Kuhusu shambulizi la Sri Lanka

Kuhusu shambulizi la Sri Lanka

Na.Dr.Omar Ali.

Nataka niandike kwa upana kuhusu mauaji ya sri lanka na kutuhumiwa waislamu ila muda hauruhusu
ila kiufupi tu niseme kuwa:

-Waliofanya vitendo hivyo wawe ni waislam au wawe dini yeyote ile,ni vitendo visivyokubalika katika jamii yeyote ulimwenguni,na uislam uko mbali na mafundisho hayo.

-Uislam umekataza kuadhibu mtu yeyote asie na hatia,na ndio maana mtume saw alipokuwa anapeleka jeshi vitani lazma awaambie yafuatayo:
musishambulie makazi ya watu,musiue vichanga wala wanawake,na musipigane na mtu ambae hajanyanyua silaha dhidi yenu.

-Ikiwa hoja ni kuwa wanalipiza kisasi cha waislam waliouliwa New Zealand,haya ni makosa,kwani uislam umeruhusu kisasi lakini ukaweka sharti maalumu:

Kwanza kifanywe kupitia wenye mamlaka ili kuepusha kujichukulia hatua mkononi.

Pili,Masuala muhimu yote ya kimahakama yapite.

Tatu wafanyiwe kisasi watu waliofanya uovu ili iwe fundisho kwa wengine na kupunguza jinai katika jamii.

Sasa kwenda kuvamia jamii nyengine isiyohusika,japo wanafanana kiimani na waliotenda jinai la mwanzo,ni makosa kwani uislam mafunzo yake hayako hivyo.

Wito kwa wasio kuwa waislam.
-Msichukulie makosa ya waislam wanayofanya kuwa ndio uislam ndivyo ulivyo,kwani wakosefu wapo katika kila aina ya watu.

-Kutofautiana kiimani isiwe ugomvi,uislam haumlazimishi mtu kuwa muislam,Mtume saw alichinja mbuzi akausia apelekewe jirani yake myahudi.

-Waislam na wakristo tumeshirikiana katika mambo ya kijamii miaka mingi sana,pasi kufanyiana ubaya,ukitoa dhulma ya watawala dhidi ya jamii fulani katika nchi zetu.

-Zanzibar ni jamii yenye waislam 99% lakini kanisa la kwanza Afrika mashariki limejengwa Zanzibar na halijawahi kufanyiwa uadui wowote na wazanzibari,bali pakitokea dharura kama vile moto basi waislam ndio wa kwanza kushiriki kuuzima ili kuokoa roho za watu.

-Matukio kama haya yasifanye tuchukiane,tushutumiane,maana mwanaadamu hajitoshelezi peke yake,ukiangalia mitaani tunakoishi wake zetu wakienda masokoni watoto huwaacha kwa majirani wakicheza bila kujali dini zao,hujali zaidi maelewano yao na zile familia,sasa je tukichukiana vizazi vyetu vitakuwa salama?

-Uislam ni dini inayofundisha mahusiano mema na dini nyegine na ndio maana imekataza kutukana dini nyengine rejea surat an-aam aya ya 108.

HITIMISHO.
Kwa sie tuliosoma criminology kidogo na criminal psycology,tunajifunza kuwa:
Tabia za kupenda,kuchukia,kujali,kufanya uhalifu,ni tabia za kimaumbile mtu yeyote anaweza kuwa nazo,na ni tabia ya kiasili mtu huzaliwa nayo,atabadilika kulingana na malezi na ataendelea nayo pia kulingana na malezi.

Mimi kama muislam ninayejitambua na ninayejali haki ya kuishi ya kila mtu,nalaani vikali matukio kama haya ya kigaidi yafanywe na mtu yeyote yule.

Gaidi sio mhalifu,bali ni gaidi,kwa hiyo tuache double standard ya kupunguza makali ya ugaidi na kumwita mhalifu pale anapokua upande wako.

Usimuhurumie gaidi eti kwa sababu muna mahusiano nae,hao kwa wayatendayo wako mbaali kabisa na wewe kama wewe ni mtu mwema katika jamii yako.

Serikali ziache kuwapachikia ugaidi wale wasiowapenda simply kwa sababu wamewapinga katika mambo fulani fulani,kwani hali kama hizi zinaweza kusababisha machafuko katika jamii.

Watuhumiwa wowote ambao wako katika majela,kesi zao ziharakishwe ili wakipatwa na hatia wakatumikie vifungo vyao ili wajutie kwa waliyoyafanya,kuendelea kuwashikilia bila sababu maalum ni dhulma kubwa ambayo inaweza kusababisha taharuki katika jamii zao na kuhofiwa watu wanaowaheshimu kubeba chuki na hatimae kuleta machafuko.
Mwenendo wa makosa ya jinai unaeleza kuwa"mtuhumiwa ataendelea kuwa hana hatia mpaka atakapotiwa hatiani"
Sasa basi wanaowashikilia waepuke kuwafanyia ubaya wowote watu wasio na hatia.
Nchi nyingi leo zilizoingia kwenye machafuko sababu kubwa ni utawala usio wa haki,na kuwatia korokoroni pasi na haki viongozi wanaoheshimika katika jamii,na kukuza chuki katika vifua vya wafuasi wao.
Chuki ikizidi haina macho,Mungu atunusuru.
Naomba nisiandike mengi niwatakie mchana mwema na nawapenda sana[emoji7][emoji7][emoji7].
Km Muhammad wenu alikuwa na Jeshi na aliamrisha amri mbalimbali .Basi leo tusishangae hawa magaidi wanaopigania dini kwa kujilipua. sababu hata kiongozi wao alitafuta wafuasi wapya wa dini yake tukufu kwa mtutu na mapanga . Ila yesu kristo hakutumia Jeshi km Muhammad
 
mosi kiswahili hujui,

Pili quraan haikushuka kwa kiswahili,tatu soma quraan yote siyo unaokota aya mtandaoni unakuja mbio

Ninavyo fahamu Madhumuni ya kushuka Quran, acha Quran yenyewe iseme...umebakia Hujui Hujui huku husemi wapi sivyo! Sasa unanishauri nisome yoote nakushangaa wakati Quran yenyewe haikushuka yooote ila aya kwa na sehemu ilipo shuka na sababu ya kushuka na jinsi MTUME alivyo fundisha!
IMG_20190426_170833_125.jpeg
 
Kwahy unataka kusema hizo aya hazitumiki tena! !
ni wasiokuwa waislam ambao walikuwa wanapiga vita uislam wakati uislam ndio ulikuwa na dola,na walikataa kulipa kodi,ila wakristo wote waliokubali kulipa kodi(jizya)walikuwa wako chini ya ulinzi wa waislam,kuanzia mali zao na kila kitu.
 
Huyu mtoa post nina shaka na imaan yake ya tauheed, aina hii ndo wale wanaosema rasulullah baada ya kurudi badr alisema hakuna jihad tena baada ya hii bimana kuna jihad nafsi subhallah hua sipendi kujadili mambo ya kidini humu ila kwa hili na hizo hoja zako hapo juu hatutavumilia
 
Nyamaza kimya kwa kumuogopa allah maana utakuja ulizwa juu ya hiki ulichokitolea ufafanuzi ili khali haujui kitu
 
Huyu mtoa post nina shaka na imaan yake ya tauheed, aina hii ndo wale wanaosema rasulullah baada ya kurudi badr alisema hakuna jihad tena baada ya hii bimana kuna jihad nafsi subhallah hua sipendi kujadili mambo ya kidini humu ila kwa hili na hizo hoja zako hapo juu hatutavumilia
"Uislam umekataza kuadhibu mtu yeyote asie na hatia......."
Kwahyo kama amekosea inahuruhusiwa kuua?
 
Back
Top Bottom