Kuhusu maandamano ya kumpinga rais wa Tanzania Washington DC

Tanzania bado tuna mijitu mijinga ajabu, wao kazi yao ni kujikomba kwa watawala as if waiting to win favours. Waandamanaji wako Marekani, wewe uko upande mwingine ukijikomba komba labda angalau ka U-DC kakushukie, pilipili iko shamba, wewe huku mjini inakuwashia nini?. Nashauri peleka utumbo wako huu kule kule kwako wanakojadili kwa nyimbo za sifa na mapambio kuhusu uozo wa serikali yetu sio humu jf!.
 
Unachokipinga kwenye hayo maandamano ni nini?

Umetaka mshule ukanyimwa?
Umetaka zahanati ukanyimwa?
Umetaka viwanda ukanyimwa?
Umetaka kulima ukanyimwa?
Umetaka kula ukanyimwa?
Umetaka kuongea ukanyimwa?
Umetaka maji ukanyimwa?
Umetaka katiba mpya ukanyimwa?
Umetaka michezo ukanyimwa?
Umetaka demokrasia ukanyimwa?
Umetaka kuabudu ukanyimwa?
Umetaka barabara ukanyimwa?
Umetaka vyuo ukanyimwa?
Umetaka ujasiriamli ukanyimwa?
Umetaka watalii ukanyimwa?
Umetaka wawekezaji ukanyimwa?
Umetaka kufichua ufisadi ukanyimwa?
Nini ulichotaka ukanyimwa?

Au unapinga kwa sababu ya wivu na uoga wa kuona na wengine sasa watakuwa na fursa zote hizo?

mkuu zomba,

hapo kwenye bold, mbona ni mengi tu watanzania wanataka na wananyimwa? inakuwaje we mwenzetu huyaoni? chukulia mfano wa umeme, unapopewa umeme leo na kesho hupewi hujanyimwa tu hapo? au uwekezaji, fursa za uwekezaji alizonazo mwanamfalme wa tz Riz1 kweli ni sawa na nilizonazo mimi? yeye kamaliza shule majuzi tu, hata kazi za uwakili hajawahi kuzigusa na leo tunaambiwa ni bilionaire akimiliki chains za vituo vya mafuta! biashara ngapi za watanzania wengine zimeanzishwa miongo mingi na hazijafikia scale kama hiyo?

hebu angalia, ardhi kubwa kubwa zinapomilikishwa kwa wawekezaji kwa mikataba mirefu, sie watoto wetu hawajanyimwa shamba la kulima kwa siku za usoni? au unajengewa zahanati haina hata wembe wa kukatia kitovu cha mtoto mama anapojifungua, utasema zahanati hujanyimwa hapo? au zahanati kwako ni jengo tu? hapo hujagusa maji, elimu (rejea matokeo ya form 4 ya mwaka jana),

wastaafu wanalilia mafao bora yanayoendana na hali ngumu ya maisha. majuzi generali sarakikya alikuwa akilalamika kuwa licha ya utumishi wake wa muda mrefu jeshini, anapewa sh 50,000/- kama pensheni ya mwezi huku mbunge akipata mara tatu ya hizo kwa siku moja tu! huyo ni CDF mstaafu, je, wengine wana hali gani? kila siku tunasoma wengine wakililia mafao yao hadi wanakufa bila kuyaonja yaliyotokana na jasho la utumishi wao huku hela za michango yao zikichukuliwa kwa nguvu kutekeleza mipango ya kisiasa ya chama tawala, mfano ujenzi wa UDOM na sasa NSSF imepewa kazi ya kuzalisha umeme nchi nzima, (ni hela za wafanyakazi zitachotwa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii hapo), hapo si kunyimwa? nk nk. kwa kweli yako mengi sana, ukifungua macho utayaona!

kwa ujumla, watanzania wanataka maisha bora kwa wote waliyoahidiwa na wamenyimwa! kama hawakunyimwa ni nini, manake mkisema hela hakuna, je, hela ya mkuu wa nchi kutalii na kuizunguka dunia inatoka wapi?, hela ya mashangungi kwa kila kiongozi wa umma inatoka wapi? hela kuwalipa dowans/symbion zinatoka wapi? hela za kutorosha na kuhifadhi nje ya nchi kama zile za hivi karibuni zilizogunduliwa na interpol huko south afrika zilitoka wapi?

kwa kweli watanzania wamenyimwa mengi, na ni wakati sasa wa kusikiliza kilio chao na kukifanyia kazi

ubarikiwe mkuu
ramadhani njema
 
Eeeh! naona haya maandamano ya wadau wa US yameanza kumsumbua JK hadi ameanza kuwatumia akina SHY kujaribu kubadilisha mtizamo wa watu......
 
Hayo maneno kayaseme kule kijijin, tena co vjj vya karbu! U can not fool a literate person, eti maandamano lazma kiongozi, unataka baloz aandamane kumpinga bosi wake?

Kiongoz ni yule aleanzisha wazo la maandamano hayo. Eti hawajui matatzo ya watanzani! VASCO DA GAMA tu ndo hajui matatzo yetu, thats why ziara za nje kila wiki.

Asante kwa kutusimulia tamthilia yakusadikika!! Au unamaslah na kikwete kuwapo ikulu? Maana kama cvyo, nakuonea huruma!
Hvi leo kwako kuna umeme kweli?

Pole Sana ndugu!
 
Kwa yeyote ambaye anapendezwa na serikali iliyoko madarakani sasa.. Huyo haitakii nchi mema. Jk ameshindwa kuongoza nchi hii na ni kwa sababu tu hatujaanza maandamano kama yale ya syria hapa bongo; ila tukiacha nadhani ya syria na tunisia yatakuwa madogo. .

Kwa hiyo njia sahihi ya kuonesha kutopendezwa na serikali ni kuanzisha maandamano ya kuitoa, kwa maoni yako sasa tuachane na taratibu za uchaguzi? Yaani kwa sasa tufanye juhudi kuhimiza watu wetu waandamane ili tumuweke Slaa madarakani kwa lengo la kuwapendeza watu wanaochukizwa na uwepo wa Kikwete madarakani.
 
Unachokipinga kwenye hayo maandamano ni nini?

Umetaka mshule ukanyimwa?
Umetaka zahanati ukanyimwa?
Umetaka viwanda ukanyimwa?
Umetaka kulima ukanyimwa?
Umetaka kula ukanyimwa?
Umetaka kuongea ukanyimwa?
Umetaka maji ukanyimwa?
Umetaka katiba mpya ukanyimwa?
Umetaka michezo ukanyimwa?
Umetaka demokrasia ukanyimwa?
Umetaka kuabudu ukanyimwa?
Umetaka barabara ukanyimwa?
Umetaka vyuo ukanyimwa?
Umetaka ujasiriamli ukanyimwa?
Umetaka watalii ukanyimwa?
Umetaka wawekezaji ukanyimwa?
Umetaka kufichua ufisadi ukanyimwa?
Nini ulichotaka ukanyimwa?

Au unapinga kwa sababu ya wivu na uoga wa kuona na wengine sasa watakuwa na fursa zote hizo?
unaongea nini wewe?
Shule yenye mwalimu mmoja?
Wawekezaji BARRICK, RICHMOND, DOWANS,?
Zahanati zisizo na dawa?
Uwekezaji bila umeme, na kodi ya kufa m2!
Barabara ipi?
Nyumba za nyasi!
Viwanda 'GENERAL TYRE' iliyoliwa na magamba!
Maji mgawo!
Umeme mgawo!
Demokrasia ipi ya kumuua mtu anayeandamana!
Haki ipi mnamchagua meya madiwan wa chama kimoja?
HEBU JIONEE AIBU NA HURUMA PIA!
Unapata maslahi gani na haya yote unayoyakingia kifua? Hebu wapende ndugu zako na waonee huruma wanaojifungua chini kwa kukosa vitanda hspt, na wale wanaofia uzazi eti 'hawana pesa za vfaa'
waonee huruma wanafunzi wanaoacha chuo kwa kukosa 'ADA'!
Muonee huruma mama'ntilie anayenyang'anya mtaji wake na mgambo wa jiji!! Acho akina Rostam wafurahie lakn co wewe!! Au we ndo RIZ ONE? Pole sana!
 
mwizi lazima tumpinge! hajafanya lolote zaidi ya kugawana mali zetu na family yake! nchi haina utawala wa sheria wezi wanatetewa mpaka bungeni eti wanapewa muda kurudisha pesa waliyokwiba hata kutajwa hadharani haiwezekani huyo ndo mtu kapewa dhamana kweli ya kuongoza nchi, mnamwita rais!! maskini TZ bd tuna vibaraka wanatetea huu uozo! eti kwa nini tuandamane kupinga rais wetu! Rais au RAHISI!!
 
Errneus kyambo and the likes, ure the great. Tuungane kumtoa huyu mwehu njiwa na wenzake. Nizaidi ya matapishi.
 
Aliyeanzisha mada sina iman nae,wanaotaka kuandamana wametoa hoja za msingi,tuje hoja ya msingi ni kwann hutaki watanzania wenzako watoe maoni yao kwa njia ya aman?unataka waingie msitun ndo utaelewa wanamaanisha nn,naeshim mawazo yako,ila bila hoja ts crp
 
Hakuna kurudi nyuma........tungepata na bongo huku wa kumfunga paka kengele......kingeeleweka mapema,but the time will tel
 
Maandamano ya kumpinga JK sio lazima viongozi wake wafahamike kwa majina ili yawe na mafanikio au yawe na taswira ya uzalendo. Kama viongozi wanaoyandaa wanaona mazingira hayaruhusu wanaweza kuficha majina yao, nasaba zao na jinsia zao lakini ujumbe ukafika. Tunakumbuka kule Uingereza jinsi wakulima na wafanyakazi walivyoandaa mgomo na maandamano kupinga unyonyaji uliokuwaukifanywa na matajiri waliomiliki njia kuu za uchumi hasa mashamba na viwanda kwa kile kilichojulikana kama Ludism and Chartism. Mtu alijitambulisha kwa jina la bandia kuwa Lord Ludy aliendesha mapambano mpaka kikaeleweka.
Hivyo Watanzania walioko Washigton waungwe mkono na Watanzania wenye mapenzi mema kokote pale waliko huko Amerika ili maandamano haya yafanyike na ujumbe mzito ufike kwa rais mtembezi aka Vasco da Gama. Na tunahitaji mwisho wa siku tufanye thathmini za safari za huyu jamaa kama zina tija kwa mwnanchi masikini anayeishi chini ya dola moja.Tangu ashike madaraka amekuwa ni mtembezi wa safari zisizoisha. Kuna kipindi alikaa nje ya nchi zaidi ya siku 15 na nchi ikiwa gizani na ikawa inatangazwa analala Londoni kesho yake anaamkia nchi za Scandanavia. Je, hapa kulikwa na value for money? Na safari nyingi zimekuwa ni pale anapoacha nchi ina matatizo.Mabomu Gongolamboto yeye akaenda safari nje ya nchi. Ziara nyingine anazoenda tungeweza hata kuwakilishwa na waziri wa mambo ya nje au hata mabalzi walioko kule.

Safari hizi ni hasara big up wenzetu wa US tunawatakia maandamano yenye mafanikio na mtume ujumbe mkali kwa rais asiyependa kufanya ikazi zake-hapambani na rushwa lakini ni zao la rushwa, mdini, mbaguzi wa wenye mawazo tofauti naye na kila aliyempinga kwenye harakati zake chafu za kuwa rais ameula wa chuya


kazi zake,
 
"No nation has the right to make decisions for another nation; no people for another people. "Julius Kambarage Nyerere, from his A
Peaceful New Year speech given in Tanzania on 1 January 1968. Nimesoma kwa masikitiko makubwa sana juhudi za Kundi la Wanaojiita watanzania wa nchini Marekani kufanya maandamano ya Amani kupinga Ziara ya Raisi wa Tanzania Nchini humo.

Nimejaribu kusoma Kundi hilo jina lake ni nini ? Sijapata , Kiongozi wake ni nani ? Sijaona popote badala yake nimeona watu wakijitambulisha kwa majina bandia ambayo sio yao kwa uhakika na matumizi ya Barua pepe wanazotengeneza Kila mara . Kwa kawaida watu wanavyoitisha maandamano kwanza wanakuwa na Agenda zao baada ya kujipanga na kufanya majadiliano kadhaa pia wanakuwa wameomba ruhusa za maandamano hayo ili kuweza kupata ulinzi na miongozo mengine kwa ajili ya maandamano hayo na mwisho wa siku wanakuwa na viongozi wao .

Kutokuwa na viongozi pamoja na agenda na masuala mengine muhimu kwenye maandamano madhara yake yanakuwa kama nchi ya Misri inavyozidi kuangamia sasa hivi kwa kukosa viongozi baada ya maandamano ya kuondoa utawala Fulani madarakani sasa hivi nchini humo kila mtu hamwamini mwenzake na hata maandambano hayajulikani viongozi wake haswa ili waweze kuweka jamii na nchi yao sawa . Utashangaa na kuona aibu ni maandamano gani yasiyokuwa na viongozi tena yanayofanyika katika nchi za watu na watu ambao hawajafika Tanzania kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita na hawajui shida zozote zinazoikabili nchi kwa sasa hivi kwa vitendo zaidi ya kusoma kwenye mitandao bila kuchukuwa hatua yoyote .

Hawa ni watu waliosomeshwa kwa kodi zetu wenyewe wakaamua kuasi na kubaki huko na sasa wanaanza kutumiwa na nchi hizo kama vibaraka kwa kificha nyuso zao , majina yao na hata kujitenga na jamii nyingine za watanzania zilizoko Ulaya na Marekani kwa sababu hata vyama na jamii hizo hazitambui wito wa maandamano hayo wala wale walioyaandaa . Tunawataka watu hao warudi nchini , waje kujenga nchi na sasa hivi kuna fursa nyingi sana kwa sababu ya jumuiya ya afrika mashariki , Comesa , Sadc na nyingine nyingi ambazo nchi yetu imejiunga nazo .

Hizi ni Fursa ambazo waandamanaji hawajawahi kuzihoji wala kuzitumia badala yake ni kupanga maandamano ya kumdhalilisha kiongozi wa nchi pamoja na kuziba fursa nyingine kwa wale wanaotaka kujua zaidi kuhusu Tanzania haswa wageni na wawekezaji . Ni matumaini yangu watu hao wanaojiita watanzania watabadilisha mawazo na muelekeo wao na kuacha kutumia jina la watanzania waishio marekani kwa malengo ya kuharibu jina la nchi na viongozi wake bila kujali itikadi ya vyama vyao , makabila wala dini zao .

Wengine tunaopata fursa za kutoa maoni yetu kwenye mijadala kama mimi hapa , tutumie fursa hizi vizuri na kwa uhuru katika kuelimisha watu bila kuchoka na bila kuogopa vitisho vyovyote toka kwenye makundi ya watu wowote . "...intellectuals have a special contribution to make to the development of our nation, and to Africa. And I am askin understanding that they should possess, should be used for the benefit of the
society of which we are all members."Julius Kambarage Nyerere, from his book Uhuru na Maendeleo (Freedom and Development), 1973.
Unaumwa wewe Mzee kwa mawazo mgando.
Dunia sasa ni kijiji. Usije ukafikiri kizamani kuwa unaweza kufungia mwanao ndani ukimtesa ukidai ni mwanao hata akifa.
Dunia ni kijiji. usije ukajilinda na upumbavu wa utaifa wa ukandamizaji. pole mzee yanayotokea Libya, na kwingineko ni matokeo ya huo mgando.
Kindly update yourself!!!
 
Aliyeleta hii thread ni jamii ya magamba ambao Mungu kawapiga upofu milele. Yaani hata Misri kumtoa mbaka uchumi wao bado unaona hawakufanya kitu. Shame on u, na mjiandae kuwajibishwa maana hamna uwezo wa kuzuia nguvu ya mabadiliko ambayo yanakuja kwa kasi ya ajabu. Nawapa big up sana watz mlioko US, Fanyeni kweli maana huku wanatuua kwa risasi na mabom. Kusema kweli tumechoka sana bado kidogo tu kufikia kikomo the point of no return.
 
Shy, hujielewi .

Hivi nyie vibaraka mnao msifu Jk na blanda zote hizo mnafikira kutumia nini kama sio wowoo. Kama wewe ni waziri au kiongozi mkubwa serikalini huna budi kuandika ushudu kama huo. Lakini kama ni mlalahoi wa kawaida huna Akiri complete. Yaani unaombwe kichani. Hivi matatizo yote haya tunayopata kilaza anachomoka from no where kuja kupotosha hapa.

Yaani umeniharibia siku unadeserve kutupwa kama dawa ya penzi used. Nenda kauzimu na mawazo yako mgando.
 
SHY,
Mkuu wangu ungekuwa na sababu safi sana ya kujieleza au kutetea hoja yako kama unge simamia swala zima la maandamano lakini makosa makubwa umeyafanya ulipoanza kuingia ktk maisha ya watu. Watu hawakukimbia nchi na wala hili neno WAASI sii neno zuri kulitumia isipokuwa kwa viongozi wenye hasira na vijana waishio nje bila hata kutafuta kuelewa sababu zao. wapo watu waliokuja huku nje kwa sababu ya ndoa zao, wapo waliopata uraia au makazi kutokana na elimu au ajira zao. Na ajabu kubwa ni kwamba mnalia sana kupata wawekezaji kutoka nje unafikiri nao pia wameasi nchi zao? maanake kuna Wachina wanavuta mikokoteni hao waliasi Uchina... Mko dunia gani Yarabi nyie wasomi wa Kitanzania tembeeni nje ya nchi mpate kufunua akili zetu..

Kusema kwamba sisi watanzani waishio nje ni waaasi na kutaka warudi nyumbani kwa maelekezo ya jinsi unavyofikiria wewe ni kukosa heshima kwao. Ikiwa wewe mwenyewe unaganga njaa itakuwaje uwe na maelekezo na mipango ya maana sana!. Ndivyo Mlivyo yaani siku zote watanzania wazuri sana kwa ushauri wa biashara na kujenga maisha bora nyumba za watu wakati wao wenyewe hawana maisha kabisa!. Utasikia mtu akishauri jinsi ya kuwekeza, fanya hiki, wekeza hapa - mbona yeye mwenyewe hana mradi hata wa nyanya..Hakuwekeza mahala popote anaganga njaa, kutwa vijiweni?.

Waliopanga maandamano ya Washington DC waache wafanye walichopania kukifanya na kama unapinga maandamano hayo usihusishe kabisa maamuzi yao na maisha yao kwa sababu HAIHUSU!..wewe kama Unafaidika na EAC, Comesa, SADC na jumuiya za Kiafrika endelea kufaidika nazo lakini haipotezi ukweli kwamba JK nchi imemshinda kuongoza!....
Ujumbe huu tunakuomba umfikishie.
 
Mkuu katika dunia ya sasa ukweli na uwazi ni jambo la lazima. Viongozi hawapaswi kuogopa ikiwa wako wazi ni ni wakweli. waache watu waandamane kueleza hisia zao ikiwa ni uzushi tutajua tu maana tuna akili. Viongozi wa sasa wajue hakuna siri tena wawe makini. ukifanya mambo kibabe utaumbuka
 
Maandamano ni ishara muhimu ya kujitathimini na kujisahihihsha Viongozi wasiogope
 
Mimi nina swali wakuu. Je kuandamana Marekani kuhusu matatizo ya Tanzania kutasaidia kitu? Nauliza hivi kwa sababu nia na madhumuni ya maandamano ni kushinikiza. Sasa kama maandamano hayo hayata pewa air time ya kutosha kwenye vyombo vya habari vya Marekani na Tanzania tutakuwa tumepata faidia gani?Nauliza haya kwa sababu si mara ya kwanza kusikia Watanzania waliopo Marekani wanataka kuandamana. Mwaka wa jana baada ya uchaguzi walisema wataandamana. Sasa sijui kama waliandamana na kama waliandamana basi hayo maandamano haya kutimiza lengo kwa sababu hamna mwananchi wa kawaida Tanzania aliye yasikia wala kuyaona.We have limited resources. Let us direct them towards plan that actually work. Kama maandamano yanayo fanyika Tanzania na Chadema naona faida zake kwani zina shinikiza serikali kujiangalia. Sasa haya ya Marekani sioni any positive effect from them.
Mimi naamini kwamba maandamano hayo ya ughaibuni yatatusaidia sana tu. cha msingi hapa ni kwamba tunahitaji kupata namba inayoongezeka ya watu ambao wapo tayari kujitokeza kuandamana kupinga vitendo vya serikali inayoongozwa na JK. JK hajazoea kupingwa. ile walk out ya CHADEMA ilimkera sana, na kadhalika any form of dissent kwake inamkera. pengine itasaidia kumfanya atafakari zaidi. lakini hata kama ni sikio la kufa, tunahitaji kumobilise watanzania nje na ndani tuwe kitu kimoja katika kupinga utawala wa JK. dunia sasa ni kijiji kwa hiyo kufanya action nje ya nchi haipaswi kuwa kitu cha ajabu. hata kama formal media hawataipa air time, tunaweza kutumia social media kuisambaza, kumbuka kwamba walengwa sio hasa watu wa nje, bali tunahitaji kumobilise watanzania. kitendo cha JK kupingwa na watanzania walioko huko katika diaspora, kita -galvanise wale waliopo ndani
 
Hakuna kurudi nyuma lazima tuandamane..Watanzania wenzetu wakiandamana wanapigwa na risasi zamoto wakidai haki yao..sasa tuone na nani atakayetupiga na risasi za moto..
Nidhamu ya woga ilikwisha habari yake..

Waambie hao vibaraka wa utawala ulioshindwa kukidhi matakwa ya Watanzania, labda siku moja watafunguka na kuacha ukibaraka wao.
 
Inatia aibu kuona mtu mwenye ufahamu akishabikia utawala ambao umeshindwa kuperform hata vile viashiria vidogo vya utawala thabiti.mf kukemea,kuonya,kuelekeza na kutoa maelekezo ya nchi ina kwenda wapi kwa nguvu gani. Ni aibu kwa taifa kuliendesha kwa kufuata nguvu za matukio,kila mwenye mamlaka katika nchi ana lake, katibu kiongozi, rais,wewe salva,pm, jairo kila mtu anatenda kutokana na matukio! bila tukio hakuna kazi.kazi ni kupanga mikakati ya kuficha ukweli na hadaa ili kufanikisha ulaji.

Jana tumeambiwa mafuta yamepungua,leo yamepanda! tunajiuliza hivi mpo makini na kazi kweli hata msijue maamuzi yunu ya leo yatasimama kweli kwa muda gani? aibu,aibu,aibu.mlitudanganya ili bajeti yenu ipite ili muweze kufanya safari ya marekani kwa garama itakayo tokana na mauzo ya mafuta.siri ya mafaniko ya malengo ya kisiasa lazima mambo yenu yasiwe wazi.hawa ndugu zetu wa marekani hawatajiweka wazi kwa maslahi ya mipango yao. je wewe ambaye unalalamika kuhusu kupinga maandamano haya,mbona haujaweka wazi jina lako? tunakujua kwa mtiririko wa hoja zako.ukiokota maandishi ya mwl nyerere hata kama haja andika jina utafahamu ni mwl kwa kuwa mtiriko wa hoja utakutambulisha huyu ni julius.

nchi ikikombolewa mtatafuta pa kwenda na hamta papata.msiniulize ni lini na itachukua muda gani! lakini muda c mrefu na muda c mfupi. amandla! amandla!
 
Back
Top Bottom