Yona F. Maro
R I P
- Nov 2, 2006
- 4,202
- 218
"No nation has the right to make decisions for another nation; no people for another people. "Julius Kambarage Nyerere, from his A
Peaceful New Year speech given in Tanzania on 1 January 1968. Nimesoma kwa masikitiko makubwa sana juhudi za Kundi la Wanaojiita watanzania wa nchini Marekani kufanya maandamano ya Amani kupinga Ziara ya Raisi wa Tanzania Nchini humo.
Nimejaribu kusoma Kundi hilo jina lake ni nini ? Sijapata , Kiongozi wake ni nani ? Sijaona popote badala yake nimeona watu wakijitambulisha kwa majina bandia ambayo sio yao kwa uhakika na matumizi ya Barua pepe wanazotengeneza Kila mara . Kwa kawaida watu wanavyoitisha maandamano kwanza wanakuwa na Agenda zao baada ya kujipanga na kufanya majadiliano kadhaa pia wanakuwa wameomba ruhusa za maandamano hayo ili kuweza kupata ulinzi na miongozo mengine kwa ajili ya maandamano hayo na mwisho wa siku wanakuwa na viongozi wao .
Kutokuwa na viongozi pamoja na agenda na masuala mengine muhimu kwenye maandamano madhara yake yanakuwa kama nchi ya Misri inavyozidi kuangamia sasa hivi kwa kukosa viongozi baada ya maandamano ya kuondoa utawala Fulani madarakani sasa hivi nchini humo kila mtu hamwamini mwenzake na hata maandambano hayajulikani viongozi wake haswa ili waweze kuweka jamii na nchi yao sawa . Utashangaa na kuona aibu ni maandamano gani yasiyokuwa na viongozi tena yanayofanyika katika nchi za watu na watu ambao hawajafika Tanzania kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita na hawajui shida zozote zinazoikabili nchi kwa sasa hivi kwa vitendo zaidi ya kusoma kwenye mitandao bila kuchukuwa hatua yoyote .
Hawa ni watu waliosomeshwa kwa kodi zetu wenyewe wakaamua kuasi na kubaki huko na sasa wanaanza kutumiwa na nchi hizo kama vibaraka kwa kificha nyuso zao , majina yao na hata kujitenga na jamii nyingine za watanzania zilizoko Ulaya na Marekani kwa sababu hata vyama na jamii hizo hazitambui wito wa maandamano hayo wala wale walioyaandaa . Tunawataka watu hao warudi nchini , waje kujenga nchi na sasa hivi kuna fursa nyingi sana kwa sababu ya jumuiya ya afrika mashariki , Comesa , Sadc na nyingine nyingi ambazo nchi yetu imejiunga nazo .
Hizi ni Fursa ambazo waandamanaji hawajawahi kuzihoji wala kuzitumia badala yake ni kupanga maandamano ya kumdhalilisha kiongozi wa nchi pamoja na kuziba fursa nyingine kwa wale wanaotaka kujua zaidi kuhusu Tanzania haswa wageni na wawekezaji . Ni matumaini yangu watu hao wanaojiita watanzania watabadilisha mawazo na muelekeo wao na kuacha kutumia jina la watanzania waishio marekani kwa malengo ya kuharibu jina la nchi na viongozi wake bila kujali itikadi ya vyama vyao , makabila wala dini zao .
Wengine tunaopata fursa za kutoa maoni yetu kwenye mijadala kama mimi hapa , tutumie fursa hizi vizuri na kwa uhuru katika kuelimisha watu bila kuchoka na bila kuogopa vitisho vyovyote toka kwenye makundi ya watu wowote . "...intellectuals have a special contribution to make to the development of our nation, and to Africa. And I am askin understanding that they should possess, should be used for the benefit of the
society of which we are all members."Julius Kambarage Nyerere, from his book Uhuru na Maendeleo (Freedom and Development), 1973.