Kuhusu maandamano ya kumpinga rais wa Tanzania Washington DC

Nimefurahi kuona kwamba member wengi wa jf ni waelewa, ila wapo baadhi ambao wanajisahau kwamba jf si mahala pa kutukanana bali kujengana kwa hoja,tujadili vitu ambavyo hata ukikuta kundi la watu linajadili basi uwe na uelewa wa kutosha.

Binafsi,kuandamana hakukatazwi ila hoja ya msingi ya kuandamana ni nini?Hawa watu walishajiita watanzania waishio marekani pengine wengi wao hawana mpango wa kurudi kuishi Tanzania. Hawana uchungu wowote na Tanzania yetu,sidhani kama walishajaribu kuleta mchango wao kwa serikali yetu.Ikumbukwe kwamba watanzania Hawahawa ndo walimkaribisha kikwete kwa shangwe,ndelemo na vifijo alipotembelea marekani kwa mara ya kwanza pindi alipochanguliwa kuwa rais wa Tanzania.

Tusiwaige hawa, bali sisi kama taifa tunatakiwa kuwa na msimamo wetu thabiti na kuendelea kujitafutia riziki za siku hadi siku.
 
Kwanza niwapongeze hao walioanzisha hii move ni watu waelewa, hawa ambao wanajidai wanapinga hayo maandamano ni wanafiki. Tatizo la nchi kwa sasa ni UNAFIKI na ndiyo chanzo cha matatizo ya hii nchi, utakuta mtu anafikiri akimsifia kikwete atafanikiwa na matokeo yake mnaona hata uteuzi wa viongozi unabase kwa watu ambao ni WANAFIKI.

Kikwete anajulikana udhahifu wake ni rais asiye na uwezo na ni jambo kusikitisha hata wale wanaojua bado wanamshabikia kisa kuna namna wananufaika na utawala MBOVU wa huyu jamaa. Lazima kifanyike kitu vinginevyo nchi itaangamia.
 
Shy,

Badilika ndugu yangu hizi story za kunukuu mambo ya mwalimu ndizo mnazitumia kuua nchi hii ili kuararisha uovu, kitu cha kujua ni kuwa hivi
sasa watanzania hadi vijijini wanajua shida zao. Leo hii niliko ni siku ya nne hakuna umeme numeenda tanesco wanasema ni mgao sasa unawambia nini watanzania miaka hamsini ya uhuru you are so absolute. Hivi leo nani asiyejua uovu wa serikali ya awamu ya nne ni wizi,ufisadi.

Ndugu yangu badilika labda kama wewe ni waziri au mkurugenzi ndiyo wanashabikia unufaikaji usio halali lakini mtanzania wa kawaida amerudi kwenye ujima. Bora mkoloni arudi kuliko serikali ya KIKWETE ni utumbo wa kupindukia muwe mnamwambia nyinyi vibaraka wake kwamba uwezo wake ni DUNI na ni balaa kwa watanzania kuwa na kiongozi kama yeye. Badilika umepitwa na wakati.
 
mkuu, mi nadhani kama kweli azma yao itatimia, bas watakuwa wamefuata taratibu zote zinazotakiwa na mamlaka za huko wanakoishi, kwa hiyo kama mamalaka za huko zitawataka wataje viongozi wao na matakwa mengine naamini watafanya hivyo na kinyume chake hawataruhusiwa.

kuhusu kumdhalilisha mheshimiwa rais, mi sioni kama ni ishu hapo kwani kuandamana ni kutoa mawazo tu ili wasikike maoni yao, ni mbinu ambayo watu wanyonge hutumia kuwashauri wakubwa hasa wale wasiofikika kirahisi. mfano hatuwezi kusikia mawaziri wakiandamana na mabango barabarani kwa sababu wao wana utaratibu wa kumshauri rais mara kwa mara kadiri inavyohitajika, lakini mfano mimi kama sijaridhishwa na mambo yanavyoenda, huyo raisi nitamshauri saa ngapi? na hii nchi ya kidemokrasia?

kuhusu utanzania wa wanaotarajiwa kushiriki, sina hakika kama una utata au la, ila kama ni watanzania, nafikiri tusiwaelewe vibaya. naamini kwa kuishi kwao nje ya nchi wameona tofauti ya maendeleo na namna yanavyopatikana hivyo kama raia wenye wajibu hawawezi kukosa namna ya kushauri na/au kushinikiza mabadiliko wanayodhani yanapaswa kufanyika, na ndivyo wanavyofanya hivyo sioni ubaya.

pia ni vizuri nyinyi mlio karibu na mheshimiwa rais mkamshauri kuwa sasa ni wakati muafaka ajifanyie tathmini mwenyewe juu ya safari zake za mara kwa mara na gharama za safari hizo huku nchi yake ikiwa hoi kuichumi na shida za wanachi zinaongezeka kila kukicha, na namna umma unavyoutazama uwajibikaji wake hasa wakati kama huu wa vizungumkuti kibao ndani ya nchi kama umeme, mafuta, sukari, rushwa nk badala ya kuwatazama kwa jicho baya kila wanaotaka kumuona akiwajibika zaidi. sisemi kuwa hawajibiki, bali nasema wengi wanataka kumuona akiwajibika ZAIDI.

mwisho nashauri tujitahidi kuona nguvu hizi za mabadiliko na kuzipa mtazamo chanya kwani haziwezi kuendelea kusitirika kama ilivyokuwa zamani. mabadiliko hayana budi kuja, jinsi maandamano yanavyoshika kasi nchini ndivyo na watz walio nje ya nchi wanavyozidi kuamka na kujiunga katika maandamano ili waweze kushiriki kwa vitendo michakato ya maendeleo ya taifa lao hata wawapo huko nje

natunaini nimeeleweka vyema,
ni mtazamo wangu tu na naweza kusahihishwa

asante


Umeeleweka vyema Miss Judith.
 
Rejea article ya wiki iliyopita katika Raia Mwema
"Tutafuturu na kuandamana pamoja"
By Msomaji Raia
 
Mimi nina swali wakuu. Je kuandamana Marekani kuhusu matatizo ya Tanzania kutasaidia kitu? Nauliza hivi kwa sababu nia na madhumuni ya maandamano ni kushinikiza. Sasa kama maandamano hayo hayata pewa air time ya kutosha kwenye vyombo vya habari vya Marekani na Tanzania tutakuwa tumepata faidia gani?

Nauliza haya kwa sababu si mara ya kwanza kusikia Watanzania waliopo Marekani wanataka kuandamana. Mwaka wa jana baada ya uchaguzi walisema wataandamana. Sasa sijui kama waliandamana na kama waliandamana basi hayo maandamano haya kutimiza lengo kwa sababu hamna mwananchi wa kawaida Tanzania aliye yasikia wala kuyaona.

We have limited resources. Let us direct them towards plan that actually work. Kama maandamano yanayo fanyika Tanzania na Chadema naona faida zake kwani zina shinikiza serikali kujiangalia. Sasa haya ya Marekani sioni any positive effect from them.

Kwanza, maandamano ni haki inayotambuliwa na kupewa hadhi ya juu sana Marekani kama mnara wa haki ya kila mwananchi kujieleza bila ya kuwa na woge wowote. Pili, maandamano haya kama yatafanyika, na kwa sababu Rais anakuja Marekani, kwa hiyo ni sahihi. Hili eti la maandamano kufanyika nje ya nchi na eti kutokuwa na faida Tanzania ni dhana butu kwa sababu haki ya kujieleza inapita mipaka ya kijiografia na watanzania hawa watakaoandamana wanayohaki hii hata kama hawako kwenye ardhi ya Tanzania. Hali ya nchi inaendelea kudorora, gharama za maisha zinazidi kupanda kwa mwananchi wa kawaida, lakini hawa viongozi waliochaguliwa na wananchi karibu asilimia 80 ambao bado wanaishi kwenye nyumba za tembe, hawana maji safi, wanaendelea kuwa "victims" huku viongozi hawa wanaendelea kufuja pesa za hawa hawa walipa kodi watanzania wanyonge.
 
Kwa hiyo mtanzania yeyote anayeishi nje asipomuunga mkono kikwete ni mhaini, siyo mtanzania, hajui lolote kuhusu Tanzania, na hatarudi Tanzania!!! Ikiwa maandamano hayo hayana faida kwa nini mmechachawa kiasi hicho kuyapinga?! Yanawagharimu nini nyie?! Na kwa taarifa yenu baadhi ya wabongo waishio Canada wanaangalia uwezekano wa kushiriki... Walio nchini Mexico japo ni wachache wataenda US. Kama mnafikiri kikwete siyo binadamu na hafai kuaibika kama kaboronga, kafanyeni homework yenu upya.
 
Kwani wewe unamuonea huruma au unahofia ulaji, unaona anachotutenda ni kizuri au na wewe ni fisadi miongoni mwao yani mpaka watu wa mbali wameamka we bado uko usingizini!
 
Mimi nina swali wakuu. Je kuandamana Marekani kuhusu matatizo ya Tanzania kutasaidia kitu? Nauliza hivi kwa sababu nia na madhumuni ya maandamano ni kushinikiza. Sasa kama maandamano hayo hayata pewa air time ya kutosha kwenye vyombo vya habari vya Marekani na Tanzania tutakuwa tumepata faidia gani?

Nauliza haya kwa sababu si mara ya kwanza kusikia Watanzania waliopo Marekani wanataka kuandamana. Mwaka wa jana baada ya uchaguzi walisema wataandamana. Sasa sijui kama waliandamana na kama waliandamana basi hayo maandamano haya kutimiza lengo kwa sababu hamna mwananchi wa kawaida Tanzania aliye yasikia wala kuyaona.

We have limited resources. Let us direct them towards plan that actually work. Kama maandamano yanayo fanyika Tanzania na Chadema naona faida zake kwani zina shinikiza serikali kujiangalia. Sasa haya ya Marekani sioni any positive effect from them.

The era of kidding are gone. Hakuna mtu kizazi hiki utamfundisha njia ya kutumia anapotaka kufikisha ujumbe kwa mtu mwenye ulemavu wa ku pay attention kwa matatizo ya anaowaongoza. Lengo la haya maandamano ni kumlazimisha rais kuelewa nchi ipo pabaya kwani inawezekana haya yanapofanyika TZ anaona watu ni wapuuzi. Hakuna mtu anafanya maandamano ili yatangazwe au yaonekane kwenye vyombo vya nje kwani kama lengo ni hilo yangeweza kufanyika tu hata bila kusubiri JK afike USA. Maandamano haya yana lengo la kumwamsha JK kwenye usingizi mzito aliolala wakati waTZ wakipitia kipindi kigumu sana huku yeye akiwa kimya bila kuwa na ujasiri wa kuchukua hatua yoyote.
 
Ujumbe ni kwa jk sio kwa vyombo vya habari naona jamaa kasahau hapo, natamani siku hiyo ifike nione kama jamaa atakuwa anachekacheka kama kawaida yake.
 
nimejihisi kutapika kwa ujinga ulio uandika hapa,

1. Wale ni watanzania ambao ni ndugu zetu na wanaumia kuona sisi ndugu zao tunaumia na kupata shida bila sababu ya msingi.

2. Hata wao wanaatthirika kiuchumi wao binafsi kwani lazima watumie sehem ya kipato chao kwa kuwatumia ndugu zao ambao wapo Tanzania kwaajili ya kugaramia elimu na matibabu,huduma ambayo wangepaswa kupewa bure na serikali.

3. Wanakila sababu ya kufanya hivyo kwani kwetu hapa Tanzania tumekosa fursa huru ya maandamano na kama kwa maandamano ya kumpinga meya tu wa arusha mjini(sio mbunge sio waziri) watu 3 waliuawa na makumi kujeruhiwa, je tukiandamana kumpinga rais watuua wangapi? (si maanishi hakuna cku halitatokea hili, ila waambie hao walio kutuma kuwa wanatengeneza taifa la watu wasio na cha kupoteza!)

We mwakilishi wa walanchi umepotosha kila jambo ulilojaribu kulijengea hoja, Hiv unadhan watanzania wote tuna weza kuwa wajinga kiasi hicho, Hiv unadhan hatujui sheria ya maandamano marekani inasemaje! Mbona unakurupuka kumpa mkeo vidonge vya majira wakati ni mjamzito? Bob alisema ''the time will tell'' . . . . . .

WanaJF tuachane na huyu mwenye fikra finyu na mawazo mgando na tuwaunge mkono hawa wakombozi wetu, hata kama hawaishi tanzania kwa sasa! Mbona aliyefanya mapinduzi ya Zanzibar hakuwa MZanzibari? Mbona che guevara hakuwa mcuba lakini alishiriki kufanya mapinduzi cuba na nchi nyingine nyingi duniani? Mi niwaombe mnao weza kwenda Marekani kuwaunga mkono wakombozi wetu hawa mfanye hivyo!

Pamoja mkuu. Tanzania ni yetu sote si ya mafisadi wachache.
 
Back
Top Bottom