Kuibiwa kwenye Daladala

M
mie nimetapeliwa mara moja na hela yenyewe ni ya nyanya tu.. tangia siku hiyo nipo makini vibaya mnoooo.... mie huwa napoteza vitu na sio kuibiwa
Mimi mara moja mara ya pili huyo mtu huwa akiniona ana badili njia nilimsaka miezi 3 nilipompata tulichomtendea Mungu atusamehe tu kisa laki tano ila aliijutia
 
Niliibiwa mkufu wa dhahabu wakati najiandaa kuteremka kutoka kwenye daladala nilihisi ni panga limekata shingo kumbe ni kofi lililonishtua na jamaa kuambaa na mkufu nikiwa namuona. Ni kitambo kdg miaka ya 90+
Pole sana dada.
Aisee kofi kama panga? Hawa watu hawa kiboko.
 
Mkuu hawatumii dawa ni tekniki tu, ile ukishaishika mara moja weka mfukoni kwako usimrudishie tena wee lipa ela uone kama watakubali, ule mfuko anaoweka ile simu kuna sabuni imefanana vilevile kwa hiyo akitoa mfukoni unaona ndio ile kumbe tayari keshabadilisha.
 
nililizwa kishamba sana, nimekomaa na mmoja kumbe kuna wenhine walinilia mingo ila ndio kujifunza pia.
 
Hii kitu iliwahi kunikuta, haki nilicheka hadi machozi.
 
Washanikosa pale external kituoni wakati wa kupanda daladala la tabata segerea

Nimetoka chuga nikashukia ubungo mataa mida ya usiku nikachomoa wallet nikatoa pesa zote nikaacha ATM card na ID

Nimekaa kituoni daladala ikaja nikaanza kuparangana ili nipande Mara nasikia simu inachomolewa mfukoni

Nikazuia mkono ila kuzuia nasikia kwa nyuma wallet inachomolewa sikua na jinsi kwa sababu mkono mmoja nimeshikilia rasket mwingine nimezuia simu

Ikabidi nivumilie tu wallet ikaenda na wahuni ila pesa hawakupata
 
Dahh walinitoa laki 3 kweny wallet nimetoka kuchukua hesabu ya Jioni ofsn hakika walinibakishia buku niliyoweka kweny mfuko wa shati namshukuru Mungu hyo buku ilinisaidia kwenda nyumbn .

Toka siku hyo sijapanda hais tena kama usafir Wang unashida aheri nichukue Toyo.

Machalii arusha mnatabia mbaya sana ila nishawasamehe.
 
kuna sehemu... mchana wahuni wanapiga tizi.. (mazoezi ya ngumi).. alaf usiku wanakaba.... mie nikawa nimewasoma... kuna siku natoka zangu Maeneo ya kujidai... nipo mwenyewe... mkononi nimeshika kibegi kina pc.. maana nilivyotoka chuo nikapitia maeneo.. sasa ile nakatisha vichochoro saa 6 usiku.. nikakutana na jamaa kama watatu hivi.. hawajashika silaha wala nini.. mie kama kawaida yangu uskiu huwa napasua katikati... ya watu (kama wamekaa kimstari)... sasa ile nakaribia kuwafikia wakasimama... mie sina habari hapo najua wahuni tu na mambo yao... nikashangaa mmoja ananiambia "oya.. unaziweza??? kama hautuwezi tuachie kila kitu ondoka... kama unatuchukulia kinyonge njoo tupambane.."

kucheki.. huku na huko.. kimyaa... sisi tu... nikasema kimoyomoyo leo afe kipa afe beki... kitaeleweka...

nikachukua kibegi changu nikakivaa.. fresh.. (mkono mmoja)... aisee zilipigika ngumi pale..... hahahahahaha narudi nyumbani suruali nimeipasua katikati... kiatu kimabanduka soli.. pc imeweka crack katika kioo.... hahaha daah nimekumbuka mbali..
 
Nimewahi kuvunjiwa chumba ila wizi mwingine wote bado
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…