Kuhusu Ruhazwe Jr na Miss chit chat

Kuhusu Ruhazwe Jr na Miss chit chat

Slave

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2010
Posts
5,313
Reaction score
2,657
Habari zenu wapendwa, binafsi nalazimika kuliandika hili hapa jamvini kwa sababu naliona halijakaa sawa na naamini wapo wengi tu wenye mtazamo kama wangu, kwa kuwa hapa ni chit chat naona ni vema tuambiane ukweli kwa macho makavu badala ya kuteta teta pembeni ili kuwekana sawa.

Tukumbuke kuwa tulikuwa na shindano la kumsaka miss chit chat mwishoni mwa mwaka jana, wana chit chat wote tulishiriki kwa namna moja ama nyingine, wapo walioshiriki kama washindani, wapo waliopiga kampeni, wapo waliojitolea kufadhili zawadi, wapo waliopiga kura na pia wapo walioshiriki kwa ku like na comments na hata kwa kuangalia tu.

Naamini wote tulishiriki sio ili tufaidike na zawadi atakazopata miss. la hasha , bali ni katika kuendeleza uhusiano na kuchangamana kupitia jukwaa hili kama ilivyokuwa kwa safari ya Tanga, white party n.k. Ruhazwe Jr alipobuni kuratibu hili shindano wengi tulifurahia na lilikuwa linapata ushabiki mkubwa hapa jukwaani, Lakini kwa kilichofanyika kwenye shindano la mwisho kinakera na hakifai.

Pamoja na kuelezwa kuwa Ruhazwe Jr alipatwa na matatizo lakini naamini bado kuna jambo angeweza kulifanya after sometime ikiwepo japo kutoa feedback ya nini kinachoendelea ili kuepusha watu kukosa imani nae, kitendo cha yeye kupotea mazima afu anakuja Mu-sir na kauli za danganya toto kinaudhi, Najua kuna watu watafyatuka hapa na kauli flani flani ila ieleweke kuwa tunatambua kuwepo na kutokea kwa matatizo, hakuna aliyeagana na Mungu kila mtu anafikwa na matatizo lakini unapokuwa unatazamwa na watu wengi ni vema ukaangalia namna ya kufanya ili kulinda hadhi na Imani ya watu kwako. Now it sounds like you've made a fool of us all. Tunapungukiwa Imani kwa matukio ya namna hii .
pia inaonyesha tarehe na siku ya mwisho ambayo aliingia kwa


Join Date
31st January 2011
Last Activity
28th January 2013 16:35

Wadhamini
- masopakyindi - Tshs 60,000/=
- Ruhazwe JR - Tshs 42,000/=
- Samaritan Tshs 11,000/=
- kitalolo - 10,000/=
- Mu-sir -Tsh 10,000/=
- Chimbuvu -Tsh 5,000/=
- Jiwe Linaloishi- Tsh 3,000/
- Slave - Tshs 2,000/=
JUMLA 143,000/=

View attachment chit chat.bmp

copy: cacico Remmy Madame B Ciello charminglady
@Arabela

wengine ......
Invisible na mod's wengine Baba V King'asti evelyne salt manoh na wengine kibao



CHIT CHAT MUCH LOVE.....
 
Kiasi kikubwa huyu jamaa nimeshindwa kumuelewa hata kwa sekunde, hatukatai matatizo yapo lakini hii inaleta maswali mengi zaidi kuliko majibtu. RUHazwe should come to the surface and say something....!!
 
Last edited by a moderator:
143000/ ni nyingi sana ndugu, kuiacha ipotee juu juu bila sababu za msingi ni uzembe. Kupafahamu kwao itasaidia maana huenda hata mnae mjadili huenda ka is dead zamani ila hamna taarifa rasmi. =
Hahahah...nacheka utadhani mazuri, sasa mkuu hata ukipafahamu sidhani kama itasaidia kitu chochote.
 
Heeee kumbe aliingia January 2013 Lol
Huyu alidhamiria aisee si bure!
Mbona amejiharibia kwa mambo ya kipuuzi?
Wenzake wanakimbia na mabilions yeye hata kilaki hakifiki? Duh
Kweli wanadamu tunatofautiana ujasiri!
Nawachukia watu wa namna hii!
Kwanini upoteze utu wako kwa pesa?
-----------------------------------

I miss you Kipipi
 
Last edited by a moderator:
Heeee kumbe aliingia January 2013 Lol
Huyu alidhamiria aisee si bure!
Mbona amejiharibia kwa mambo ya kipuuzi?
Wenzake wanakimbia na mabilions yeye hata kilaki hakifiki? Duh
Kweli wanadamu tunatofautiana ujasiri!
Nawachukia watu wa namna hii!
Kwanini upoteze utu wako kwa pesa?
-----------------------------------

I miss you Kipipi
kwakweli mkuu hata mie nimeshindwa kumsoma kabisa
 
mimi nilikuwa mganga wa wawashiriki. washiriki wote walikuja kwangu, nikawapa tunguru za upendo wa kutosha
Bujibuji sasa kumbe wewe ndo mbaya wao kwanini hukuwapa na dawa ya kinga sidi ya pesa zao???
 
Last edited by a moderator:
143000/ ni nyingi sana ndugu, kuiacha ipotee juu juu bila sababu za msingi ni uzembe. Kupafahamu kwao itasaidia maana huenda hata mnae mjadili huenda ka is dead zamani ila hamna taarifa rasmi. =

sure noahism
 
Last edited by a moderator:
Erickb52 kuna huyu anajiita Mu-sir ni muongo wa kupindukia kwa taarifa alizokuwa anazileta naona ameumbuliwa na last activity ya jamaa yake ama ID yake nyingine
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom