Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,197
- 25,517
Leo,katika kipindi cha Maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu Bungeni Dodoma,Kiongozi wa Upinzani Bungeni Mhe.Freeman Mbowe alimuuliza Waziri Mkuu,pamoja na mambo mengine,kuhusu wachunguzi wa kimataifa.
Akichagiza swali lake na tukio la kuungua kwa benki kuu ya Tanzania na kuja kwa Scotland Yard hapa nchini kufanya uchunguzi,Mbowe alitaka kujua Serikali inapata kigugumizi gani kuwaruhusu wachunguzi wa kimataifa katika matukio ya utekaji,mauwaji na kushambuliwa kwa watu mbalimbali hapa nchini hasa wanasiasa wa upinzani.
Nikiri,mimi binafsi,swali la Mbowe lilikuwa gumu na la mtego kwa Waziri Mkuu. Lakini,swali la Mbowe lililenga kupata jibu la mwisho ili kufunga mjadala kuhusu kuruhusiwa au kutokuruhusiwa kwa Wachunguzi wa Kimataifa hapa nchini. Jibu la mwisho likatolewa.
Kwa umahiri mkubwa na ubobezi wa kisiasa,Waziri Mkuu alijibu kuwa hadi sasa Serikali ina imani kubwa kwa vyombo vya uchunguzi vya ndani. Akaongeza kuwa Serikali,hadi sasa,haioni haja ya kuruhusu Wachunguzi wa Kimataifa kwakuwa vyombo vyetu vya ndani vina uwezo na Serikali ina imani navyo. Akamaliza kwa kusema kuwa kama vyombo vya ndani vitaona havina uwezo,vitatoa taarifa kwa umma!
Hakika,jibu la Waziri Mkuu lilikuwa la umakini mkubwa na lililofunga mjadala. Haiwezekani vyombo vya uchunguzi vya ndani kusema havina uwezo. Kamwe! Pia,haiwezekani Serikali iseme haina imani na uwezo wa vyombo vya ndani. Ndiyo kusema,jibu la Waziri Mkuu ni final and conclusive. Ni wazi kuwa Wachunguzi wa Kimataifa hawaruhusiwa nchini na Serikali hii kwakuwa haja haionekani!