzibar kwa kula za Maruhani?
Kinachotokea huko Morroco na Sahara Magharibi ndio kinachotokea Tanganyika na Zanzibar.Sisi sasa hatuna budi kumkaribisha Mfalme wa Morroco maana sote kuna "Viinchi" tunavitawala.

Nyerere was a typical "Political Diplomat" na ndio maana hakuona sbb ya Tz kuwa huru kabla ya wengine kuwa huru.Kwa sasa tulishaua Azimio la Arusha,tulienda Znz,kule tukasema kila kitu sasa ni ubepari,na bepari huwa hana huruma kwa mnyonge,yeye ni kunyonya tu kama kupe.Tumechagua kuwa mabepari,haya ndio maisha ya ubepari.
 
Siku hizi ukiwa chadema 'ulofa na upumbavu' ndio sifa kuu,Chandimu mliandika humu umuhimu wa diplomasia ya kushirikiana na mataifa ya nje...mkamlaumu JPM hasafiri....sasa ameshawishi ushirikiano na mataifa mnakuja na nyimbo,ujinga ujinga....Huyu aliyefubaza akili ni nani?...kama ni Mbowe au Lowassa mimi ntawasaidia muondokane na minyororo ya ujinga.
Suala la uchadema au chama chochote hapa linakujaje waungwana? Mtu katoa maoni yake na ukiyaangalia yana mantiki pia, wengine badala ya kujibu hoja kwa hoja zenye mantiki wanaanza kubeza wenzao kichamachama! Inasikitisha kwa kweli.
 
Yote kwakuwa umetajwa Msikiti ila lingetajwa Kanisa njemba zingekuja na makala tofauti full mapambio.
 
Katika ulimwengu wa sasa NO FREE LUNCH, Hata mabilionea duniani hawawezi kukupa pesa bure tu pasipokujiuliza impact ya msaada anaokupa labda kwake yeye, jamii inayokuzunguka, majirani zako, na wadau wote kwa ujumla. Kwa hili kukubaliliwa kujengewa uwanja wa mpira na msikiti mkubwa are there the priorities of the nation??? Je zipo kwenye ilani ya chama. Watakonufaika na uwanja na msikiti ni wangapi.

Ni vijiji vingapi havina maji, huduma ya afya, elimu. Vipi swali NYETI la kujenga viwanda ambalo ndo makakati wa nchi kwa ujumla. Bado nina wasiwasi kuwa ahadi ya kufanya hayo hazikuombwa na mkuu wa kaya BALI ni kitu anachohitaji kufanya mfalme mtukufu mgeni katika ardhi yetu kwa agenda binafsi ya kurahisisha baadhi ya mambo amabayo tutajaona siku za usoni.
TUNAJIDANGANYA TU.

Henry Kissinger wakati Fulani alipata kuishauri serikali ya Marekani enzi hizo. Kwamba ukitaka kulikamata bara la Afrika nenda kamweke sawa Julius Nyerere na Tanzania. Ukimweka sawa Nyerere basi ni rahisi kwa mataifa mengine.

KUHUSU MOROCCO
Miaka 32 iliopita tuliwatangazia Morocco msimamo wetu kupinga mabavu yake huko Sahara Magharibi. Tuliwaambia pia waafrika wenzetu.Tuliutangazia ulimwengu wote. Msimamo wetu ulikuwa kuwaunga mkono Sahara Magharibi ili wajitawale.

Miaka 32 baadaye tumeikaribisha Morocco nchini kwa gego na fizi (Hongereni). Tumeketi mezani kuzungumza na Mfalme Mohammed VI (sina hiyana Naye).

Tumemwambia ushirikiano wetu ni diplomasia ya uchumi, demokrasia na mengineyo. Halafu tumemwambia atujengee nyumba ya Ibada na uwanja wa soka huko Dodoma. Vyote amekubali. Sina tatizo na maombi hayo. Tatizo ni kujidanganya kwetu bila soni.

Toka mwezi Januari mwaka huu kuna kampeni kubwa imeshika kasi Morocco irudishiwe uanachama wa AU. Julai 17 mwaka huu kule Kigali, Rwanda, Mfalme Mohammed VI aliandika barua kwenda kwa Mwenyekiti wa AU, Rais Idris Derb kwamba wapewe nafasi yao AU. Akaomba huruma ya wanachama wa AU(kuna mgawanyiko, na naamini pia utazihusisha Anglophone na Francophone).

Morocco imefanikiwa kushawishi baadhi ya wanachama kwa Afrika kaskazini na magharibi. Kwa upande wa nchi za SADC Ina maana Morocco wamefuata ushauri wa Henry Kissinger, ikamate Tanzania na mengine yatafuata. Naamini kwa SADC ni Tanzania na Afrika kusini tu. Wanachama wa EAC hawana ubavu huo ukiondoa Tanzania.

Sasa tumemtangazia "njaa" Mfalme. Tunamtegemea "kiuchumi" atufadhili. Hivi utakuwa na msimamo gani dhidi yake? Hivi Mfalme hawezi kusema aungwe mkono kwenye juhudi za kurejea AU? Halafu sharti lake ni kwamba Sahara Magharibi ibakie kuwa sehemu yake.

Tunajua Novemba wakuu wa Afrika wamekaribishwa Morocco. Naamini hakuna sababu ya kujidanganya wala kumung'unya maneno.

Tuseme kuwa tumebadili msimamo na tunaungana na Morocco. Ama baniani mbaya Kiatu chake dawa? Nimeambiwa ni suala la kibiashara ndicho tunachojali. Heee! Hakika hayo?? Tunajidanganya mno.

Tuseme ukweli tumekamatwa tayari. Nadhani pia siyo mbali sana ila siyo sasa, tutawakaribisha Israel, na pengine hata Makaburu wangekuwepo Afrika kusini tungewapa mwaliko.

Mimi yangu ni hayo tu. Na wazo hili ruksa kulibishia.

Wasaalamu. ©Markus Mpangala "Markus M.M
Mkuu eleza pia huo msimamo wetu (Tanzania) kwa Morocco kwa miaka 32 umeisaidia vipi Sahara magharibi?
 
Kususa tutasusa kwa maneno tu ili kujaribu kuwatishia msuli watoaji ila kiuhalisia baada ya kuwachimba mkwara kwa maneno wao wanakutwangia barua ya kukutembelea na kukupa unacho hitaji hapo ndio ukweli hunapo jitokeza kwa ombaomba huwa mkali anapokuwa na njaa ila si kuwa hapendi kupewa misaada, u
 
Kama tuliweza kumkubali yule jamaa mwenye tuhuma za ufisadi kuwa mgombea urais,unafikiri kuna nini ambalo tutaweza kulikataa tena? Kama wanachi tuko hivyo basi na viongozi wetu wako hivyohivyo.
 
Yote kwakuwa umetajwa Msikiti ila lingetajwa Kanisa njemba zingekuja na makala tofauti full mapambio.
Hahahahaaaa don't be short sighted men!!
Kujengwa kwa misikiti si mra ya kwanza, ukienda butiama Gadafi alijenga msikiti mkubwa pale kijijini nimefika wala si ya kusimuliwa. Kujengwa kwa kanisa au msikiti ni jambo jema, yote ni heri kaka maana itatumiwa na watu, na watu ndo sisi kaka, ni bora tuendeleze misingi aliyotuachia Mwl Nyerere ya kutotambua na kuweka mbele mambo ya ndini kattika mambo ya maendeleo. Hope jammaa umeelewa vizuri
 
Kama tuliweza kumkubali yule jamaa mwenye tuhuma za ufisadi kuwa mgombea urais,unafikiri kuna nini ambalo tutaweza kulikataa tena? Kama wanachi tuko hivyo basi na viongozi wetu wako hivyohivyo.
Watu husema siasa ni mchezo mchafu, ni kweli kwa jinsi mambo yanavyokwenda watu wapo tayari kupoteza utashi kwa maslahi ya jambo fulani. Kwa upande mwingine kama kuna ushahidi wa moja kwa moja kuwa alikuwa fisadi mbona mpaka sasa hakuna hatua yeyote iliyochukuliwa kwake. Yule aliyejenga bandari bagamoyo kulikuwa na mahitaji ya kitaifa kuwa na hiyo bandari, yeye tunamweka kundi lipi? 90% wa wenye madaraka wala element ya ufisadi trust me!
 
mliandika humu umuhimu wa diplomasia ya kushirikiana na mataifa ya nje...mkamlaumu JPM hasafiri....sasa ameshawishi ushirikiano na mataifa mnakuja na nyimbo,ujinga ujinga....Huyu aliyefubaza akili ni nani?...kama ni Mbowe au Lowassa mimi ntawasaidia muondokane na minyororo ya ujinga.
Tuliaminishwa Nyerere mpya kapatikana. Nyerere gani anayelea ujinga Wa mwafrika kumnyanyasa muafrika mwenzake!?
 
mkuu umenena sawa ila unasahau kuwa ulimwengu wa sasa si wa kuangalia unataka nini,unaangalia unatoa nini,sahara magharibi wanakitu gani cha kuipa TZ ya sasa kuliko hao Morocco,hilo moja ,mbili Kumbuka jana imesainiwa mikataba aidi ya 22 ya ushirikiano katika sekta za kijamii,kiuchumi na kitamaduni pia na mengi imejikita katika suala zima la diplomasia ya kiuchumi sasa huoni hapo bado JPM anaendeleza harakati zake za ndoto ya viwanda?

Tisa kumi,huo uwanja ukijengwa huko Dodoma si wamorocco watao kuja kufanya kazi bali ni ndugu zetu watanzania wenye ujuzi huo wataajiriwa hivyo kupunguza ombwe la ajira kwa kiasi fulani

Itakuchukua miaka mingi kumwelewa mleta uzi. Hivi hii miaka 30 tu watu wamesahau POLISARIO? Kweli? Ni upendo gani huu ambao hauna riba? Hivi Morocco kurudishwa AU lazima awe kama anatuhonga? Mnasingizia uchumi, uchumi kwamba kwa sasa Tanzania itapokea msaada wowote bila kujali unatoka wapi na kwa nini umetolewa? Umaskini kitu kibaya sana!!!! Haya hebu tufanye hivi: Je,kwa nini tusimwombe mfalme huyo atusaidie katika huduma ya afya? Atuachie sisi kazi ya kutafuta madawa, lakini kwa hiyo bilioni 80 hadi 100 ajenge wodi za akina mama na hata kuzijaza vitanda? A stadium??? What for!!
 
Kwani hao sahara magharibi wanamsaada gani kwa Tz
 
Kweli sisi tu wavivu kiasi hata cha kushindwa kulala, hatujui hata kitu cha kuomba? Morocco inakuja na mipesa yake, jamani nataka kurudi AU, naomba mnisaidie kushawishi wenzenu. Sisi tukasema sawa tutakusaidia, lakini kwa lipi? Morocco ikajibu lolote nyinyi ombeni! Katika maombi, tukaomba kujengewa msikiti na uwanja wa mpira. Haki ya Mungu!
 
-->>Japo baadhi nayabishia lakini 85% yafanyikayo ni mema kwa dhati./
-->>Sifikiri kama wakijenga uwanja utakuwa wa bure kabisa,au nyumba hapana./ispokuwa msikiti waweza kuwa bureee...!./
•Tujifunze kupambanua mambo/
hawa mostly ni wafanya biashara na wawekezaji short wanataka faida./
 
Itakuchukua miaka mingi kumwelewa mleta uzi. Hivi hii miaka 30 tu watu wamesahau POLISARIO? Kweli? Ni upendo gani huu ambao hauna riba? Hivi Morocco kurudishwa AU lazima awe kama anatuhonga? Mnasingizia uchumi, uchumi kwamba kwa sasa Tanzania itapokea msaada wowote bila kujali unatoka wapi na kwa nini umetolewa? Umaskini kitu kibaya sana!!!! Haya hebu tufanye hivi: Je,kwa nini tusimwombe mfalme huyo atusaidie katika huduma ya afya? Atuachie sisi kazi ya kutafuta madawa, lakini kwa hiyo bilioni 80 hadi 100 ajenge wodi za akina mama na hata kuzijaza vitanda? A stadium??? What for!!
ukiwa na fikra za kupinga kila kitu daima hutaona jema hata moja,mathalani kama ulifuatilia vizuri kilichokuwa kinazungumzwa jana wala leo hii usingekuwa na kwanini zako hizo,kingine sisi watanzania ebu tujifunze kufanya vitu kwa mipango endelevu na sio kwa ajili ya kuridhisha watu,bado nitatetea kuwa JPM jana alisema kuwa uwanja ,msikiti ni baadhi ya vitu vingi ambavyo wameongea na kukubaliana na mflame yule katika kuhakikisha mafaniko yanafikiwa.

Kingine kumbuka Mfalme huyu kaja hapa kwa malengo mawili aua matatu tofauti,moja kuomba kuungwa mkono,pili ni ziara rasmi ya kiserikali ,tatu amekuja kwa ajili ya kutalii ndio maana ataenda na ngorongoro kule.

Ukija katika ziara ya kiserikali ndio utaona kuwa wamesaini mikataba ya ushirikiano zaidi ya 22 na YOTE NI YA kimaendeleo hasa ikilenda diplomasia ya uchumi,theni hilo la kuunwa mkono ni sehemu tu ya ziada katika safari yake
 
Back
Top Bottom