Mkuu haya mambo wala yasikuumize sana kichwa.haya mambo ni kukopi na kupesti tu.
Yani vimeitwa hivyo kwa sababu ya huyo mvumbuzi kaviita na yeye ndo kavipima.
Ndo mana lile duara lau angetangulia mtu akaliita lile ndo pembe tatu na pembe tatu ndo duara basi tungeamini hivyo na kukubaali na tungezowea.
Zamani mambo yalikuwa yanaenda kwa majira ya kuangalia machomozo na machweo ya jua tu.
Hivyo kipimo cha sekunde huyo aliyeweka wala hakuzingatia vigezo vyovyote bali ilikuwa ni maoni yake tu na yakatumika ulimwengu mzima.
Na pia huwenda angetokea mtu hii dakika angeweka ndo sekunde basi ingekuwa hivyo na tungezOwea tu bila shida.
Ni sawa na moja kuiandika 6.waliotangulia wangeliita hiyo ndiyo moja basi na sisi tunhezowea hivyo hivyo.
Lau kama hii namba 5 waliotutangulia wangeiita mbili basi tungezowea hivyo lakini hawakuita hivyo.
Ukisema muda kwa kukusudia sekunde,dakika,saa,siku,wiki,mwezi na mwaka basi tujue kwamba hayo masekunde na madakika kuna watu tu walijifanya wasomi wakaweka vipimo vyao.
HIVI fikiria kwanza kama saa hizo za mishale na namba zisingekuwepo unadhani kungekuwa na kitu kinaitwa dakika?
Je sekunde ingekuwepo?
Je saa ingekuwepo?
Kama vingekuwepo vingepimwa kwa kutumia kitu gani kinyume na hizi saa zanamba na mishale?
Hapa tunaweza kutizama na kuona kwamba aliyeleta sekunde na dakika basi ndiyo aliyeleta saa.
Huwenda zamani walikuwa hesabu zao ni mwaka na siku na nyakati kwa kuangalia masika mpaka masika wanajua sasa ni mwaka huo.
Kwa kuangalia kuchomoza kwa jua wanajua siku mpya hiyo.
Kwa kuangalia kuwa kati kati kwa jua na likawa kali wakajua kwamba sasa ni mchana na njaa zikawauma na kiu zikawashika wakatamani kula.
Na kwa kuingia giza wakajua sasa ni usiku huo wakapatwa na usingizi wakatamani kulala.
Lakini sasa kusema kwamba sasa hivi mi saa saba na dakika 5 haya ni maoni ya watu ambao wametengeneza hizo saa na teknolojia.
Hivi wangesema kwamba pale jua linapokuwa kali ile ndo saa mbili mchana nani amgelikataa kwa wakati huo waliouanzisha?
Kwa hvyo ni mambo madogo tu haya.
Sent using
Jamii Forums mobile app