acha povu., tumesema Tanganyika wamechukua mamlaka ya Nchi ya Zanzibar juzi kwenye kero za muungano selemani jaffo amesema wametoa kibali cha zanzibar kuruhusiwa kujenga barabara za chake chake mkoani, Wazanzibar wanahoji kwanini vibali vya maendeleo ya Zanzibar vinatoka tanganyika?Umewahi sikia mahali kuna ubalozi wa Scotland, Wales, Northern Ireland, Catalonia, California, Texas, Kerala n.k.? Tangu lini umesikia barabara za Zanzibar zimeingia kwenye bajeti ya Tanganyika? Kama mnataka kuwa na balozi zenu vunjeni Muungano. Badala ya kuzunguka mbuyu mwambieni Rais wa JMT kuwa hamtaki Muungano, sio kujificha kwenye kile mnachoita kero. Pitisheni muswaada kwenye Baraza lenu la kusema kuwa hamtaki Muungano. Chama chake cha ACT Wazalendo kiweke kwenye ilani yake kuwa hakitaki Muungano. Shida kwani iko wapi? Fanyeni hivyo halafu muuone watanganyika wangapi watawabembeleza. Na mnaweza kukuta ndugu zenu wenyewe watawageuka.
Amandla...
Wanaoutaka muungano na kuubembeleza zaidi sio wazanzibari ni Watanganyika maana ndio wanaonufaika nao wamekuwa wakiinyonya zanzibar miaka nenda miaka rudi sasa ccm wa zanzibar hawawezi inua mdomo kusema chochote., Ofisi za TRA zimejazana Zanzibar zinakusanya kodi kutoka kwa wazanzibari zikiwanufaisha watanganyika kulipana mishahara, posho na chakula chao cha kila siku.
Kama nchi 2 huru zimeungana kwanini mamlaka ya kuteuwa mabalozi kuwakilisha tanzania wanatoka bara pekee? Wazanzibar wamekuwa wakiukataa muungano miaka yote lakini ni kwa sababu zanzibar imepokwa soverenity yake toka enzi za mchonga meno., kwanini Karume aliuwawa?? lete majibu