Maandamano ya Februari 20 Mbeya, kiongozi wetu atakuwepo nchini?

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,114
22,566
Salaam,Shalom!!

Baada ya kumaliza msiba, tuendelee na ujenzi wa Nchi yetu.

Yalifanyika maandamano katika majiji makubwa nchini ,Dar es Salaam na Mwanza,maandamano hayo yameendelea kupata mwitikio mkubwa wa wananchi, hayo yametokea kiongozi wetu ,Mkuu wa Nchi akiwa nje ya Nchi ziarani. Je ni coincidence au planned?

Kunako TAREHE 20 mwezi February 2024, yatafanyika tena maandamano ya Amani jijini Mbeya. HOJA kuu za wananchi zikiwa;

1. Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi, kabla ya Uchaguzi wowote.

2. Kukithiri Kwa Mgao wa Umeme,

3. Kuadimika sukari nchini.

4. Kupanda gharama za Maisha.

5. Madai ya Tume HURU ya UCHAGUZI Kwa kuondoa Miswada iliyo bungeni, Ili irejeshwe UPYA Kwa kubadili vifungu vya Katiba kumwondoa Rais kuteua Tume ya Uchaguzi na wasimamizi wake nknk, HOJA ambazo hazijapatiwa majibu Hadi sasa.

Ningependa kujua ikiwa kiongozi wetu, mkuu wa Nchi atakuwepo nchini siku hiyo au ataendelea na ziara nje ya Nchi.

Maandamano ya Arusha Feb 27, atakuwepo, au atakuwa ziara ingine nje ya Nchi?

Karibuni 🙏
 
Sidhani Kama atakubali Hilo litokee akiwa nyumbani!yule katibu mkuu kiongozi atampangia safari!!

Washauri wangemsaidia kimawazo akabaki Ili atatue KERO za wananchi ambazo ni mwiba Kwa awamu hii!asimuachie makonda pekee coz yeye hakula kiapo cha utii na uaminifu Kwa Dola iliyomweka yeye madarakani!!
 
Changamoto hazikimbiwi,

Angekaa angalau awakemee wasaidizi wake angalau sukari ipatikane.

Tangu uhuru hatujawahi nunua sukari 6,000/= per kg!!!

Na waathirika ni CCM, upinzani na wasio na vyama.
 
Changamoto hazikimbiwi,

Angekaa angalau awakemee wasaidizi wake angalau sukari ipatikane.

Tangu uhuru hatujawahi nunua sukari 6,000/= per kg!!!

Na waathirika ni CCM, upinzani na wasio na vyama.
Unajua hii nchi kuiongoza rahisi sana!

Ukisimami uadilifu kwanza ndani ya chama na una back up ya Dola ,utatatua zaidi ya asilimia 90 ya matatizo yaliyopo!!

Nchi zetu hizi zinahitaji seriousness na uadilifu kutatua changamoto nyingi Sana zilizopo!!

Ripoti ya cag ipo hiyo ndiyo frame work ya kuonekana how serious you are kiutendaji na kuweka direction mpya!

Kamata fungal filisi by the name of the state!nani atakulaumu!!?
 
Duh,

Kuwakamata madon wanaohujumu upatikanaji wa Sukari nchini SI rahisi.

Magu amewahi kukiri kuwa, kuwakamata baadhi ya watu Nchi hii, LAZIMA mtikisiko utokee!!

Tubadili mifumo ya Nchi yetu, Kwa kupata Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi kabla ya Uchaguzi wowote.
 
Safari zake nje ya nchi hazina tija kama maisha ya wananchi yanazidi kuwa magumu, apunguze matumizi ya serikali yasiyo ya lazima
 
Safari zake nje ya nchi hazina tija kama maisha ya wananchi yanazidi kuwa magumu, apunguze matumizi ya serikali yasiyo ya lazima
Muhimu ni kutatua kero zinazowasibu wananchi.

Hayupo hv sasa ajuaye sababu Hasa ya Nchi kuwa gizani mabwawa YOTE yakifurika maji ya mvua za ernino.
 
Duh,

Kuwakamata madon wanaohujumu upatikanaji wa Sukari nchini SI rahisi.

Magu amewahi kukiri kuwa, kuwakamata baadhi ya watu Nchi hii, LAZIMA mtikisiko utokee!!

Tubadili mifumo ya Nchi yetu, Kwa kupata Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi kabla ya Uchaguzi wowote.
Asee kaliunga Ethiopia!!!

Kumbe zile safari ni mahsus kukwepa kujibu HOJA za waandamanaji!!

Tutafika tumechoka sana!!
 
Yaani swali limejibiwa Kwa vitendo.

Inamaana uhaba wa Sukari nchini na ukosefu wa umeme wa HAKIKA kwake ni petty issues?

Wananchi tuongeze ukali kidogo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom