Kuhusu CV na PhD ya Dr. Slaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuhusu CV na PhD ya Dr. Slaa

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Watanzania, Aug 30, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #1
  Aug 30, 2011
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa muda mrefu sasa, suala kuhusu kisomo cha darasani cha Dr. Slaa na hasa PhD limejitokeza mara nyingi. Kwa namna ya pekee nimeshavutiwa kuanzisha mjadala wa tafakuri ya kina kuhusu PhD ya Dr Slaa ambaye ni rais wa moyoni kwa watu wengi. Kwa kuanzia, nawasilisha mawazo ya mwana JF ambaye amedhihaki CV ya Dr Slaa. Ningependa kumwalika ndugu huyu kushiriki katika mjadala ili kujaribu kujibu maswali yafuatayo ambayo yametokana na dhihaka juu ya PhD ya kusomea ya Dr. Slaa.

  Barubaru aliandika kwa kubeza CV hii ya Dr. Slaa hivi:

  ''Profile ya Dr Slaa EDUCATION
  International Eye H. Centre Certificate in Eye Health 1993-1993

  TransWorld Tutorial College, London Certificate in Management 1985-1985

  St. Thomas Aquinas University Advanced Diploma in Rural Development 1980-1981

  St. Urban University, Rome PhD (JCD) Law 1977-1981 [Doctor of Canon Law (Latin: Juris Canonici Doctor or JCD)]

  Kipalapala Seminary Certificate in Theology 1974-1977
  Kibosho Seminary School Certificate in Philosophy 1972-1973

  Itaga Seminary School A-Level Education 1970-1971
  Dung'unyi Seminary School O-Level Education 1966-1969

  Karatu Primary School Primary Education 1962-1965
  Daudi Primary School Primary Education 1961-1961
  Kwermusl Primary School (Mbulu) Primary Education 1958-1960''

  Maswali kwa Barubaru na wachangiaji wengine:

  1. Je kuna tofauti gani ya kifalsafa na ki-empirical katika NADHARIA zinazoongoza utafiti wa sheria za kanisa na sheria nyingine?

  2. Je kuna tofauti gani ya kifalsafa na ki-empirical katika njia za kufanya UTAFITI katika sheria za kanisa na sheria nyingine?

  3. Je ndugu anayedhihaki PhD ya Dr. Slaa anamfahamu vipi Thomas Aquino?

  4. Je ndugu anayedhihaki kisomo cha darasani cha PhD ya Dr. Slaa anafahamu jinsi St. Thomas Aquino (Dr. Slaa amesomea chuo cha St. Thomas Aquino mwasisi wa elimu ya sheria ya nchi za Magharibi kama alivyoonyesha ndugu anayetoa dhihaka) alivyochangia katika maendeleo ya elimu ya sheria katika nchi za Magharibi? Kwa kujibu maswali hayo utaona dhahiri ubora wa hali ya juu wa PhD ya sheria na ya kusomea ya Dr. Slaa.
   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  Aug 30, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kwa mtu mwenye akili timamu mwenye kutaka kuhoji elimu ya Dr Slaa anatakiwa kwanza aelewe 'mfumo' wa elimu ndani ya kanisa katoliki na uhusiono uliopo kati ya elimu hiyo na hii elimu tunayopata kwenye institutions za kawaida. Huwezi kukosoa chemistry wakati haujui hata benson burner ni nini?
   
 3. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #3
  Aug 30, 2011
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndio maana majibu yanahitajika ili kutathmini kisomo cha Dr Slaa na kumaliza maswali au upotoshwaji wa makusudi wa kubobea kwa Dr. Slaa katika kisomo chake cha darasani
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Aug 30, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hata ukiwapa majibu yanayohitajika watu kama Barubaru ambao wanaongozwa na kutawaliwa na udini hawataridhika.
   
 5. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #5
  Aug 30, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hivi bado kuna punguwani anyeulizia usomi wa darasani wa Dr Slaa??
   
 6. Mbugi

  Mbugi JF-Expert Member

  #6
  Aug 30, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,488
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 160
  kama ana elimu inayohusiana na mambo ya dini, huyu anastahili kukabidhiwa mwanakondoo amchunge,
   
 7. Aggrey86

  Aggrey86 JF-Expert Member

  #7
  Aug 30, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 856
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Jamani kuna maprofesa kibao, madokta(phd) kibao lakini huyu jamaa dr.slaa ni Gifted,
   
 8. Aggrey86

  Aggrey86 JF-Expert Member

  #8
  Aug 30, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 856
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Jamani kuna maprofesa kibao, madokta(phd) kibao lakini huyu jamaa dr.slaa ni Gifted, kama bado kuna m2 hamkubali huyu bwana mi ntakaa kimya2 na kumwacha!
   
 9. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #9
  Aug 30, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,063
  Likes Received: 7,531
  Trophy Points: 280
  Bishana na mjinga and end-up being Mjinga.....Huyo anayehoji hayo ni afadhali angekuwa hajui peke yake, tatizo lake ni hajui, halafu anaogopa kujua na kuishia kutotaka kujua...mtapoteza muda naye.
   
 10. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #10
  Aug 30, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Barubaru ni Dr (PhD) anayefanya kazi huko Doha na nakumbuka tukio la kumsaidia Mtanzania mmoja aliyepita hapo Doha na pia kutuma Tende/Halua wakati wa Mwezi wa Ramadhani.
  Ni Mhasibu wa kampuni kubwa tu (Alishajitambulisha hivyo na si kuwa namwaga habari zake) na alishakuwa Mhasibu hapabongo kabla hajatofautiana na Wanasiasa wa CCM anao walamba miguu.
  Kutokana na kuwa na Biashara zake kubwa tu hapa Tanzania, inabidi awatetee CCM kwani Kisasi cha Kikwete kinaweza kuwa kibaya sana kwake. Jamaa anafahamu sana anachokiandika na anafahamiana na Dr. Slaa kwa karibu tu na si kama sisi wengi wetu hapa tunamsoma tu.
  Sijui walikosana wapi hadi akaanza kumchukia Dr. Slaa au huyu Barubaru wa sasa, siyo huyo Msomi aliyepo Doha (PhD). Au jamaa ANAPOTEZA tu muda hapa na kama ambavyo aliandika mwanzo, yupo kujifunza Kiswahili na kuhakikisha hasau. Anyway, kama hasomi alama za nyakati na anazidi kumshambulia Dr. Slaa, siku ikifika basi kampuni zake itabidi zimulikwe vizuri ki Sheria.
   
 11. kanyasu

  kanyasu JF-Expert Member

  #11
  Aug 30, 2011
  Joined: Feb 9, 2009
  Messages: 235
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  mfumo wa elimu wa nini bwana huyui hana PHD ya academician ni ya heshima kwa sheria za kanisa,uliona wapi PHD unapewa baada ya kusoma diproma bwana?
   
 12. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #12
  Aug 30, 2011
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Haya wenye PhD za kweli ni Dr.JK, Dr.Nagu, Dr.Lwakatare na Dr.Nchimbi ila Rais wa kweli ajaye ni Dr.Slaa.
   
 13. F

  FJM JF-Expert Member

  #13
  Aug 30, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  @Kinyasu, ndio maana nilisema kwa mtu kutaka kuhoji elimu ya Dr Slaa ni vema ajue MFUMO wa elimu ndani ya kanisa katoliki. Kwa majibu yako nahisi wewe binafsi huelewi mfumo wa elimu unaotumiwa na kanisa katoliki. PhD ya Slaa siyo ya heshma, kaisotea ndugu yangu.

  Sasa hapo kwenye red: Naomba ruhusa wanJF niweke majibu ya mdau mmoja toka wanabidii aliyotoa kuhusu elimu ya kanisa katoliki. Alikuwa anamjibu mdau mwingine aliyeonekana kuhoji elimu ya Dr Slaa bila kujua mfumo uliompa PhD. (sitotaja majina lakini na hakika huyu mdau wa wanabidii hatokasikira mimi kuweka mchango wake hapa). here we go...

  Tukianza na Kipalapala, hapa mwanafunzi anasoma form 5 & 6 pamoja na masomo ya Theology na baada ya hapo huunganisha na degrii ya theology.

  "Kipalapla kama ilivyo Institutions zote za Kanisa Katoliki (kwa level ya Philosophy na Theology) iiko affiliated na vyuo vikuu mbalimbali duniani kutoka nchi moja hadi nyingine.

  Mfano, wanaosoma Zomba Theological College Malawi (Theology) na Kachebere Philosophical College (Philosophy) mpakani mwa Malawi na Zambia wanafuata marking scheme ya Chancellor College - University of Malawi. Kuna chuo kingine kiko Balaka Consorsium Philosophical College nadhani kiko affiliated na St Urban University, Rome.

  Missionary Institute London (MIL) iko affiliated kwa Middlesex University (chuo cha serikali cha Uingereza) na Luvein University (Belgium). Wanaofuata mfumo wa Middlesex University kupata BA wanasoma miaka 3 na passmark yao ni 40%. Wanaofuata mfumo wa Luvein University kupata BA wanasoma miaka 4 na passmark yao ni 60%. Muhula unaanza Oktoba na kwisha Juni (miezi 8).

  Mfumo wa kutoa final mark ni 1) class presentation na participation 2) essay writing 3) oral examination 4) defence of dissertation mbele ya internal & external examiners. Pia mtu anayepata first class, papers zake lazima ziwe marked na internal na external examiners na ajadiliwe kama anastahili first class degree na siyo tu kupata kwenye karatasi. Pia anayeshindwa, paper zake zinasahishiswa na examiners tofauti ili kuonesha kashindwa kweli au kama amepunjwa marks.

  Kwa Tanzania, kwa sasa vyuo vyote kwa level ya Philosophy na Theology viko affiliated na St Urban University, Rome. Zamani, falsafa ilikuwa miaka 2 (sasa ni 3) na teolojia ilikuwa miaka 3 (sasa 4). Mtu akimaliza (Tanzania) alikuwa anapata certificate siyo kwa sababu masomo yalikuwa level ya chini ila kwa sababu maaskofu walikuwa hawajaridhia wahitimu wao kupata digrii licha ya kuwa walikuwa wanaombwa wanafunzi wapewe magamba kama ilivyokuwa kwenye vyuo vingine. Ilichukua muda kidogo.

  Lakini kama mtu aliendelea na masomo ya juu walithamanisha masomo yale kwa chuo ambacho mtu anaenda kusoma maana content ya syllabus ya masomo ya falsafa na teolojia ni (universal) kwa vyuo vyote vya Kanisa Katoliki duniani tofauti ni kwa kila nchi wanaongeza mambo yanayohusu cultural understanding ya nchi husika including its legal system.

  Uganda mtu akimaliza Jinja Philosophical College (Philosophy) anapata BA katika Philosophy. Akiendelea na Theology chuo kingine, anapata BA katika Theology na kuna vyuo vingine akimaliza Theology anapata MA. Inategemea chuo kina mfumo gani na kinafundisha nini - maana kuna baadhi ya masomo kama mtu hakuyafanya wakati wa philosophy atayafanya wakati wa theology.

  Kwa baadhi ya vyuo, mtu mwenye BA ya Philosphy na BA ya Theology, akiendea na masomo ya juu 'specialisation', anaenda moja kwa moja kusoma PhD kulingana na vigezo walivyoweka (mfano, vyuo ambavyo vinafundisha Philosophy na Theology kwa pamoja). Kwa baadhi ya vyuo masomo haya yanatenganishwa - yaani, mwanafunzi anaamua ku'specialise' kwenye pure philosophy au pure theology. Na katika masomo yote mwanafunzi anafundishwa the secular view na religious view.

  Maana ni hasa kumwezesha mwanafunzi kupata "solid and consistent knowledge of man, the world and God... The students should rely on that philosophical patrimony which is forever valid, but should also take account of modern philosophical studies, especially those which have greater influence in their own country, as well as recent progress in the sciences. Thus, by correctly understanding the modern mind, students will be prepared to enter into dialogue with their contemporaries." ( Vatican II, Training of Priests, Paragrapah No 15).

  Kuna vyuo kama alikosoma Dr Slaa lecturers wote ni wa level ya profesa na kwenda kusoma huko mpaka uwe 'exceptional student' nadhani kama sikosei wanachukua wale tu wenye 'first class'.

  Kitu kingine ninachoona kinampa wasiwasi (jina limehifadhiwa) ni pale anaposoma "Canon Law" au "Catholic Education" kwa kudhani padre anasoma tu biblia au mafundisho ya Kanisa. Mfano, Dr Slaa amespecialise katika Canon Law ambayo ndiyo mother of secular law na kusoma Canon Law ni lazima kuanza na how law developed na mpaka kuja kugawanyika into secular na religious laws.

  Advantage ya Dr Slaa si tu kwamba ana'knoweldge' ya Canon Law lakini pia nini kinaitwa secular law na kwa nini - tofauti na similarities. Mfano, definitions of what is an irregurality, malice aforethought, the difference between legality and validity of an act, what is a valid marriage and a legal marriage, etc.

  All Catholic Universities undertake secular studies mfano ni Catholic University of East Africa (CUEA), Kenya, ambako hata Waislamu wanasoma huko, St Augustine, Mwanza, Luvein University etc. kwa hiyo mtu akihitimu kwenye vyuo hivyo, huwa haangaliwi kuwa amesoma elimu ya dini bali kwamba ni mtaalamu katika taaluma fulani aliyoisomea.

  Tofauti kwa mapadre ni kwamba mfumo wao wa mafunzo unachukua muda mrefu na wanajifunza mambo mengi - maana hadi kufikia upadre ni mpaka uwe walau umesoma miaka 10 baada ya Form VI". (mwisho wa kunukuu)
   
 14. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #14
  Aug 30, 2011
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,653
  Trophy Points: 280
  HAPANA; hili lilishamshinda kitambo!!!!!!
   
 15. M

  Moghati Member

  #15
  Aug 30, 2011
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 88
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  <br />
  <br />
  kumbe huyu jamaa kaonganisha vicertificate kibao vya ajabu, alafu hana hata degree,,,ni kijiproma tu...alafu cv ina utata mbona form 5na6 kasoma mwaka mmoja? mchakachuaji huyu jamaa...alafu umesahau cv yake ile aliyo chakachua hela za msaada wa walemavu pale baraza la maskofu akiwa katibu mkuu na wakamtimua...teh teh teh!!!
   
 16. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #16
  Aug 31, 2011
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hujasaidia kujubu hata swali moja kati ya maswali manne yaliyoulizwa kwenye threadi.
   
 17. l

  lady roranky Member

  #17
  Sep 1, 2011
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 75
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  <br />phd anayo na kasotea kama kwako phd ni ndoto so sorry ,he z the person who can show hz phd without certficates coz he z more than a bright ,active mind he wil always be the topic coz he has somethinng different wt others
  <br />
   
 18. HT

  HT JF-Expert Member

  #18
  Sep 1, 2011
  Joined: Jul 29, 2011
  Messages: 1,899
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Phd haziongozi nchi. So I don't care.
  Alimradi anaweza kuendesha nchi tukaendelea, vingine ni irrelevant
   
 19. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #19
  Sep 1, 2011
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  <br />
  <br />
  umesema sawia ! Umewaeleza vizuri.
   
 20. m

  mwanza JF-Expert Member

  #20
  Sep 4, 2011
  Joined: May 7, 2009
  Messages: 508
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60
  Ni afadhali PHD ya Dr. Slaa kuliko PHD ya Prof. Lipumba kama unataka kujua ukweli nendaserikalini uwaulize ni mwanasiasa gani huwa akiongea wanakosa usingizi au nenda kwa wananchi uwaulize ni mwanasiasa gani akiitisha mikutano watajazana kumsikiliza. Dr. Slaa ni exeptional hata rais anajua
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...