Kuhusu kukaribisha wageni chakula

Kuhusu kukaribisha wageni chakula

Eating together is intimate. It's very sensual. When you invite someone to sit at your table, you're inviting a person into your life.
 
Ndugu,
Siwezi sema ulichofanya ni kosa ama Si kosa kutokana na jinsi unavyoelewa kuhusu kosa.
Ila kwa lugha nyepesi ulichofanya sio ustaarabu.
Swala la mgeni kuja bila kutoa taarifa ama kutoa taarifa ni utaratibu wako wa maisha, ni utaratibu mzuri lakini hiyo haimaanishi kuwa ni utaratibu bora.
Mngeweza kuongeza kipimo cha chakula mara baada ya kupata wageni.
Ungeweza kukaa kimya mbele ya wageni na kisha kuongea na rafiki yako juu ya aina ya makubaliano mliyonayo.
Dunia hii ndogo sana, leo umewanyima jamaa ugali dagaa kesho utakutana nao mahali na utahitaji msaada wao.
Ni vyema kuwa na taratibu lakini sizivuke mipaka ya ustaarabu.

Wakati mwingine kuwa mstahilivu kidogo.
 
Huo ni uchoyo uliovuka kiwango,
Duuuh hata aibu huoni eti 'kuna kosa lolote nililolifanya?'

Shame.
Dada sioni hapo kama kuna uchoyo hivi simu zote zilivyoojaa hawajaweza hata kumpigia mwenyeji wao kama wanakwenda kumuona. Sasa kama wangelikula si jamaa angelala na njaa na kubakia kuwasema. Bora alivyo waabia kuliko kuwasema
 
Hellow,
Mimi nakaa nyumba moja na rafiki yangu ambae ni teacher wa sekondari, na kwenye bajeti yetu ya mwezi kila cku tumeweka portion ya watu 2, kwenye swala la msosi.

Juzi Juzi ticha alitembelewa na rafiki zake wawili wa kiume muda wa mchana, walimkuta teacher akiwa anapika, chakula kilipoiva, teacher alipomaliza kukaribisha rafiki zake msosi nilimuuliza kama wageni waliokuja walitoa taarifa kabla ya kuja, teacher akasema hamna c wamekuja kunsalimia tu, na blah blah nyingine, mm nikawauliza wageni wale kama walitoa taarifa kabla ya kuja nao walisema oh unajua, oh.., mm nkamwambia teacher live mbele ya wageni kuwa share ya msosi iliyopo ni ya watu 2, na nliwaambia wageni kuwa kwa vile mmekuja bila taarifa cha kuwasaidia ni kuwapa maji, msosi uliopo hapa ni wa watu 2, so sitakubali tu-share na nyie huu msosi, bac wale wageni walikaa pale mwishowe wakaondoka, hlf baadae teacher alintupia lawama kuwa I was rude, hiv jamani kuna kosa lolote nlilolifanya?

Naombeni mawazo yenu
yes it was rude. kwani mngegawana four ways hata kama ni kidogo, mngepungukiwa nini? wakati chakula chote unaenda kukiacha chooni!
 
Hahaha.... We umetisha. Maana syo kwa uchoyo huo. Kwani chakula ni nini?! Ungewaacha wale tu
 
Dada sioni hapo kama kuna uchoyo hivi simu zote zilivyoojaa hawajaweza hata kumpigia mwenyeji wao kama wanakwenda kumuona. Sasa kama wangelikula si jamaa angelala na njaa na kubakia kuwasema. Bora alivyo waabia kuliko kuwasema
Wewe nae ni mchoyo tena mlafi tena una roho yenye kutu.
Unasapoti huo ujinga kweli? Rizki unatoa wewe?
Tena kwa taarifa yako ukitembelewa na wageni hlf chakula kikawa kidogo mkila kwa pmj utashangaa nyote mnashiba na hata kusaza,

Ndio nyie mkisikia hodi mnaficha chakula uvunguni, looh! hapo tu chakula hata hao wazazi wenu mnawatunza kweli? Au ndio nyie mnaosema ooh tumezaliwa wengi sio mimi tu mpk nimtunze.

Acheni hizo bhana tena mwanaume kua mchoyo wa chakula ni kichefu chefu kisichokua na tiba.
 
Mkuu hii hta km ni hadithi lkn ukiiweka kwny ukweli aisee inaumiza sana hah!!!kunyima chakula??huo ni uchoyo ucio na mfano dunian!!!afu anawacmanga wgeni mzma kwli hyu!!??
Huyu sio mzima kbs tena kuna mchoyo mwenzie anamsapoti,
Duuh sikujua kama kuna binaadamu wanajali kula kiasi hiki,
Hawa watu hata maskini akiomba chakula watamgawia kweli?
Au ndio watampiga teke apotelee mbali.
 
Daaaaah kwani ungewakaribisha kwa mfano ingekuwaje labda?? Au kilikuwa chakula adimu nini???
 
nimekariri id yako mchoyo mkubwa wewe!! mkuu chakula mlo mmoja tu?? kwani mkuu wewe haujawahi kuhudumiwa vema ugenini licha ya kwenda bila taarifa?? bas****d
 
Wewe nae ni mchoyo tena mlafi tena una roho yenye kutu.
Unasapoti huo ujinga kweli? Rizki unatoa wewe?
Tena kwa taarifa yako ukitembelewa na wageni hlf chakula kikawa kidogo mkila kwa pmj utashangaa nyote mnashiba na hata kusaza,

Ndio nyie mkisikia hodi mnaficha chakula uvunguni, looh! hapo tu chakula hata hao wazazi wenu mnawatunza kweli? Au ndio nyie mnaosema ooh tumezaliwa wengi sio mimi tu mpk nimtunze.

Acheni hizo bhana tena mwanaume kua mchoyo wa chakula ni kichefu chefu kisichokua na tiba.
Mimi acha kuwa na roho yenye kutu nataka niwe na mavi haswa lakini kama hujanipa taarifa unakuja hulii kitu. Nishafanya hivyo mara kadhaa na wala sijali.
Kuhusu kula kwa pamoja hayo maneno ya wazee wa zamani hakuna ukweli wowote hapo ndio maana mpaka leo akili zetu migando kwa misemo yao ya kale.
Kuhusu mzee wangu namtunza kama mboni ya macho nime mjengea nyumba na kila mwenzi nampa hela ya matumizi 500k.
Narejea tena bila ya taarifa sikukaribishi kula sio kama mchoyo bali mawasiliano yapo kwanini ujilete kama jini au malaika mtoa roho bila ya taarifa.
 
Mm ni mwanaume, na sio mchoyo kama unavyofikiria ila sometimes inabid tuwekane sawa Tamama Diva Beyonce
Wewe si tu mchoyo na Kauzu kama dagaa; pia uwezo wako wa kufikiri ni finyu sana!
Hukuwekwa hapa duniani upambanie kula. Uliwekwa hapa kama utukufu wa Mungu na uyashuhudie maajabu yake. One of the wonders ni upendo utokao kwa Mungu na kusambaa kati yetu wanadamu. Huu upendo ni sacrificial , yani kujitoa kwa ajili ya wengine. Bajeti inabana lakini wewe unaamua kujitoa mhanga na kuwahudumia wageni. When its time for your death and God gives you the favor to recall your life. Its moments like those that you will remember! Hutakumbuka jinsi ulivyobana budget ukajilimbikizia vitu ambavyo mwisho wa siku utaviacha....
 
Ulikosea kabisaa...chakula tu??? Ungewapa tu halafu baadae uwaambie next time mtoe taarifa.
Acha uchoyo bana..
 
Back
Top Bottom