Kuhusu wachunguzi wa kimataifa: Majibu ya Waziri Mkuu ni final and conclusive. Hawataruhusiwa!

Mjadala wa kuleta wachunguzi kutoka nje labda wahame nchi wakaufanyie KTN TV station na actually zao.
 
Wakati wa harakati za kumzuia asichaguliwe kuwa rais wa TLS Lissu mwenyewe alipata kuandika vizuri tu: the people high up were no longer thinking rationally. Serikali yetu imechagua kutuhumiwa kuliko kweli uchunguzi kufanywa na watu huru!
 
Leo,katika kipindi cha Maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu Bungeni Dodoma,Kiongozi wa Upinzani Bungeni Mhe.Freeman Mbowe alimuuliza Waziri Mkuu,pamoja na mambo mengine,kuhusu wachunguzi wa kimataifa.

Akichagiza swali lake na tukio la kuungua kwa benki kuu ya Tanzania na kuja kwa Scotland Yard hapa nchini kufanya uchunguzi,Mbowe alitaka kujua Serikali inapata kigugumizi gani kuwaruhusu wachunguzi wa kimataifa katika matukio ya utekaji,mauwaji na kushambuliwa kwa watu mbalimbali hapa nchini hasa wanasiasa wa upinzani.

Nikiri,mimi binafsi,swali la Mbowe lilikuwa gumu na la mtego kwa Waziri Mkuu. Lakini,swali la Mbowe lililenga kupata jibu la mwisho ili kufunga mjadala kuhusu kuruhusiwa au kutokuruhusiwa kwa Wachunguzi wa Kimataifa hapa nchini. Jibu la mwisho likatolewa.

Kwa umahiri mkubwa na ubobezi wa kisiasa,Waziri Mkuu alijibu kuwa hadi sasa Serikali ina imani kubwa kwa vyombo vya uchunguzi vya ndani. Akaongeza kuwa Serikali,hadi sasa,haioni haja ya kuruhusu Wachunguzi wa Kimataifa kwakuwa vyombo vyetu vya ndani vina uwezo na Serikali ina imani navyo. Akamaliza kwa kusema kuwa kama vyombo vya ndani vitaona havina uwezo,vitatoa taarifa kwa umma!

Hakika,jibu la Waziri Mkuu lilikuwa la umakini mkubwa na lililofunga mjadala. Haiwezekani vyombo vya uchunguzi vya ndani kusema havina uwezo. Kamwe! Pia,haiwezekani Serikali iseme haina imani na uwezo wa vyombo vya ndani. Ndiyo kusema,jibu la Waziri Mkuu ni final and conclusive. Ni wazi kuwa Wachunguzi wa Kimataifa hawaruhusiwa nchini na Serikali hii kwakuwa haja haionekani!
Link Hivi Ndivyo Tukio la kushambuliwa Tundu Lissu Limeharibu Heshima Ya Tanzania
 
Kama wanaamini vyombo vya nje ndo vnaweza kumudu uchunguzi, bas hatuna imani tena na upinzani Wa ndani, tuletewe upinzani wa nje kupambana na CCM!

Ciao!
 
Kama ana imani na vyombo vyake vya ulinzi na usalama angejibu pia tangu tukio litokee wamefikia wapi na vipi watuhumiwa wamesha kamatwa?
Kwann wasingeanzia kwa yule aliyemtolea nape bastola inaweza kuwa ni mtandao mmoja unaofanya uhalifu....au na yule hakuonekana? Vip nape hakumwona?, kitenge je ? , au hamorapa? Kwann wasikae na hao watu nliowataja ili waweze kumtambua mtuhumiwa hatae tupate mtandao mzima wa waalifu.
Tangu Ulimboka ang'olewe kucha wamekamata wangapi? Kibanda, Kubenea, Nnape, waliotupa miili baharini mpaka kifika kwa Lisu jibu lipo wapi? Tunauliza Saa Nane yupo wapi?
 
Mkuu huyu jamaa ni Mwanasheria ZWAZWA njaa inamsumbua sana kaamua kusifia kila upuuzi ndani ya Serikali ili aonekane na hivyo kukumbukukwa kwenye teuzi za kila wiki.
Insta-image-2.jpg
 
Leo,katika kipindi cha Maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu Bungeni Dodoma,Kiongozi wa Upinzani Bungeni Mhe.Freeman Mbowe alimuuliza Waziri Mkuu,pamoja na mambo mengine,kuhusu wachunguzi wa kimataifa.
Akichagiza swali lake na tukio la kuungua kwa benki kuu ya Tanzania na kuja kwa Scotland Yard hapa nchini kufanya uchunguzi,Mbowe alitaka kujua Serikali inapata kigugumizi gani kuwaruhusu wachunguzi wa kimataifa katika matukio ya utekaji,mauwaji na kushambuliwa kwa watu mbalimbali hapa nchini hasa wanasiasa wa upinzani.

Nikiri,mimi binafsi,swali la Mbowe lilikuwa gumu na la mtego kwa Waziri Mkuu. Lakini,swali la Mbowe lililenga kupata jibu la mwisho ili kufunga mjadala kuhusu kuruhusiwa au kutokuruhusiwa kwa Wachunguzi wa Kimataifa hapa nchini. Jibu la mwisho likatolewa.

Kwa umahiri mkubwa na ubobezi wa kisiasa,Waziri Mkuu alijibu kuwa hadi sasa Serikali ina imani kubwa kwa vyombo vya uchunguzi vya ndani. Akaongeza kuwa Serikali,hadi sasa,haioni haja ya kuruhusu Wachunguzi wa Kimataifa kwakuwa vyombo vyetu vya ndani vina uwezo na Serikali ina imani navyo. Akamaliza kwa kusema kuwa kama vyombo vya ndani vitaona havina uwezo,vitatoa taarifa kwa umma!

Hakika,jibu la Waziri Mkuu lilikuwa la umakini mkubwa na lililofunga mjadala. Haiwezekani vyombo vya uchunguzi vya ndani kusema havina uwezo. Kamwe! Pia,haiwezekani Serikali iseme haina imani na uwezo wa vyombo vya ndani. Ndiyo kusema,jibu la Waziri Mkuu ni final and conclusive. Ni wazi kuwa Wachunguzi wa Kimataifa hawaruhusiwa nchini na Serikali hii kwakuwa haja haionekani!
Majibu ya PM yametupa picha halisi kuwa serikali inamjua mtu aliyempiga risasi Tundu Lissu.

Hebu na mimi nijaribu kukuuliza "wakili msomi" maswali yafuatayo:-

1. Imekuwaje vyombo vyetu vya ndani vimeshindwa kutukamatia hata mtu mmoja wa kumhoji, licha ya dereva wa Lissu kuwatajia gari iliyofanya unyama ule kuwa ni Nissan nyeupe yenye namba T932AKN??

2. Unyama ule umefanyika mchana kweupe tena kwenye makazi ya wakubwa, huku getini kukiwa na wainzi, ilikuwaje walinzi wakawafungulia wauaji wale, wakafanya unyama ule na hapo hapo walinzi wakawafungulia geti na kutoka na kwenda kusikojulikana??

3. Ilikuwaje camera za CCTV zikang'olewa Mara tu baada ya tukio lile??

Ukiunganisha dots hapo unakuwa ushawafahamu watu waliompiga risasi "beyond reasonable doubts" kuwa ni vyombo vyetu vya ulinzi na usalama!

Ukichanganya na majibu hayo ya PM wala huna haja ya kuumiza tena kichwa!

Kwa hiyo hapo Mbowe yupo sahihi kuwa ili "kitendawili" hiki kifunguke ni lazima kuwapata wapelelezi toka nje ya nchi......OVA
 
Mbowe aache kubwabwaja ni dhahiri kashikwa pabaya, tukileta hivyo vyombo vya nje kutoka hapo Nairobi vichunguze michango ilitumika vipi ataumbuka.
Ukimuangalia mshambuliaji Lissu hali yake kimwili sasa haina neema kabisa.
M/kiti kakomba kila kitu na kuondoka kuwaachia familia majanga.
Michango ile zaidi ya mil 300 ingemfikia mlengwa mpk sasa tungeongea mengine.
Kufa kufaana.
 
Hili suala nadhani tuliache tu....... Hasa kwa vile bado "tuna imani na vyombo vyetu vya uchunguzi"
 
Suala la Lissu halitakufa kirahisi inaweza kuwa wakati wa utawala huu au wa baadaye lakini lazima kuna mtu atakuja kuumbuka hata baada ya Miaka 20!
It's true

Wacha wajidanganye tu kutokana na kiburi na ulevi wa madaraka unaowakabili.

Lakini wakumbuke kuwa ipo mahakama ya kimataifa iitwayo ICC iliyopo kule The Hague, ambayo inaweza kusikiliza shauri hili
 
Huwezi kukosa imani na wanaokulinda na kama ukifanya hivyo basi kunakua hakuna haja ya hao walinzi wako kuapo.
 
Mbowe aache kubwabwaja ni dhahiri kashikwa pabaya, tukileta hivyo vyombo vya nje kutoka hapo Nairobi vichunguze michango ilitumika vipi ataumbuka.
Ukimuangalia mshambuliaji Lissu hali yake kimwili sasa haina neema kabisa.
M/kiti kakomba kila kitu na kuondoka kuwaachia familia majanga.
Michango ile zaidi ya mil 300 ingemfikia mlengwa mpk sasa tungeongea mengine.
Kufa kufaana.
Ulichoongea wewe ni Pumba Plus!
 
Back
Top Bottom