Kuhusu katiba mpya; msimamo wa CCM ni upi?

Comrade ukiambiwa uandike msimamo wa chama chetu kuhusu katiba mpya kwa sasa utaandika nini?
Ilani inajieleza na hakuna sehemu Ilani imebadilishwa.Hakuna kikao cha chama kilichoifuta sehemu hii ya ilani(I wish wafanye hivyo tuendelee kutengeneza wataalamu wa AI na wanasayansi wa kwenda Angani badala ya kutumia fedha za posho)

Swali muhimu...Je mazingira ya kuleta katiba mpya yapo?Je unaleta katiba mpya huku kuna watu hawataki kukaa mezani?
 
Mnaweza ku-opt njia hiyo ambayo mmeanza kuijaribu yaani kutaka damu imwagike lakini ni njia isiyowezekana kwa Tanzania..Hata wakati wa kudai uhuru TANU na ASP walikuwa na options hizo lakini kamwe zisingeweza kuleta uhuru wa kweli na kuliacha Taifa salama.
Nguvu hujibiwa kwa nguvu kinzani ...hoja hujibiwa kwa hoja.
Nasema hivi, hamna umma wa kutambia tena, katiba itaandikwa hata kwa kumwaga damu. Mliokuwa mnawatumia kuwabeba, hata wao wanajua hamna support ya umma tena. Ni suala la muda tu, lakini katiba itaandikwa kwa heri ama kwa shwari.
 
Ilani inajieleza na hakuna sehemu Ilani imebadilishwa.
Swali muhimu...Je mazingira ya kuleta katiba mpya yapo?Je unaleta katiba mpya huku kuna watu hawataki kukaa mezani?
Wakae mezani na matapeli? Ni mara ngapi na miaka mingapi mmetakiwa ipatikane katiba mpya mkagoma? Narudia tena, ile voters turn out imeonyesha mko nje ya muda. Katiba itaandikwa tena ile tunayoitaka watanzania, sio hiyo ya hao majizi wa ccm.
 
Je msimamo wa Ilani ya CCM 2025 uliheshimiwa na wadau wengine kama wanaharakati na vyama vya siasa??
hudhani kuwa response ya wadau na wanaharakati ilikuwa ni matusi,kejeli na kujaribu kuipindua Serikali halali?
Kwa muktadha huu na ishara hizi unategemea CCM iendelee kuchimba kaburi lake yenyewe?
Siku wanaharakati na wapinzani watakapoacha kuitumia hitaji la katiba kama silaha yao ya kuchukua nchi ndio siku muafaka ya kuwa na katiba ya wananchi utafikiwa.
Kamwe isitokee na ni laana kuandaa katiba yenye lengo la kuifuta CCM na mrengo wa Ujamaa.
JE TUNATAKA KATIBA YA KUREJESHA MATAKWA YA WAKOLONI???
Katiba mpya na bora itatokana na CCM na itatoka ndani ya CCM...
Kama kweli unaitaka katiba mpya jenga hoja ukiwa ndani ya CCM na uoneshe namna ambavyo CCM inaweza kuishi madarakani au kuweza kuachia na kurudi madarakani....hii ndio itakuwa akili na sio kwa mwenendo wa sasa wa hooligans na vibaraka wa walami wanaolazimisha katiba mpya bila hata kutaja vipengele vinavyomgusa mwananchi asiye mwanasiasa.
Wewe ni mpu.mbav.u mwandamizi,Yaani principal foolish.Katiba sio ya ccm,ni ya wananchi wote.Ccm imekufa inategemea polisi.ndo ukweli huo.😂😂😂😂
 
Nasema hivi, hamna umma wa kutambia tena, katiba itaandikwa hata kwa kumwaga damu. Mliokuwa mnawatumia kuwabeba, hata wao wanajua hamna support ya umma tena. Ni suala la muda tu, lakini katiba itaandikwa kwa heri ama kwa shwari.
Ni uamuzi wenu lakini kamwe hautofanikiwa ...hakuna mtanzania aliye tayari kuandika katiba kwa kumwaga damu....yupo kibaraka,raia wa nje na mkoloni mamboleo anayechochea haya na stance hiyo hiyo atajibiwa vilivyo.
 
Ilani inajieleza na hakuna sehemu Ilani imebadilishwa.Hakuna kikao cha chama kilichoifuta sehemu hii ya ilani(I wish wafanye hivyo tuendelee kutengeneza wataalamu wa AI na wanasayansi wa kwenda Angani badala ya kutumia fedha za posho)

Swali muhimu...Je mazingira ya kuleta katiba mpya yapo?Je unaleta katiba mpya huku kuna watu hawataki kukaa mezani?

Eti ilani inajieleza, hicho kiilani chenu si ndio kilisema siku 100 mtaanza kuandika katiba leo ni siku ya 1 jinga lao?

Kwanini hamtaki tuanzie katika ile rasimu ya jaji Warioba ya 2014 ambayo ilikua na ni mwiba mkali katika miiko na maadili viongizi badala ya kutapanya pesa kuanza upya kwa kitu ambacho kilikua kimekakilika kwa 60%

Na hao wakukaa mezani ni akina nani na kwanini wakae mezani kuna shida gani jinga lao?
 
Mwenyekiti yeyote wa ccm hatakuwa tayari chama kifie mikononi mwake. Na kitakachoiua ccm ni Katiba mpya. Ukiwa raisi wa nchi kwa Katiba iliyopo hutakubali mabadiliko ya Katiba. Mimi sioni uwezekano wa kuipata Katiba mpya kwa utawala huu wa sasa.
Nadhani utashi kwamba tunatengeneza katiba ya kuwezesha kuiondoa CCM madarakani ndio chanzo cha mkwamo tulionao. Mm nadhani kwenye katiba mpya tulenge kupata mwafaka wa kitaifa, utakaotujengea misingi mizuri ya kisiasa, kiuchumi na kijamii. Tukianza kutaka katiba mpya ya kuitoa CCM madarakani, CCM hawatakuwa na sababu ya kuunga mkono mchakato wa aina hiyo.
 
Mnaweza ku-opt njia hiyo ambayo mmeanza kuijaribu yaani kutaka damu imwagike lakini ni njia isiyowezekana kwa Tanzania..Hata wakati wa kudai uhuru TANU na ASP walikuwa na options hizo lakini kamwe zisingeweza kuleta uhuru wa kweli na kuliacha Taifa salama.
Nguvu hujibiwa kwa nguvu kinzani ...hoja hujibiwa kwa hoja.
We sio Mungu Wala mtabiri
 
Ccm ni matapeli, huenda siku zote ulikuwa huijui.Nadhani sasa unaanza kuona mambo ambayo sisi tulio nje ya box tumekuwa tukiyaona siku zote. Ukishaona chama kinategemea mbeleko ya vyombo vya dola tu kuendelea kuwepo madarakani, basi ujue hilo ni genge la wahuni.

CCM imetekwa na wahuni by People
 
Ni uamuzi wenu lakini kamwe hautofanikiwa ...hakuna mtanzania aliye tayari kuandika katiba kwa kumwaga damu....yupo kibaraka,raia wa nje na mkoloni mamboleo anayechochea haya na stance hiyo hiyo atajibiwa vilivyo.
Nasema hivi, nafasi ya kuandika katiba kwa amani mlipewa mkawaona watu ni wajinga, ule uchaguzi wa juzi umeonyesha umma umewachoka. Hiyo nguvu ya dola na vikundi vya watekaji navyo vitafikia mwisho tu. Hamna nguvu wala uhalali wa kasimamia uandikwaji wa katiba ya watanzania. Na mkilogwa mkaiandika kihuni, tutamwaga damu kuipata inayotakiwa na watanzania, na wote mtaishia jela, ama kukimbia nchi. Inshort katiba mpya ni lazima na sio ombi.
 
Mnaweza ku-opt njia hiyo ambayo mmeanza kuijaribu yaani kutaka damu imwagike lakini ni njia isiyowezekana kwa Tanzania..Hata wakati wa kudai uhuru TANU na ASP walikuwa na options hizo lakini kamwe zisingeweza kuleta uhuru wa kweli na kuliacha Taifa salama.
Nguvu hujibiwa kwa nguvu kinzani ...hoja hujibiwa kwa hoja.
CCM itajibu hoja gani kwasasa? Ukidai Katiba Mpya usipopewa kesi ya Ugaidi basi watakuambia unaitishia Serikali wewe ni muhaini! Wao ata ukiwatama wabadilishe sheria basi umeitisha Serikali.
 
Eti ilani inajieleza, hicho kiilani chenu si ndio kilisema siku 100 mtaanza kuandika katiba leo ni siku ya 1 jinga lao?

Kwanini hamtaki tuanzie katika ile rasimu ya jaji Warioba ya 2014 ambayo ilikua na ni mwiba mkali katika miiko na maadili viongizi badala ya kutapanya pesa kuanza upya kwa kitu ambacho kilikua kimekakilika kwa 60%

Na hao wakukaa mezani ni akina nani na kwanini wakae mezani kuna shida gani jinga lao?
Utawala wa CCM wangekuwa wnaheshimu na kutekeleza ilani yao angalau kwa 60% tu kama taifa tungeshakuwa mbali sana.

Ila huu mchezo wao wa kuifanyie updates kila msimu wa uchaguzi halafu wanaitekeleza kwa 30% tu na blah blah lukuki. Tutaendelea kupiga mark time ya kufa mtu hadi siku Yesu atakaporudi.
 
Ilani inajieleza na hakuna sehemu Ilani imebadilishwa.Hakuna kikao cha chama kilichoifuta sehemu hii ya ilani(I wish wafanye hivyo tuendelee kutengeneza wataalamu wa AI na wanasayansi wa kwenda Angani badala ya kutumia fedha za posho)

Swali muhimu...Je mazingira ya kuleta katiba mpya yapo?Je unaleta katiba mpya huku kuna watu hawataki kukaa mezani?
Kongole comrade, umetoa somo kubwa sana leo:
"Je, mazingira ya kuleta katiba mpya kwasasa yapo?"
Hili ndilo jibu linalohitimisha makala hii!
 
Km nchi inaendeshwa kwa Zidumu fikra za mwenyekiti unategemea nini??
 
Utawala wa CCM wangekuwa wnaheshimu na kutekeleza ilani yao angalau kwa 60% tu kama taifa tungeshakuwa mbali sana.

Ila huu mchezo wao wa kuifanyie updates kila msimu wa uchaguzi halafu wanaitekeleza kwa 30% tu na blah blah lukuki. Tutaendelea kupiga mark time ya kufa mtu hadi siku Yesu atakaporudi.

Ukiipitia rasimu ile ya Warioba iliweka mkazo sana kwenye maadili na miiko ya uongozi.

Kwa katiba kama ingepitishwa tungekua tumefunga mafisadi wengi sana na kuwafisili na pesa za umma kwenda zilikokusudiwa ila walipoona maslahi yao yataguswa vibaya wakaweka vikwazo na kuvuruga kila kitu.

Hizi ilani za CCM ni makaratasi kudanganyia watu utekelezaji wake ni mdogo mno haiwezekani watu wameua halafu wanasema waliouwawa walikua vijana kutoka Kenya.
 
Wakae mezani na matapeli? Ni mara ngapi na miaka mingapi mmetakiwa ipatikane katiba mpya mkagoma? Narudia tena, ile voters turn out imeonyesha mko nje ya muda. Katiba itaandikwa tena ile tunayoitaka watanzania, sio hiyo ya hao majizi wa ccm.
Kuwaita WanaCCM majizi ni kutaka kuwadhalilisha na kuwaondolea credibility yao mbele ya jamii jambo ambalo kamwe hawatolikubali.unawahitaji wana CCM ili upate katiba mpya ...hii ni given kama Pi(kama ulisoma physics lakini).
Ukitaka kuonesha umwamba wako mbele ya wanaCCM na wao wataonesha ubabe wao wa asili kabla hujazaliwa ...CCM walikuwa wababe haswa na hawakuwahi kutishwa na vibaraka au mabwana zao ndio maana leo hii tupo huru kama Taifa.
Kama umeshawajua ni matapeli tumia akili kukaa nao na kuzungumza nao kama matapeli...na wewe wafanyie utapeli ushinde ila kwa kutumia undava na ubabe CCM ni wababe kwelikweli na wameshapitia stage zote za kivita .
voters turn ni ngapi unayoijua wewe?
 
Ukiipitia rasimu ile ya Warioba iliweka mkazo sana kwenye maadili na miiko ya uongozi.

Kwa katiba kama ingepitishwa tungekua tumefunga mafisadi wengi sana na kuwafisili na pesa za umma kwenda zilikokusudiwa ila walipoona maslahi yao yataguswa vibaya wakaweka vikwazo na kuvuruga kila kitu.

Hizi ilani za CCM ni makaratasi kudanganyia watu utekelezaji wake ni mdogo mno haiwezekani watu wameua halafu wanasema waliouwawa walikua vijana kutoka Kenya.
Mambo mengine ni ya kipumbavu sana.
Wanaposema vijana waliouawa ni kutoka nje wanamaanisha mipaka ya nchi haipo salama na vyombo husika havitimizi majukumu yake kikamilifu. Sijui huwa wanawaza nini kabla kuropoka maujinga yao.
 
Nadhani utashi kwamba tunatengeneza katiba ya kuwezesha kuiondoa CCM madarakani ndio chanzo cha mkwamo tulionao. Mm nadhani kwenye katiba mpya tulenge kupata mwafaka wa kitaifa, utakaotujengea misingi mizuri ya kisiasa, kiuchumi na kijamii. Tukianza kutaka katiba mpya ya kuitoa CCM madarakani, CCM hawatakuwa na sababu ya kuunga mkono mchakato wa aina hiyo.
Lengo si kuiondoa ccm madarakani, ni kupunguza mamlaka ya raisi, asionekane kama mungu-mtu kama ilivyo sasa, Tume ya uchaguzi iwe huru kiutendaji siyo kwa jina.
 
Back
Top Bottom