safuher
JF-Expert Member
- Feb 11, 2019
- 12,314
- 18,146
Shukrani kwa hii nyongeza ya nguvu mkuu.Mkuu Safuher, umetoa majibu mazuri sana, majibu hata mimi ningejibu kimsingi ningejibu hivyo hivyo.
Ila cha kuongeza kidogo ni kwamba wahenga wanasema shida ni mgunduzi na kitu chenye manufaa hudumu manaa yake ni kwamba siku zote akili ya mwanadamu inafanya kazi kupambana na mazingira yake, ilipofika wakati ambapo muda ilibidi upimwe ndipo mwanadamu toka awali akabuni mbinu mbalimbali kupima muda kwa siku- hususan walitumia jua kujua wakati wa mawio,mchana na machweo pia walitumia vivuli vya miti na vijiti vinavyobadilika kimo kutokana na mwendo wa jua nk,pia watu hao walitumia matukio makubwa kama vipimo vya wiki,miezi na miaka, kwani utasikia wazee wa zamani wanakuambia kwamba; "mimi nilizaliwa mwaka wa nzige"yaani ni kipindi kile ambacho nzige wengi walitokea katika eneo lao.
Leo binadamu amefikia maendeleo makubwa makubwa mno sio tu ya kupima muda bali hata kujua muda uliopita na kuuhifadhi tofauti na ilivyokuwa karne zilizopita, leo kuna "nuclear clock" saa inayolinda muda kwa usahihi zaidi kuliko saa zote duniani (karibu saa zote zinapoteza majira kadiri muda unavyopita). Bado uvumbuzi unaendelea kila uchao na mambo yasiyokuwa na manufaa binadamu huyaacha na hubaki na yale yenye manufaa tu ndivyo Mungu alipanga hivyo.
Muda ni nini?, hakuna definition maalumu ya muda, ila A, Einstein mwanafizikia maarufu akitoa definition ya muda na alisema; "time is what stops two things from happening at the same time"--- yaani; muda ni ile hali inayozuia vitu viwili visitokee kipindi kimoja. Mfano kama vitu viwili vitasnza kutenda kazi kwa pamoja na kuacha kutenda kwa pamoja na ukaulizwa utoe utofauti wa muda kati ya vitu hivyo vilipoanza kutenda kazi na kumaliza utaona muda ni sufuri lakini vingeanza kipindi tofauti hapo ungepata muda uliokuwa tofauti--- hiyo ndiyo definition ya muda/wakati iliyotolewa na A. Einstein.
Mungu ni wa kushukuriwa aliyeweka mazingira hadi sisi binadamu tukaweza kupima muda kwa faida yetu.
Ila sasa ina maana kwa mujibu wa bwana eiinsten Ina maana mimi na wewe tukianza kukimbia dk ya 1 mpaka dakika ya 10 tukasimama maana yake ni kwamba wote itakuwa tumetumia dk 10 kukimbia.
Sasa hapo dakika kumi ni MUDA ambao ni sawa na sekunde 600.
Kwa mujibu wa huyo nguli na huu mfano anatuambiaje kuhusu maana ya muda?
Mana sijaelewa vizuri
Maelezo hayo nimeyaona kwa kiasi fulani ndiyo yanakaribia kujibu msingi wa maswali yaliyoulizwa na mleta mada, na hapa chini nimejaribu kutafsiri kwa kiswahili na kama atakuwepo mjuzi zaidi naye anakaribishwa kutoa tafsiri nzuri zaudi.