Kuhusu shambulizi la Sri Lanka

Kuhusu shambulizi la Sri Lanka

Mashambulio hayo kwenye makanisa tatu pale Sri Lanka, wakati waumini wakiwa kwenye ibada ya siku adhimu kwao ya Pasaka, imeniumiza sana. Hapa hamna kutetea ujangili usio eleweka!. Nimesikitika sana na umwagaji wa damu ya watu wasio kuwa na hatia. Umma ya Waislamu kote duniani lazima ijitokeze kulaani tukio hii ya kinyama, na wasimame bega kwa bega na waathirika kuonyesha umoja na ubinadamu. Pale inapohitajika waislamu watoe msaada ya hali na mali. Wataje magaidi waliojificha muongoni mwao duniani kote.
Watu wengi wamepoteza maisha, Mungu awalaze mahali pema peponi! Watu wengi wamejeruhiwa, Mungu awapone! Watu wengi wameathirika kiuchumi, Mungu awapunguzie makali. Amen.
Usitegemee siku Waislam au Viongozi wao wakajitokeza mbele ya Vyombo vya habari na kuanza kulaini kuhusu Ugaidi.......coz vinavyotokea vimeagizwa na Mohammed! Na wao hawawezi kwenda kinyume na mafundisho......
 
Mambo ya imani magumu sana kwa kweli binafsi yangu nachukia violence ya aina yeyote ile na hawa wanaofanyaga haya mambo sijui wanakuwa na shida gani kichwani hivi inakuwaje unamdhuru mtu ambaye hana mapigano na mapambano na wewe
 
Mkuu, tafadhali acha kujidanganya. Ni kundi la waislamu yenye msimamo mkali - National Tawheed Jamaat iliyohusika na shambulio!!

Mkuu, tafadhali acha kujidanganya. Ni kundi la waislamu yenye msimamo mkali - National Tawheed Jamaat iliyohusika na shambulio!!

Lete ushahidi unao thibitisha hayo uyasemayo sio meneno bila ushahidi itakuwa ni kubwabwaja tu.
 
Usitegemee siku Waislam au Viongozi wao wakajitokeza mbele ya Vyombo vya habari na kuanza kulaini kuhusu Ugaidi.......coz vinavyotokea vimeagizwa na Mohammed! Na wao hawawezi kwenda kinyume na mafundisho......

Viongozi kadha ya nchi ya Kiislamu - Iran, Pakistan wamejitokeza kulaani tukio hili. Halafu unakosea vibaya kumlaumu Mtume Mohammed SAW, yeye na mafundisho yake yako mbali sana na ukatili. Watu wenye agenda zao wamehijack uislamu na kuiletea sifa mbaya. Waislamu wanatakiwa kuwaexpose hawa watu wenye nia mbaya wanaoharibu uislamu!
 
Lete ushahidi unao thibitisha hayo uyasemayo sio meneno bila ushahidi itakuwa ni kubwabwaja tu.

Pitia BBC, wameeleza story nzima. Waziri Mkuu wa Sri Lanka alitamka bungeni kuwa mashambulio yalifanywa na kikundi ya kiislamu yenye msimamo mkali, ili kulipiza kisasi ya pale NZ pamoja na sababu zingine.
 
Kunya anye kuku akinya bata kaarisha nakifikiria wale matabilii waliouwa msikitini mafia Tanzania na shekhe aliyehisiwa jambazi na kuuwa na polisi mpaka ndugu wakataka kususa maiti yake lisha ya mbunge wao kulisemea bungeni hakuna MTU hata mmoja aliyelaani
 
Sema waislamu wamechelewa sana tena sana kushutumu mauaji yanayofanyika kwa jina la huyo mtume na Mungu wao. Nakumbuka waislamu walishangilia sana septemba 11 na pia walipiga vigelegele mauaji ya Dsm na Nairobi, na kibaya wameendelea bila kukanusha kuwa muislamu akiua mkristu au dini yeyote anapata zawadi ya ma bikra 100 huko ahera hivyo anaenjoy uroda mpaka basi, na ndiyo maana unakuta vijana wadogo wanaona bora wajitunze waue watu waende ahera wakavinjari vimwana

Katik masuala ya serious kama haya ya uhai wa binaadamu usilete maneno ya jikoni,September 11 ni vita kati ya Muarabu na mwamerika hawa walikuwa wa kiwindana na ndio maana balozi zilizo shambuliwa ni za waamerika tu kwanini wasishambuliwe taifa jingine kwani wamerika ndio wakristu tu kama hoja ni ukristo?
Na alieanzisha masuala ya ugaidi ni mwamerika kushsambulia na kukaa nchi za waarabu kwa mabavu. Na kama wewe unafuaatilia masuala haya kwa akili timamu, mpaka leo kampuni ilojenga ile minara ya world shoping centre inaamini kwa ushahidi wa wazi kabisa yale majengo yaliripuliwa na serikali ya Amerika sio Osama, kwa serikali kushindwa kutoa majibu ya maswali 15 yalio ulizwa na kampuni kuhusu mripuko wa kuteketeza mjengo yale namna ile,
Nia ya kuyaripua majengo ni kutafuta au kuhalilisha kuipiga Afaghanistani na nchi zingine za kiarabu na kweli kaharibu maisha ktk nchi nyingi za kiarabu,
 
Pitia BBC, wameeleza story nzima. Waziri Mkuu wa Sri Lanka alitamka bungeni kuwa mashambulio yalifanywa na kikundi ya kiislamu yenye msimamo mkali, ili kulipiza kisasi ya pale NZ pamoja na sababu zingine.

Pitia BBC, wameeleza story nzima. Waziri Mkuu wa Sri Lanka alitamka bungeni kuwa mashambulio yalifanywa na kikundi ya kiislamu yenye msimamo mkali, ili kulipiza kisasi ya pale NZ pamoja na sababu zingine.

Wewe. !!! upuuzi huo tuache kuwa na akili ya kicheche kweli mauwaji yafanyike NZ kisase kifanyike Siri Lanka inaingia akilini au ni kupagawa kwa huyo waziri, sasa hivi upuuzi na ukatili na unyama utakapo fanyika popote pale kwa kulipizana visase vya kukandamizana ktk utawala wenyewe kwa wenyewe, jibu la haraka haraka rahisi tu waislam hao bila uchunguzi wa kina bila ushahidi wa kutosha maana uislam ndio escaping goat wa kila ovu.
 
huo unaojua ww uko vipi?lete mafundisho usilete matendo,maana hata wale waliowaua waislam new zealand ni wakristo,je ukristo ndivyo ulivyofundisha vile?
tiririka
Hamna kutiririka hapa msg deriver. Asante.
 
Hicho ulicho nakili hapo ni nini nyie mnapotezana hakuna aya ya quran ina anza nahicho ulicho andika
أتلوا الذين
hi nini sasa ,au ndio quran yenu mnayo jitungia?
Tuwekee suratul tawba aya ya.29 wanaJamvi wasome Mkuu!
 
Na.Dr.Omar Ali.

Nataka niandike kwa upana kuhusu mauaji ya sri lanka na kutuhumiwa waislamu ila muda hauruhusu
ila kiufupi tu niseme kuwa:

-Waliofanya vitendo hivyo wawe ni waislam au wawe dini yeyote ile,ni vitendo visivyokubalika katika jamii yeyote ulimwenguni,na uislam uko mbali na mafundisho hayo.

-Uislam umekataza kuadhibu mtu yeyote asie na hatia,na ndio maana mtume saw alipokuwa anapeleka jeshi vitani lazma awaambie yafuatayo:
musishambulie makazi ya watu,musiue vichanga wala wanawake,na musipigane na mtu ambae hajanyanyua silaha dhidi yenu.

-Ikiwa hoja ni kuwa wanalipiza kisasi cha waislam waliouliwa New Zealand,haya ni makosa,kwani uislam umeruhusu kisasi lakini ukaweka sharti maalumu:

Kwanza kifanywe kupitia wenye mamlaka ili kuepusha kujichukulia hatua mkononi.

Pili,Masuala muhimu yote ya kimahakama yapite.

Tatu wafanyiwe kisasi watu waliofanya uovu ili iwe fundisho kwa wengine na kupunguza jinai katika jamii.

Sasa kwenda kuvamia jamii nyengine isiyohusika,japo wanafanana kiimani na waliotenda jinai la mwanzo,ni makosa kwani uislam mafunzo yake hayako hivyo.

Wito kwa wasio kuwa waislam.
-Msichukulie makosa ya waislam wanayofanya kuwa ndio uislam ndivyo ulivyo,kwani wakosefu wapo katika kila aina ya watu.

-Kutofautiana kiimani isiwe ugomvi,uislam haumlazimishi mtu kuwa muislam,Mtume saw alichinja mbuzi akausia apelekewe jirani yake myahudi.

-Waislam na wakristo tumeshirikiana katika mambo ya kijamii miaka mingi sana,pasi kufanyiana ubaya,ukitoa dhulma ya watawala dhidi ya jamii fulani katika nchi zetu.

-Zanzibar ni jamii yenye waislam 99% lakini kanisa la kwanza Afrika mashariki limejengwa Zanzibar na halijawahi kufanyiwa uadui wowote na wazanzibari,bali pakitokea dharura kama vile moto basi waislam ndio wa kwanza kushiriki kuuzima ili kuokoa roho za watu.

-Matukio kama haya yasifanye tuchukiane,tushutumiane,maana mwanaadamu hajitoshelezi peke yake,ukiangalia mitaani tunakoishi wake zetu wakienda masokoni watoto huwaacha kwa majirani wakicheza bila kujali dini zao,hujali zaidi maelewano yao na zile familia,sasa je tukichukiana vizazi vyetu vitakuwa salama?

-Uislam ni dini inayofundisha mahusiano mema na dini nyegine na ndio maana imekataza kutukana dini nyengine rejea surat an-aam aya ya 108.

HITIMISHO.
Kwa sie tuliosoma criminology kidogo na criminal psycology,tunajifunza kuwa:
Tabia za kupenda,kuchukia,kujali,kufanya uhalifu,ni tabia za kimaumbile mtu yeyote anaweza kuwa nazo,na ni tabia ya kiasili mtu huzaliwa nayo,atabadilika kulingana na malezi na ataendelea nayo pia kulingana na malezi.

Mimi kama muislam ninayejitambua na ninayejali haki ya kuishi ya kila mtu,nalaani vikali matukio kama haya ya kigaidi yafanywe na mtu yeyote yule.

Gaidi sio mhalifu,bali ni gaidi,kwa hiyo tuache double standard ya kupunguza makali ya ugaidi na kumwita mhalifu pale anapokua upande wako.

Usimuhurumie gaidi eti kwa sababu muna mahusiano nae,hao kwa wayatendayo wako mbaali kabisa na wewe kama wewe ni mtu mwema katika jamii yako.

Serikali ziache kuwapachikia ugaidi wale wasiowapenda simply kwa sababu wamewapinga katika mambo fulani fulani,kwani hali kama hizi zinaweza kusababisha machafuko katika jamii.

Watuhumiwa wowote ambao wako katika majela,kesi zao ziharakishwe ili wakipatwa na hatia wakatumikie vifungo vyao ili wajutie kwa waliyoyafanya,kuendelea kuwashikilia bila sababu maalum ni dhulma kubwa ambayo inaweza kusababisha taharuki katika jamii zao na kuhofiwa watu wanaowaheshimu kubeba chuki na hatimae kuleta machafuko.
Mwenendo wa makosa ya jinai unaeleza kuwa"mtuhumiwa ataendelea kuwa hana hatia mpaka atakapotiwa hatiani"
Sasa basi wanaowashikilia waepuke kuwafanyia ubaya wowote watu wasio na hatia.
Nchi nyingi leo zilizoingia kwenye machafuko sababu kubwa ni utawala usio wa haki,na kuwatia korokoroni pasi na haki viongozi wanaoheshimika katika jamii,na kukuza chuki katika vifua vya wafuasi wao.
Chuki ikizidi haina macho,Mungu atunusuru.
Naomba nisiandike mengi niwatakie mchana mwema na nawapenda sana[emoji7][emoji7][emoji7].
Shukrani Sana mkuu umenena mema sana
 
ni wasiokuwa waislam ambao walikuwa wanapiga vita uislam wakati uislam ndio ulikuwa na dola,na walikataa kulipa kodi,ila wakristo wote waliokubali kulipa kodi(jizya)walikuwa wako chini ya ulinzi wa waislam,kuanzia mali zao na kila kitu.

Nimeuliza walio agizwa watekeleze hilo Agizo! Hicho ulicho post NI maneno yako Mkuu! Lakini Allah kwa kinywa cha MTUME Muhammad Ameagiza ref Suratul Tawba aya ya.30 ...na ukisoma ayat inayo fuata Allah anamuomba Mwenyezi MUNGU Awaangamize WAKRISTO na Wayahudi...
IMG_20190423_144735_159.jpeg
IMG_20190423_175904_489.jpeg
 
Wewe. !!! upuuzi huo tuache kuwa na akili ya kicheche kweli mauwaji yafanyike NZ kisase kifanyike Siri Lanka inaingia akilini au ni kupagawa kwa huyo waziri, sasa hivi upuuzi na ukatili na unyama utakapo fanyika popote pale kwa kulipizana visase vya kukandamizana ktk utawala wenyewe kwa wenyewe, jibu la haraka haraka rahisi tu waislam hao bila uchunguzi wa kina bila ushahidi wa kutosha maana uislam ndio escaping goat wa kila ovu.

Kwanza, please sio escaping goat ni scape goat!

Kulipiza kisasi ya yale ya NZ pale Sri Lanka wanaiona ni kitu sawa kwa sababu Waislamu ni umma mmoja na wanatetea waislamu ndugu zao! Halafu bado wanachunguza kuwa kuna msaada yametoka kutoka makundi makubwa kama IS na Al Qeada! Hii ya kulipua watu wakiwa kwenye ibada ni kitu cha kawaida pale Pakistan, Afghanistan na Misri. Wakati hawaoni dhambi ya kuuwa waislamu wenzio msikitini, kuua wakristo makanisani itakuwa dhambi kwao kweli????
 
Tuwekee suratul tawba aya ya.29 wanaJamvi wasome Mkuu!

Tuwekee suratul tawba aya ya.29 wanaJamvi wasome Mkuu!

Hakuna haja ya kuweka sura hiyo ya 9, quran huwa inajitafsiri yeyenyewe hiyo aya ya 29 wanaotakiwa kupigwa ni hawa Allah aliowataja ktk sura ya 2 aya ya 190. Sasa tuliza akili ulinganishe ni ipi aya ilio tangulia kushuka kati ya iliomu sura ya 9 na ilomo sura ya 2? Unapo taka kuleta ushahidi wa quran nilazima uifahamu kwanza quran nyewe sio kupiga picha aya na kuposti,
IMG_20190423_183012_162.JPG
 
Hakuna haja ya kuweka sura hiyo ya 9, quran huwa inajitafsiri yeyenyewe hiyo aya ya 29 wanaotakiwa kupigwa ni hawa Allah aliowataja ktk sura ya 2 aya ya 190. Sasa tuliza akili ulinganishe ni ipi aya ilio tangulia kushuka kati ya iliomu sura ya 9 na ilomo sura ya 2? Unapo taka kuleta ushahidi wa quran nilazima uifahamu kwanza quran nyewe sio kupiga picha aya na kuposti,View attachment 1079344
Walio Agizwa na Allah kupiga ni kina nani? mkuu na sababu za kupigwa amesha ziainisha hizo hapo chini...nifundishe Mkuu!
IMG_20190423_144735_159.jpeg
IMG_20190423_193131_488.jpeg
 
Wewe. !!! upuuzi huo tuache kuwa na akili ya kicheche kweli mauwaji yafanyike NZ kisase kifanyike Siri Lanka inaingia akilini au ni kupagawa kwa huyo waziri, sasa hivi upuuzi na ukatili na unyama utakapo fanyika popote pale kwa kulipizana visase vya kukandamizana ktk utawala wenyewe kwa wenyewe, jibu la haraka haraka rahisi tu waislam hao bila uchunguzi wa kina bila ushahidi wa kutosha maana uislam ndio escaping goat wa kila ovu.
Unatumia nguvu nyingi sana kuutetea uislamu
 
Back
Top Bottom