Uswahili, ujuaji uwongo ni mwingi sana kwenye huo mji,
Usiseme round about yao ni kubwa kupita zote Tanzania, watakufukuza, wenzako wanasema ni kubwa Afrika Mashariki na kati, wakati akiongea hayo nzi wamejaa kwenye kiatu hajakifua tangu akinunue, utajiuliza hiyo comparison alifanya akiwa wapi.
Baadhi ya vituo vya daladala vipo 100 metres apart, mfano: kuelekea Bigwa - toka rombo unakwenda mita 100 Lyasembe, mita 50 toka hapo ni Yehova, mita 75 toka hapo ni mwanzo wa makaburi, mita 50 toka hapo ni mti mkubwa, mita 70 toka hapo Ikweta.....mnaojua jazieni vinavyofuata nimesahau
Usipo ugua typhoid na UTI hukuwa mji kasoro bahari labda ulikuwa kwingine
Usafi wa round about hauakisi usafi wa ndani ya mji na vyoo vya public, ushahidi nenda kwenye vyoo vya migahawa, vituo vya mafuta, maofisi ya serikali na taasisi zake, vyuo vya ualimu veta nk utajionea kulivyo hovyoooo wakati viongozi wa hizo taasisi wapo kwenye suti day n night
Vitu fake vilivyoshindikana kuuzika Dar kama vipodozi, madawa ya binadamu na mifugo nk vimejaa kila kona ya mji
Ndoa za watu kudukuliwa ni kama kupokezana sigara kwa wavutaji, nilichoka niliposikia driver wa bus anasimulia kuwa mfanyakazi mwenzake hajapata unyumba miezi sita hivyo hajafika kazini kaenda baraza la usuluhishi, hayo ni baadhi ya niliyoyakuta hukooo kusiko na bahari pamoja na kuwa na kila kitu according to them