Kuhusu kukaribisha wageni chakula

Kuhusu kukaribisha wageni chakula

Katika safari yangu ya kufuta ujinga, nilikwenda nchi fulani kujifunza afya ya jamii. Tatizo kubwa katika jamii ile ilikuwa watu kuwa na uzito uliozidi. Katika kupigana na lile tatizo wakaangalia tabia za milo katika familia na mashuleni. Walikuja kugundua kuwa tofauti ya familia za kizungu na kiafrika ni kuwa mfano familia ya kizungu dinner: Familia ya watu wanne, packet ya mapaja manne ya kuku yamenunuliwa, yataokwa na viazi, sahani nne, kila sahani itapata kipande cha kuku, viazi na mboga, wamemaliza. Ukimaliza unaweza sindikizia na kibakuli cha ice cream au yoghurt.
Familia ya waafrika: familia ya watu wanne, wali utapikwa, mchuzi, mboga, mtoto ambae hajashiba anaenda kuongeza jikoni, chakula kikibaki mama anafurahi kuwa watoto wamekula mpaka wamesaza.

Hii ndiyo sababu kwa wazungu si rahisi kukaribishwa chakula kama hawana taarifa kuwa utakula nao. Haya mambo ya utandawazi yamenza kufanya baadhi ya waafrika kuacha mila zetu na kuthamini chakula. Heshima ya mwafrika ni mgeni wako ale chakula kwako, hata kama hakitoshi, mwenyeji atatoa portion yake kwa mgeni, ikibidi utakunywa chai na mkate au utapika uji mgeni akiondoka.
 
Duh! Mwanawane wewe bandidu, ukiendelee hivi utakuwa millionaire soon
 
Kuna kabila moja kanda ya Ziwa hii ni culture yao.

Kama hujatoa taarifa msosi sahau, hata ukiukuta mezani kaa pale utulie.

Mazingira yanatushepu, ila kuwaeleza moja kwa moja inabidi uwe mtata kweli.

BTW, kama mnafanya kazi wanaume kukaa nyumba moja siyo.
Hilo kabila ukigusa msosi wao ni utachezea kipigo hafu kama ulikula samaki wao wanakulamba mkono na kuupaka mchanga ili usiambulie kitu... Yaani ni nyoko

Ila pia kuna kabila ukanda huo huo wao ukifika ukakuta wanakula usisalimie maana hutoitikiwa bali wao ni unajumuika hata kama hamjuani unapiga msosi hafu chakula kikiisha ndio salamu na kuulizana wewe nani znafata.

Culture za Kitanzania zinatofautiana na zinashangaza, muhimu ni kuwa flexible na kutochukulia vitu too seriously
 
Back
Top Bottom