Kuhatarisha usalama wa Taifa? Give me a Break!

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,202
5,014

Kwa wasiojua majukumu ya taasisi hii wa-download attachment hii:


 
Hii ndo Tanzania bwana. Baadae tutatafuta mwekezaji atusaidia kusimamia usalama wa taifa. Yaani kila kitu kimebinafsishwa - hadi kufikiri. Kama kweli Chiligati amesema walipitiwa basi iko siku hii nchi tutakuwa na rais asiye mtanzania. Tatizo letu ni kulindana na kuogopa kufanya un-popular tough decision. Watu wanajua hata wasipotimiza majukumu yao nyeti hakuna atakayewawajibisha.

More to come...let us wait and see
 
Baija, ni muda mrefu tume-conclude humu jamvini kwamba Usalama wa Taifa ((UWT) ile wing ya CCM ya kinamama should be UW-CCM)nchi hii ni kama hakuna. Kimsingi wao wamekuwa kama Security & Intelligence wing ya CCM katika kupambana na upinzani wowote dhidi ya maslahi ya chama.

Mgeni yeyote toka popote wa rangi yoyote ya ngozi anaweza kuingia Tanzania akafanya anachotaka kisha ama akaondoka zake au akaendelea kudunda nchini raha mustarehe. Nchi inavyoyumbishwa kiuchumu, kiutamaduni na kimaadili ni hatari kwa usalama wake.

Ni jukumu la UWT ku-rectify issues kama hizo lakini hapa Tanzania, CCM wanachakachua kila kitu yet wao (UWT) wanakenua meno as long as akaunti zao zinanona.
 
Sidhani kama U/Taifa ni wazembe kwa kiasi hiki.

Ninachokiona mimi tatizo ni Ubishi na kupenda misifa kwa viongozi wetu wakubwa.

Kwa mfano swala la Masauni na hata lile la Chenge kurudishwa barazani lilibezi kwenye mbwembwe na ubishi tu.

Ni mambo ambayo yalikuwa wazi wazi.
 
kuna haja ya badiliko katika ofisi hiii, kunapotokea mabadiliko makubwa kwama yetu kutoka mfumo wa chama kimoja kwenda vyama vingi ilikuwa lazima ofisi hii ifumuliwe na iundwe upya, sasa sisi wamefanya kimya kimya......, anajua mkapa na wenzake
 

Kuna siku Hassy Kitine alisema haya alionekana mjinga. Alisema mawaziri wanaoteuliwa na rais wengi hawastahuli kuwepo kwenye nafasi ile, kwa kuwa usalama wa taifa haushirikishwi na wenyewe hautaki kujishirikisha. Kila siku watu wanasema usalama wa taifa wa sasa si kwa jili ya usalama wa taifa, ni usalama wa CCM, sasa naona hata usalama wa CCM inadhindwa kuulinda.

Kama maamuzi makubwa ya chama yanafanywa na NEC, kama maamuzi makubwa ya NEC yanaihusu Tanzania, na kama yanafanywa na wasio watanzania, how can you trust CCM. It is so stupid kusema eti walitupiwa, so stupid answer ina maana hata CCM haina idara ya usalama. Kama Bashe na wajumbe wengine wa NEC ni Bashe like, what do you expect. Maamuzi yatakuwa kwa manufaa ya Tanzania au ya wageni, au wafanyabiashara waliowaweka madarakani.
 
Kwa kweli usalama wa Taifa, ni moja kati ya Idara ambazo zimekufa kabisa Tanzania, kwa sababu zimebadiliza role zake kabisa. Najua wanasoma hapa Jamii Forums, subiri niwakukumbushe, hawa watu wameacha kulinda maslahi ya taifa, wanalinda viongozi, tena bora wangekua wanawalinda physically, yaani wanawalinda viongozi kwenye kashfa tu, ila physically hamna ulinzi wowote wa maana, sema tu nchi yetu ni ya amani.

Hapa Tanzania, watu toka nchi jirani wanaingia tu bila hata passport, achilia mbali visa. hebu check mikoa ya mipakani yote kuna wageni kibao, ambao wanaenda sehemu yeyote na kufanya chochote. Watu wanaambiwa sio raia wakati walishakua viongozi wakubwa tu, wanasahau kwamba usalama wanadhalilika.

CHANZO CHA TATIZO

Chanzo kikubwa cha tatizo ni Usalama wa Taifa kuwa chini ya executive, yaani wanapelekwapelekwa tu na Rais au hata Waziri, wanafanya kazi kwa maelekezo ya Rais, hii ni hatari sana kwa usalama wa nchi yetu, nchi nyingine nyingi tu ulimwenguni, usalama wa taifa una nguvu kuliko hata Rais, usalama wa Taifa unamuonya na kumkataza Rais kufanya kitu ambacho hakina maslahi ya Taifa. Na ndio maana nchi kama Marekani usalama wa Taifa wanaweza kumuua hata Rais kama anafanya vitu ambavyo havina maslahi ya Taifa. Kwa muundo huo kila mtu ataheshimu usalama wa Taifa.

USALAMA WA TAIFA BONGO? WALISHAFULIA!!!!
 
Ukiona tumefikia hapa... basi jua tatizo si la leo, ni la zamani sana na ni sugu

Kwani si tunaona mambo ya akina Upson na Mwakipesile Mbeya??? wale walikua magwiji huko... unakumbuka Kombe???

Kwahiyo ndugu yangu mimi sioni kama tunaelekea pabaya... tulikua pabaya na nio tuko kwenye mpito....
 
Usalama wa Taifa ni waajiriwa wa serikali.

Je nini majukumu ya chombo hiki na mipaka yake? Kiko chini ya Idara au taasisi gani na kinawajibika kwa nani? Kama alivyowahi kusema Hans Kitine kuwa chombo hiki hakisikilizwi na hao wanaotoa maamuzi.

Imefika wakati wa wahusika kuwaondoa dukuduku wananchi kuhusu chombo hiki. Kama ni kukiboresha au kukiunda upya kukidhi mahitaji ya karne hii,yetu macho.
 

Mkuu ukisikia jinsi jamaa wanavyofanya kazi hata huwezi kuamini.

Kuna wengine wanajua a-z na ripoti zinawafikia wanasiasa, lakini wanasiasa wetu hawana uwezo wa ku act on intel reports, isipokuwa wana uwezo sana wa kuzipoliticize. Tulifanya ujinga pale tulipopeleka maamuzi yote chini ya wanasiasa ambao hawana uwezo, can you believe Sofia Simba ndio mmoja wa wakuu wa kisiasa wa idara hiyo, angalia rekodi yake kama kweli anastahili kuwa pale.
 
Hata tulete UWT toka wapi, kama kuna kiongozi wa hovyo 'hapo juu' kama ilivyo sasa hakuna jipya.

UWT wanajua mengi sana na wangeweza kusafisha hii nchi.

Ni mabingwa wa chabo, nani kalala na nani wapi hiyo ndio kazi waliyobaki nayo. Yanayobumburuka sasa hivi ni matokeo ya ujinga na upuuzi wa watawala wa Tz.

Walioharibu UWT ndio wako madarakani sasa hivi. Waliiharibu iwasaidie kuwachafua wengine. Sasa jamaa walishazoea 'kula nyama za watu', wanaendelea
 
shida ni kua Rais kazungukwa na watu ambao Jenerali Ulimwengu amewaita wapuuzi katika makala yake ya wiki iliopita.
Fikiri juu ya wasaidizi wafuatao wa MH.Kikwete.
Mzee Makamba Yusuph
TAMBWE Hiza
John Chiligati
Sophia Simba
kulikua na Kingunge Ngombare Mwiru
Mtoto wake Ridhwan
mkewe Mama Salma
...hao ndio wasaidizi na washauri wa Rais ,mkama mwenyekiti wa chama pia.
...Orodha ni ndefu mnaweza kuendelea, katika hali hiyo ya uteuzi wa Rais, UWT , wafanye nini ? wanaangalia tu, by the way wao kazi yao sikusaidia kazi za uteuzi za CCM, Kazi yao ni usalama wa Taifa na sikufuatilia mambo yao ndani ya chama, Bashe , MALISA, hao wote walikua na wajibu waKichama zaidi.
labda uteuzi wa Chenge.
 

Umemsahau February, BumbuliOne
 
One of the techniques that the Kikwete government is using to neutralize the legislature is to fill it with intelligence operatives masquarading as MPs!Do you know how many intelligence officers were MPs in the just concluded parliament? You guessed right.! kazi yao ni kulinda maslahi ya viongozi na sio ya Taifa.
 
========

Hakuna nchi iliyowahi kufanikiwa kwa kuwafanya wana usalama kuwa wanasiasa. Hawa watu kama wameelemishwa vizuri huwa wanaharibiwa akili zao za kawaida na kuvishwa fikira zisizokuwapo ili waweze kufanya kazi yao vizuri. Sasa ukiwafanya wanasiasa, unategemea nini?

Nimewaona wakituhumiana humo bungeni na serikalini na sasa tusubiri watakavyoanza kuripuana kwa risasi. Undumila kuwili umewatawala kila wakati - mara hao kwa Lowassa, asubuhi wako kwa JK, keshikutwa kwa Sitta. Na hakuna hata mara moja utawasikia wakizungumza juu ya maslahi ya wananchi. Lugha yao ni maslahi ya kundi lao na kiongozi wao. Tumeliwa.
 

Issue ya chenge na idara ya usalama wa taifa ina uhusiano gani?
Kufoji umri na idara usalama wa taifa vina uhusiano gaini?
Na suala la kutokuwa uraia lina uhusiano gani na idrara ya usalama wa taifa? Kwa nini huzungumzii idara ya uhamiaji ambayo ndio imepewa jukumu la masuala yote ya uhamiaji?

Should we please try to analyse things instead of jumping to conclusions?
 
========

Alah

Tumegusa kitumbua! Basi tupe Job Description ya Idara ya usalama wa Taifa.

Kwangu, kabla Rais hajateua mtu kwa nafasi kubwa kama ya Waziri Chenge au kabla hajapendekeza mtu kama Masauni kuingia kwenye Cental Committee, ilibidi Idara ya Usalama impe clearance kuwa watu hawa ni safi. Hata Idara iliposhindwa kufanya hivyo, vyombo vya habari vilipiga kelele (at least kwa case ya Chenge), na hapo bado idara ya Usalama iliendelea kulala usingizi mpaka Chenge mwenyewe alipoamua kujiuzuru. Kwa kuwa wewe waonekana ni upo idara hiyo, tuelimishe sisi wajinga tujue ni nini kazi ya idara hiyo ya usalama.
 

Unaona sasa? Kwako wewe ndio unavyoona hivyo. Under what basis? can you support your argument au unaongea tuu. Mdau nakushauri ukasome kwanza Sheria ya Idara ya Usalama wa Taifa Na. 5 ya Mwaka 1996. Baada ya kusoma hiyo sheria ndio utajua mamlaka ya hiyo idara. Tusiongee tuu ili mradi tumeongea.
 

Badala ya kuuliza kama Usalama wa Taifa wapo wapi, pengine na sisi wenyewe tujiulize tupo wapi wakati nchi inaelekea pabaya.

Mie ninavyoiona Idara hiyo sio chombo cha kumulika kile kinachotendeka nchini pamoja na ukweli kwamba kama sikosei kazi yake kubwa ni kuhakikisha kwamba Taifa linaendelea kuwepo. Idara hiyo kwa kiwango kikubwa, kama ilivyo kwa vyombo vingine vya polisi, Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Uhamiaji na Magereza, inafanya kazi kwa ushirikiano na wananchi na hasa Wazalendo, kwa bahati mbaya ingawa sijui kama Idara hiyo ina watuimishi wangapi, lakini siamini kama wapo kila mahali.
 
Madudu yanayofanyika ambayo mtoa hoja anasema yangeshughulikiwa na Idara hiyo, yanaweza kuwa hayashughulikiwi kwa sababu ushirikishwaji wa wananchi yawezekana ni mdogo sana au haupo kabisa. Wananchi ambao ni pamoja na mtoa hoja wanakaa kimya pengine wakifikiri kwamba Idara na vyombo vingine vya usalama vitafanya kazi kwa kupiga ramli. Haiwezekani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…