Kuhusu "mwanga" na "giza" sayansi inasemaje?

Baba Mahendeka umenipa shinikizo la kujibu hoja zako japo ninaliogopa hili suala la mwanga. Nitasema nikijuacho, nisichokijua ntakiacha. Ngoja nikumbuke pia physics yangu ya sekondari. Kuhusu mwanga aliyeanza kusema juu ya unachokiita uzito wa mwanga ni Newton. Yeye alielezea kwamba mwanga unaundwa na chembechembe (light corpuscles). Sayansi inaunga mkono hoja hii kwa kile kinachofahamika kama Photoelectric effect, yaani kuna kiwango fulani cha mwanga kikielekezwa katika metali (metals) husababisha metali hizo kutoa elektroni. Hii inamaana kuwa elektroni zimesukumwa (knocked off) na light corpuscles (maada moja imechukua nafasi ya nyingine kama usemavyo).

Hii habari ya E=mc^2 inazungumzia kuwa ikiwa particle yeyote (hata kama ni nyumba) itakwenda kasi ya mwanga basi nishati itakayotengenezwa itakuwa sawa na uzito wa particle hiyo zidisha na kkasi hiyo ya mwanga, hata hivyo hoja kubwa zaidi ni kuwa particle ikienda kwa kasi hiyo basi particle hiyo hubehave kama energy (nimesema hubehave kama energy na si huwa energy). Nikuchanganye kidogo, kimahesabu tukiandika Tanzania=Tanganyika+Zanzibar matamshi (fikra/hoja/mantiki) sahihi zaidi ni Tanganyika na Zanzibar zimeunda Tanzania na si Tanzania imeundwa na Tanganyika na Zanzibar. Namaanisha cha kwanza ni Tanganyika na Zanzibar ndiyo ikaja Tanzania na si Tanzania iliyoundwa na Tanganyika na Zanzibar. Kimahesabu components ni upande wa kulia wa sawasawa (=), upande wa kushoto wa sawasawa (Ilipokaa Tanzania katika equation yangu au ilipokaa E katika equation ya Einstein) ni majibu ya michakato iliyofanyika upande wa kulia wa sawasawa. Chemistry ni kinyume chake kilicho upande wa kushoto wa mshale (tuseme equal sine ) ni michakato wakati majibu yako upande wa kulia (hesabu majibu ni kushoto mwa equation). Hivyo E=mc^2, hatuzungumzii mwanga halafu tukasema una uzito na unakwenda kwa kasi ya mwanga. Tunasema particle yenye uzito m, inayokwenda kwa kasi ya mwanga c itakuwa ina behave kama energy ambayo kiwango chake ni E. Hata hivyo mahusiano ya energy na particle yenye kasi ya mwanga ni yana ukaribu kiwango cha kuthibitisha tabia ya energy (especially light) kuwa na tabia ya particle na energy interchangeably (wave-particle duality nature of light). Muendelezo ya fikra hizi unakwenda hadi kwenye mawazo ya kusababisha particles fulani (neutrons mfano) ambazo huweza kwenda kwa kasi ya mwanga zigonge nyukliasi (nucleus) ya atom na particles zitakazosababishwa na kugongwa huku zigonge nucleus zingine na zingine na zingine itengenezwe energy kubwa kupindukia E=mc^2....... bomu la nyuklia. Nadhani hatukusudii kwenda mbali hivi.

MWANGA NA GIZA

Ni kazi ya ubongo kutafsiri rangi, mwanga, giza kwa msaada wa macho. Ngoja nikupe dondoo. Mwanga wa jua au mwanga mwingine wowote mweupe (simaanishi mweupe kama maziwa) ni mchanganiko wa rangi kadhaa. Mwanga huo ukitua katika shati ya MwanaCCM itakutana na pigment/chemical ambayo huzuia rangi zingine zisiakisiwe na kuakisi (kureflect) mwanga wa kijani ambao ukifika kwenye macho na kisha ubongo hutafsiriwa kuwa "rangi ya kijani." Njano hivyo hivyo, bluu, nyekundu, pinki etc. Kama rangi zote zitamezwa maana yake ubongo hautapelekewa mionzi ya mwanga. Ubongo kwa sababu ya "uvivu wa kufikiri" unatafsiri hapo ni peusi (na wala si kuwa unapelekewa rangi/mwanga mweusi).

Hivyo giza ni tafsiri tu ya ubongo kama jicho halijapeleka taarifa ya kuwepo mwanga. Jiulize, ukiwasha au kuzima taa, watu wasiokuwa na macho wanatafsiri nini? Wao all the time wanaona giza kwa sababu ubongo umekuwa programmed kuona weusi/au giza pasipokuwa na taarifa ya kuwepo mwanga. Hivyo hata kama mwanaga upo, kama hakuna taarifa, utaona giza tu. Fanya hivi sasa hivi, funga macho yako kwa mikono kwanini unaona giza? Mwanga umeenda wapi? Umezima taa? Hapana, umezuia taarifa ya mwanga, ubongo unakudanganya kuwa ni giza!!! Hivyo mwanga ukiwepo ubongo unasema kuna mwanga. Mwanga usipokuwepo ubongo unakudanganya kuwa giza hilooooo limekuja wakati si kweli kuwa giza linakuja kuchukua nafasi ya mwanga.

Niishie hapa kwanza upime kama umenielewa.
p { margin-bottom: 0.08in; }

nakubaliana na maelezo yako hasa hizo paragraph mbili za mwisho.
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
p { margin-bottom: 0.08in; }

nakubaliana na maelezo yako hasa hizo paragraph mbili za mwisho.

Angalia post namba 40 hapo juu nimejibu maswali/masuala ya Mtazamaji na Amoeba. Huenda kuna mambo utajifunza.
 
Kiza kwa asili hakipo, bali kiza kinatokana na ukosefu wa mwanga. Wataalam wanaweza kujifunza na kuchunguza aina mbalimbali za mwanga au nuru zinazotokana na mwanga, lakini uwezi kujifunza au kuchunguza kiza...
 
Haya ni baadhi ya maswali magumu mengine ni kama....... Mungu alitoka wapi?
Dunia ilitoka wapi?
Kwa nini mtu akitaka kufa anaanza kujua?

Usilete imaginary story, mtu anapotaka kufa huwa inamchukua muda gani toka anapoanza kujua hadi anapo kufa? Itabidi ukasajili dhana yako hiyo kwenye international institution unaweza ukaingia kwenye vitabu vya historia kwa vizazi vingi vijavyo kama mtu mwenye hisia tofauti kabisa na binadamu wengine ama mtu pumbavu kabisa aliye wahi kuishi
 
Kwa elimu yangu ya darasa la saba 'A'
somo la sayansi, Mwalimu Mwaisaka wa Sisimba alinifundisha kuwa mwanga ni nishati inayotuwezesha kuona.
Nikamuuliza giza ni nini, nikachapwa fimbo zaidi ya sita ambazo yeye alikuwa anaziita Sendemaaa


Mkuu ni shule gani hiyo? Mimi nilimuuliza wa kwangu hakunijibu alinipiga kiswahili pale Msimbazi Boys Primary
 
Wakati mwanadamu anaona 'giza' wengine kama paka, bundi wanaona 'mwanga'. Pia wakati mwanadamu anaona 'mwanga' bundi na popo wanaona 'giza'.
 
kwanza lazima ujuwe kuwa Mwanza una source lakini giza halina source! Hivyo mwanga una sababishwa na nguvu ya electrons zinavyo vibrate kutoka kwenye one orbit kwenda nyingine kwenye atom! Kwa kifupi ili kupata mwanga LAZIMA nguvu fulani itumike kuutengeneza. Lakini giza siyo energy ingawa kuna "NGUVU za Giza" ambayo ni mambo ya kishetani!

Mkuu ni kitu gani kinasababisha electrons kuruka kutoka orbital moja kwenda orbital nyingine, pili niwakati gani mwanga unatokea katika harakati hiyo - ni pale electron inaporuka kwenda orbital nyingine au inaporudi kwenye nafasi yake ya hasili? Thanks.
 
Nikwamba unapowasha taa kunakuwa na excited particles nyingi
ambazo zinatoa nishati (mwanya). Wakati unapozima, hizo excited
particles hupungua (giza) kwasababu zinarudi kwenye stationary
state.

Nimefurahia jibu lako, lakini ujajieleza vizuri hizo particle zinazokuwa excited zinakuwa wapi? kwenye source ya mwanga au kwenye chumba cha giza, please elaborate. Thanks.
 
ultimate questions remains unanswered if you deny God do exist!
 
Nakubaliana na Firefox lakini nataka pia kuongeza kwamba dunia hii hakuna kitu kingine kinachotembea haraka zaidi ya mwanga. Speed ya mwanga ni 300,000 km/sekunde au 1079 milioni km/hour. Nadhani hii tabia ya mwanga ndo inafanya ukiwasha tuu taa chumba chote kinajaa mwanga na ukizima mwanga unapotea na giza linajaa. kitukingine napenda kuongeza wajua jua linachukua dakika 8 na sekunde 19 kutufukia linapochomoza, najua lipo umbali wa 150millioni km kutoka duniani

Kuna sub-atomic particles zimeshaonekana ambazo zinaweza kusafiri kwa mwendokasi kuzidi huo wa mwanga! Soma hapa:
CERN observes sub-atomic particles travelling faster than light - The Frontline - a blog from V3.co.uk

au hapa:

Particles found to break speed of light | Reuters
 
Hii inamaanisha:

  1. Bila hewa hakuna sauti (medium zingine eg solids zinaweza kupitisha vibrations)
  2. Bila mfumo wa fahamu hakuna sauti zaidi ya hewa kutikisika kimyakimya.
ZIADA:
Binadamu husikia sauti yake kupitia masikio yake na kupitia vibrations ndani ya kichwa chake. Ukiziba masikio halafu ukaongea bado utajisikia, pia utasikia sauti ya mririko wa damu. Hii inamaanisha kuwa sauti zetu tunazozisikia ni tofauti kidogo na watu wengine wanavyotusikia kwa kuwa wao hawasikii vibrations tuzisikiazo ndani ya mafuvu yetu ya vichwa. Hii inamaanisha pia sauti na mitikisiko yaweza kusikika katika sehemu za ndani ya sikio bila kupitia kwanza kwenye kiwambo cha sikio

ni kweli binadamu tuna range ya kusikia sauti?

namaanisha kuna sauti zaweza kuwa kubwa sana/ndogo sana hatuzisikii lakini viumbe vingine vyasikia
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
ni kweli binadamu tuna range ya kusikia sauti?

namaanisha kuna sauti zaweza kuwa kubwa sana/ndogo sana hatuzisikii lakini viumbe vingine vyasikia

Ndiyo. Kwa mfano wanyama kama popo na tembo huweza kuwasiliana kwa sauti (zenye frequency kubwa (si sauti kubwa)) ambazo binadamu hawezi kusikia. Hii inamaanisha binadamu anaweza kuwa katikati ya popo wawili ambapo mmoja akatoa sauti na mwingine akaisikia halafu binadamu asisikie.

ZIADA
Mbali na range ya kusikia kuna range ya kuona. Mwanga tunaouna sisi uko katika range ya spectrum inayoitwa visible light. Kuna range ya mwanga tusiyoiona eg Infrared na UV light.
 
ZIADA
Mbali na range ya kusikia kuna range ya kuona. Mwanga tunaouna sisi uko katika range ya spectrum inayoitwa visible light. Kuna range ya mwanga tusiyoiona eg Infrared na UV light.
kwenye kuona, kuna mdau mmoja wa sayansi alinambia Tumbili katuacha mbali sana wanadam

hata hizi motion pictures, kwake inakuwa sivyo(anaona zilivyoungwa ungwa) ..!!!!!!!
 
kwenye kuona, kuna mdau mmoja wa sayansi alinambia Tumbili katuacha mbali sana wanadam

hata hizi motion pictures, kwake inakuwa sivyo(anaona zilivyoungwa ungwa) ..!!!!!!!

Very interesting!! Motion pictures (filamu) huonekana kama continuous motion lakini zinaundwa na series ya still pictures ambazo hurushwa kwa haraka na hivyo binadamu hawezi kugundua kuwa ni still pictures. Kwa muda mrefu filamu zimekuwa zikirushwa kwa still pictures 24 kwa kila sekunde moja (24 frames per second), katika motion pictures hii huitwa framerate. Kwa DVD ambazo husambazwa barani Asia na Afrika (PAL system) huwa na framerate ya 25 (Japo siku hizi usamazi umekuwa shaghala-bagala). Kuanzia framerate 16 binadamu huanza kupata taabu kugundua mtiririko wa still pictures na macho yake huanza kumwambia kuwa ni continuous motion.

Hivyo si ajabu wanyama fulani wakawa hawapumbaziki kwa vi-framerate vyetu!! Ukiachana na suala la akili ya kupambanua mambo binadamu anazidiwa na wanyama wengine kama vitu vingi kuanzia uwezo wa kuona mbali, kuvuta harufu, kufeel touch, nguvu ya mwili na mwendo kasi.
 
Very interesting!! Motion pictures (filamu) huonekana kama continuous motion lakini zinaundwa na series ya still pictures ambazo hurushwa kwa haraka na hivyo binadamu hawezi kugundua kuwa ni still pictures. Kwa muda mrefu filamu zimekuwa zikirushwa kwa still pictures 24 kwa kila sekunde moja (24 frames per second), katika motion pictures hii huitwa framerate. Kwa DVD ambazo husambazwa barani Asia na Afrika (PAL system) huwa na framerate ya 25 (Japo siku hizi usamazi umekuwa shaghala-bagala). Kuanzia framerate 16 binadamu huanza kupata taabu kugundua mtiririko wa still pictures na macho yake huanza kumwambia kuwa ni continuous motion.

Hivyo si ajabu wanyama fulani wakawa hawapumbaziki kwa vi-framerate vyetu!! Ukiachana na suala la akili ya kupambanua mambo binadamu anazidiwa na wanyama wengine kama vitu vingi kuanzia uwezo wa kuona mbali, kuvuta harufu, kufeel touch, nguvu ya mwili na mwendo kasi.

Nadhani hapo nilipobold kuondoa mkanganyiko ungeandika DVD player na sio DVD . Maana inaweza kuwachanganya watu
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Nadhani hapo nilipobold kuondoa mkanganyiko ungeandika DVD player na sio DVD . Maana inaweza kuwachanganya watu

  1. Kwani DVD player za PAL system husoma DVD za namna gani?
  2. Hivi katika kutengeneza DVD kuna habari ya kuseti iwe PAL ama hakuna?
 
Back
Top Bottom