Kuhusu shambulizi la Sri Lanka

Kuhusu shambulizi la Sri Lanka

albuluushiy

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2013
Posts
1,404
Reaction score
687
Na.Dr.Omar Ali.

Nataka niandike kwa upana kuhusu mauaji ya sri lanka na kutuhumiwa waislamu ila muda hauruhusu
ila kiufupi tu niseme kuwa:

-Waliofanya vitendo hivyo wawe ni waislam au wawe dini yeyote ile,ni vitendo visivyokubalika katika jamii yeyote ulimwenguni,na uislam uko mbali na mafundisho hayo.

-Uislam umekataza kuadhibu mtu yeyote asie na hatia,na ndio maana mtume saw alipokuwa anapeleka jeshi vitani lazma awaambie yafuatayo:
musishambulie makazi ya watu,musiue vichanga wala wanawake,na musipigane na mtu ambae hajanyanyua silaha dhidi yenu.

-Ikiwa hoja ni kuwa wanalipiza kisasi cha waislam waliouliwa New Zealand,haya ni makosa,kwani uislam umeruhusu kisasi lakini ukaweka sharti maalumu:

Kwanza kifanywe kupitia wenye mamlaka ili kuepusha kujichukulia hatua mkononi.

Pili,Masuala muhimu yote ya kimahakama yapite.

Tatu wafanyiwe kisasi watu waliofanya uovu ili iwe fundisho kwa wengine na kupunguza jinai katika jamii.

Sasa kwenda kuvamia jamii nyengine isiyohusika,japo wanafanana kiimani na waliotenda jinai la mwanzo,ni makosa kwani uislam mafunzo yake hayako hivyo.

Wito kwa wasio kuwa waislam.
-Msichukulie makosa ya waislam wanayofanya kuwa ndio uislam ndivyo ulivyo,kwani wakosefu wapo katika kila aina ya watu.

-Kutofautiana kiimani isiwe ugomvi,uislam haumlazimishi mtu kuwa muislam,Mtume saw alichinja mbuzi akausia apelekewe jirani yake myahudi.

-Waislam na wakristo tumeshirikiana katika mambo ya kijamii miaka mingi sana,pasi kufanyiana ubaya,ukitoa dhulma ya watawala dhidi ya jamii fulani katika nchi zetu.

-Zanzibar ni jamii yenye waislam 99% lakini kanisa la kwanza Afrika mashariki limejengwa Zanzibar na halijawahi kufanyiwa uadui wowote na wazanzibari,bali pakitokea dharura kama vile moto basi waislam ndio wa kwanza kushiriki kuuzima ili kuokoa roho za watu.

-Matukio kama haya yasifanye tuchukiane,tushutumiane,maana mwanaadamu hajitoshelezi peke yake,ukiangalia mitaani tunakoishi wake zetu wakienda masokoni watoto huwaacha kwa majirani wakicheza bila kujali dini zao,hujali zaidi maelewano yao na zile familia,sasa je tukichukiana vizazi vyetu vitakuwa salama?

-Uislam ni dini inayofundisha mahusiano mema na dini nyegine na ndio maana imekataza kutukana dini nyengine rejea surat an-aam aya ya 108.

HITIMISHO.
Kwa sie tuliosoma criminology kidogo na criminal psycology,tunajifunza kuwa:
Tabia za kupenda,kuchukia,kujali,kufanya uhalifu,ni tabia za kimaumbile mtu yeyote anaweza kuwa nazo,na ni tabia ya kiasili mtu huzaliwa nayo,atabadilika kulingana na malezi na ataendelea nayo pia kulingana na malezi.

Mimi kama muislam ninayejitambua na ninayejali haki ya kuishi ya kila mtu,nalaani vikali matukio kama haya ya kigaidi yafanywe na mtu yeyote yule.

Gaidi sio mhalifu,bali ni gaidi,kwa hiyo tuache double standard ya kupunguza makali ya ugaidi na kumwita mhalifu pale anapokua upande wako.

Usimuhurumie gaidi eti kwa sababu muna mahusiano nae,hao kwa wayatendayo wako mbaali kabisa na wewe kama wewe ni mtu mwema katika jamii yako.

Serikali ziache kuwapachikia ugaidi wale wasiowapenda simply kwa sababu wamewapinga katika mambo fulani fulani,kwani hali kama hizi zinaweza kusababisha machafuko katika jamii.

Watuhumiwa wowote ambao wako katika majela,kesi zao ziharakishwe ili wakipatwa na hatia wakatumikie vifungo vyao ili wajutie kwa waliyoyafanya,kuendelea kuwashikilia bila sababu maalum ni dhulma kubwa ambayo inaweza kusababisha taharuki katika jamii zao na kuhofiwa watu wanaowaheshimu kubeba chuki na hatimae kuleta machafuko.
Mwenendo wa makosa ya jinai unaeleza kuwa"mtuhumiwa ataendelea kuwa hana hatia mpaka atakapotiwa hatiani"
Sasa basi wanaowashikilia waepuke kuwafanyia ubaya wowote watu wasio na hatia.
Nchi nyingi leo zilizoingia kwenye machafuko sababu kubwa ni utawala usio wa haki,na kuwatia korokoroni pasi na haki viongozi wanaoheshimika katika jamii,na kukuza chuki katika vifua vya wafuasi wao.
Chuki ikizidi haina macho,Mungu atunusuru.
Naomba nisiandike mengi niwatakie mchana mwema na nawapenda sana[emoji7][emoji7][emoji7].
 
Nina hakika binaadamu anayependa amani ataelewa tanbihi iliyoko kwenye huo ujumbe. Ni maneno mujarabu kwa watu wasio amini kwamba waislamu wanauchukia ugaidi pamoja na vitendo vyote vinavyoambatana na ugaidi.
 
Kwa hakika huo ndio uislamu. Uislamu uko mbali na hizi tabia za ovyo za kuua nafsi zisizo na hatia. Ila nitoe msisitizo tu kwa wachangiaji,huu uzi umesimama vizuri sana kwahiyo watu waje na comment timamu pia. Mtu kama una jazba ni bora ukae kimya usichangie chochote.
 
Mkuu nakuomba unifahamishe hili agizo!; Allah kawaagiza kina nani walitekeleze?! na wasipo litekeleza Allah yupo radhi?
IMG_20190423_144735_159.jpeg
 
Kwenye maandishi uislam ni dini njema sana ila kiuharisia tunadanganyana tu hapa duniani.

Hilo andiko ni zuri sana kwa wasioujua uislam au maboya.

Nitarudi.
 
Wewe umeeleza vizuri bila kua bias, hongeraaaaaa, sasa ngoja wazee wa misuli, vikaoshi ya kaki na yale manusu suruale ya kombati wajee,
asaiv wanakula kashata...
ndio kina nani hao.
 
Mkuu nakuomba unifahamishe hili agizo!; Allah kawaagiza kina nani walitekeleze?! na wasipo litekeleza Allah yupo radhi?View attachment 1079096
ni wasiokuwa waislam ambao walikuwa wanapiga vita uislam wakati uislam ndio ulikuwa na dola,na walikataa kulipa kodi,ila wakristo wote waliokubali kulipa kodi(jizya)walikuwa wako chini ya ulinzi wa waislam,kuanzia mali zao na kila kitu.
 
Kwenye maandishi uislam ni dini njema sana ila kiuharisia tunadanganyana tu hapa duniani.

Hilo andiko ni zuri sana kwa wasioujua uislam au maboya.

Nitarudi.
huo unaojua ww uko vipi?lete mafundisho usilete matendo,maana hata wale waliowaua waislam new zealand ni wakristo,je ukristo ndivyo ulivyofundisha vile?
tiririka
 
Mashambulio hayo kwenye makanisa tatu pale Sri Lanka, wakati waumini wakiwa kwenye ibada ya siku adhimu kwao ya Pasaka, imeniumiza sana. Hapa hamna kutetea ujangili usio eleweka!. Nimesikitika sana na umwagaji wa damu ya watu wasio kuwa na hatia.

Umma ya Waislamu kote duniani lazima ijitokeze kulaani tukio hii ya kinyama, na wasimame bega kwa bega na waathirika kuonyesha umoja na ubinadamu. Pale inapohitajika waislamu watoe msaada ya hali na mali. Wataje magaidi waliojificha muongoni mwao duniani kote.

Watu wengi wamepoteza maisha, Mungu awalaze mahali pema peponi! Watu wengi wamejeruhiwa, Mungu awapone! Watu wengi wameathirika kiuchumi, Mungu awapunguzie makali. Amen.
 
Na wakristo wote ulimwenguni walaani mauaji ya New Zealand,pia wale wavaa yeboyebo walikua kwenye ibada yao,ndomana nmwandishi kaweka angalizo tuache double standard.
 
Na wakristo wote ulimwenguni walaani mauaji ya New Zealand,pia wale wavaa yeboyebo walikua kwenye ibada yao,ndomana nmwandishi kaweka angalizo tuache double standard.
e naam,ila kazi ipo kubwa sana katika kuwafahamisha watu nani ana haki ya kuishi,maana kuna watu wanaona wao wana haki ya kuishi kuliko wengine.
 
Na wakristo wote ulimwenguni walaani mauaji ya New Zealand,pia wale wavaa yeboyebo walikua kwenye ibada yao,ndomana nmwandishi kaweka angalizo tuache double standard.
Yale ya New Zealand yamelaaniwa yapasavyo! Serikali ya NZ ilisimama bega kwa bega na waislamu. Baada ya tukio kile, Waislamu walianza kupata Sympathy na Good Will, ambayo imeanza kupotea tena kwa sababu ya tukio hii ya Sri Lanka.

Halafu, waislamu kadha waliokuwa wanafanya kazi mahotelini wamepoteza maisha bila ya kuwa na hatia. Wameuawa na waislamu wenzio!
 
Yale ya New Zealand yamelaaniwa yapasavyo! Serikali ya NZ ilisimama bega kwa bega na waislamu. Baada ya tukio kile, Waislamu walianza kupata Sympathy na Good Will, ambayo imeanza kupotea tena kwa sababu ya tukio hii ya Sri Lanka.
Tukio la Sri Lanka mpk sasa haijajulikana nani kafanya,bado wanatuhumiwa waislam kutokana na kilicgofanyika new zealand,ila mpk sasa hakuna connection ya moja kwa moja kuwahusisha,pia kanisa nchini sri lanka lina ugomvi wa kiitikadi na mahindus na mabudha nchini humo,sasa hizo ni allegations tu not comfirmed.
 
Mkuu, tafadhali acha kujidanganya. Ni kundi la waislamu yenye msimamo mkali - National Tawheed Jamaat iliyohusika na shambulio!!
 
Back
Top Bottom