Kuhani Musa Richard Mwacha ni nani?

Niliwahi kukisia uwezo wako kiakili ila sikuhitimisha kuwa ni mdogo namna hii, tangu dunia ianze [ukiacha ile stori ya Yesu]…. ulisikia wapi wafu kufufuka katika maisha halisi?

Kama nimeweka uzi hapo tujadili kinachoendelea badala ya kuja na hoja unakuja na maneno matupu lazima wewe utakua na akili fupi kuliko mkia wa sungura

Issue zinazohusu jamii hujadiliwa kwa hoja na watu kuelimika na sio kuja na blahblah
 
Natamani sana tuthubitishe ni trick kwa umma wa watanzania ndio maana nimeambatanisha video na maelezo
Kuthibitisha nini ? (kwamba watu hawapati ahueni baada ya kwenda kwa mtu kama yeye ) ? Huenda wanapata ahueni kwa kuwapata support na kuwapa hope; ila anachowapa huenda ni kama vile wewe ukipewa sukari ukaambiwa ni pain killer (Imani yako itakuponya)

Kwahio kwenye suala la Imani (its more you na kuamini kwako) kuliko yeye ; Yeye ni support tu ya kukupa Confidence
 
Waende mahospitalini wakaponye watu na mortuary wakafufue maiti. Hizo nyingine ni michongo

Fanya uchunguzi kwanza ndio utoe hoja!? Hao wanaofufuka nini kilitokea? Walifuatwa mortuary au makaburini?
 
Kuthibitisha nini ? (kwamba watu hawapati ahueni baada ya kwenda kwa mtu kama yeye ) ? Huenda wanapata ahueni kwa kuwapata support na kuwapa hope; ila anachowapa huenda ni kama vile wewe ukipewa sukari ukaambiwa ni pain killer (Imani yako itakuponya)

Kwahio kwenye suala la Imani (its more you na kuamini kwako) kuliko yeye ; Yeye ni support tu ya kukupa Confidence

Imani ni swala la mtu binafsi ila kujadili hapa ni elimu kwa wengi. Ndio maana ya mjadala
 
Imani ni ufunuo wa Mungu kwa mwanadamu; ni ile hali ya akili ya mtu kupokea ukweli uliofunuliwa na Mungu akiambatanisha nafsi yake kwa Mungu.

Kuhani Musa Richard Mwacha amejulikana kama mtumishi wa Mungu mwenye imani kwa Kristo. Na amekua na huduma yake katika jiji la Dar es salaam kwa miaka michache sasa.

Ukifuatilia Kwa muda mfupi sana utakutana na mambo mengi sana na kati ya hayo mengi ni style ya mahubiri yake, miujiza na maajabu kwenye ibada zake na idadi kubwa ya waumini alionao ndani ya muda mfupi sana maana miaka 3 au mi4 bado huduma ni changa.

Ila swali moja la msingi huyu Kuhani Musa ni nani haswa?

Hizi shuhuda zimetolewa hadharani, ni shuhuda zinazodhihirisha mambo magumu kufikirika katika hali ya kawaida. Ila hawa walioshuhudia wapo kati yetu, mtaani kwetu hata majumbani kwetu, kigoma, chato, kilimanjaro, sumbawanga, kagera, Dar es salaam mmetisha sana. Wenyeji wa huko mnasemaje kuhusu Kuhani Musa?

Fred William Rwegasira.
View attachment 2123813
Mr Rwegasira ni mzaliwa wa mkoa wa Kagera, Bukoba kule, Mkazi wa Salasala - Dar es salaam. Na sasa anaishi kimara

Innocent Carol Paulo
View attachment 2123832
Innocent Carol Paulo ni mzaliwa wa Chato. Na mkazi wa Tabata - Dar es salaam

Levina Lyamuya na mdogo wake
View attachment 2123876
Levina ni mwenyeji wa Kilema, Moshi- Kilimanjaro

Malkia

Bwana Yusufu

Yusufu ni mzaliwa na mwenyeji wa kigoma

Sumbawanga mtoto afufuka
ttps://youtu.be/PHUUbiYOEBY

Filmee
 
Kama nimeweka uzi hapo tujadili kinachoendelea badala ya kuja na hoja unakuja na maneno matupu lazima wewe utakua na akili fupi kuliko mkia wa sungura

Issue zinazohusu jamii hujadiliwa kwa hoja na watu kuelimika na sio kuja na blahblah

Nimekuuliza kama wewe umewahi kusikia mfu kafufuka [mbali na shuhuda za madhabahu uchwara], kisha unasema hizi ni blah blah…. kisa tu hizo clips zilizoandaliwa.!

Kujadili kwa njia shirikishi, nimekuachia ujiulize…. sio wakati wote uchukue notisi.
 
Imani ni swala la mtu binafsi ila kujadili hapa ni elimu kwa wengi. Ndio maana ya mjadala
Ni kweli ila tunajadili nini labda ?

Kwamba fulani ni nani ? (Sawa ni Swali zuri wanaojua watajibu na huo mjadala unawezekana)

Kwamba fulani anasaidia au hasaidii watu ? (Huenda anasaidia sijui wanaokwenda pale wanataka nini, emotional support, hope, maneno ya kufarajiwa au support / nguvu ya kupewa confidence katika wakati mgumu walionao) hayo yote wanaweza wakapata so long as mtu huyo ana people's skills, ila huenda anachowapa ni kama waliopewa sukari wakiambiwa ni pain killer na kutokana na nguvu ya imani kweli maumivu yalipungua...

Au tunajadili so called miracles ? Ndio hapa point yangu inakuja kutokujua trick inafanyikaje haimaanishi kwamba trick hio ni kweli simple answer huenda ni kwamba mimi ndio sijui inafanyikaje..., my litmus test huwa ni vitu vinavyodefy logic ni kuviangalia kwa jicho la tatu na sio kuvimeza vizima vizima....
 
Nimekuuliza kama wewe umewahi kusikia mfu kafufuka [mbali na shuhuda za madhabahu uchwara], kisha unasema hizi ni blah blah…. kisa tu hizo clips zilizoandaliwa.!

Kujadili kwa njia shirikishi, nimekuachia ujiulize…. sio wakati wote uchukue notisi.

Povu la nini!? Watu wako hapo na maeneo wanayotoka yapo... badala ya kuja na jazba na blahblah tuje na hoja za kuonyesha hayo mambo hayawezekani kama unavyoona
 
Ni kweli ila tunajadili nini labda ?

Kwamba fulani ni nani ? (Sawa ni Swali zuri wanaojua watajibu na huo mjadala unawezekana)

Kwamba fulani anasaidia au hasaidii watu ? (Huenda anasaidia sijui wanaokwenda pale wanataka nini, emotional support, hope, maneno ya kufarajiwa au support / nguvu ya kupewa confidence katika wakati mgumu walionao) hayo yote wanaweza wakapata so long as mtu huyo ana people's skills, ila huenda anachowapa ni kama waliopewa sukari wakiambiwa ni pain killer na kutokana na nguvu ya imani kweli maumivu yalipungua...

Au tunajadili so called miracles ? Ndio hapa point yangu inakuja kutokujua trick inafanyikaje haimaanishi kwamba trick hio ni kweli simple answer huenda ni kwamba mimi sio sijui inafanyikaje..., my litmus test huwa ni vitu vinavyodefy logic ni kuviangalia kwa jicho la tatu na sio kuvimeza vizima vizima....

Rudi kasome maada uelewe
 
Nimekuuliza kama wewe umewahi kusikia mfu kafufuka [mbali na shuhuda za madhabahu uchwara], kisha unasema hizi ni blah blah…. kisa tu hizo clips zilizoandaliwa.!

Kujadili kwa njia shirikishi, nimekuachia ujiulize…. sio wakati wote uchukue notisi.

Nimewahi kusikia ndio, ila kuona bado.... ndio nataka sasa tufikie hao waliofufuka tuhakikishe kweli walikufa.
Kama walikufa lazima ilithibitika kitabibu wamekufa, lazima walipewa nyaraka za kifo na kuzika, lazima wazikaji wapo wakiwemo viongozi wa dini na serikali

Na huo ndio msingi wa mjadala

Sio kukataa au kukubali ukiwa hujui hata unachokikataa wala kukikubali zaidi ya blahblah
 
Duuh...! MUNGU atuongoze. Kukua kwangu kote sikuwahi kufikiria ipo siku dini itageuka kuwa biashara kubwa hivi. Mataperi wamejaa huko. Kweli watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.
 
Nimekuuliza kama wewe umewahi kusikia mfu kafufuka [mbali na shuhuda za madhabahu uchwara], kisha unasema hizi ni blah blah…. kisa tu hizo clips zilizoandaliwa.!

Kujadili kwa njia shirikishi, nimekuachia ujiulize…. sio wakati wote uchukue notisi.

Matendo 26: 8 "Kwa nini limedhaniwa kwenu kuwa ni neno lisilosadikika, kwamba Mungu awafufua wafu?"
 
Duuh...! MUNGU atuongoze. Kukua kwangu kote sikuwahi kufikiria ipo siku dini itageuka kuwa biashara kubwa hivi. Mataperi wamejaa huko. Kweli watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.

Mungu ametupa akili za kujiongoza.
 
Mimi nampendeaga kwenye mahubiri yake yuko vizuri sana katika kufafanua mambo mbalimbali katika biblia. Kitu kinachonikwaza kwake ni namna anavyochelewesha ibada bila kujali watu wanatoka mbali mara nyingi nikipita tembeon siku za ijuma ana jumanne utawakuta watu wamezagaa kule had saa saba wanatoka ibadani kweli hii sio salama sana,ajitahidi amalize ibada walau saa mbili na nusu watu wawahi kwao.

Mengine jamaa yuko vizuri sana na nazani ndio maana amepata mafanikio Makubwa kwa muda mfupi an kuwazidi hata waliomtangulia
Nakubaliana na wewe kwa time management hayupo vizuri na watu wengi inawakera hii kuna upotezaji muda sana mambo yasiyo muhimu ajifunze kwa wenzake wanaofanya huduma fupi fupi na watu wanafunguliwa
 
Huyu anayejiita Kuhani kuna mambo ya kujiuliza sana toka nilipomfahamu akiwa msaidizi wa Mulilege Mukombo au Mzee wa Yesu aliyekuwa na huduma pale Boko magengeni.

Ilikuwa ukifika kwa mzee wa yesu naye alikuwa na style ya Maombi,uponyaji na maombezi kama Mussa Mwacha , baba yake wa kiroho na ndio aliyempokea Kutoka Congo DRC na kumlea kiimani na hatimaye kumuozesha mwanae wa kike kama mtumishi wa kanisa lake akikuombea kwa mbwembwe nyingi za kufunga macho anakupatia mtumishi mussa uende naye kwako nyumbani au Ofisini akakufanyie maombi ni lazima atatoa vibuyu, hirizi na uchawi aina nyingine.

Style hii ya maombi ya kutoa uchawi wanayo wachungaji wengi wanaotokea Congo DRC hapa Tanzania yupo kijana mmoja mchungaji alikuwa pale Kunduchi baada tuu ya Shule ya Bahari ile njia ya kwenda Rungwe Oceanic naye ana upako aina hii lakini ni wa kisanii. Anakuwa anaficha hirizi halafu akija nyumbani mnaomba mmefumba macho anazitupia kwenye mito makochi hata vyungu vya maua.

Mussa amepitia na kukua toka kwa Mzee wa yesu ambaye haieleweki baadae walitofautiana sana mpaka ndoa yake na mtoto wa.mzee wa yesu ikafika mwisho.

Maoni yangu inawezekana ni mtumishi wa mungu lakini sababu ya kuwajua wacongo watumishi wengi wanaongeza nguvu za mitishamba na fahamu kwamba Congo kuna.msitu mkubwa.sana hivyo kuna.mitishamba ya hatari sana. Nguvu za miujiza, nguvu za kuvuta watu au wateja. Unaweza kumfatilia pia mchungaji tajiri Johanessburg Alpha Lukau ambaye kanisa lake lina Bank clerks ukitaka kutoa sadaka unaenda kwa bank clerks una chanja tuu.

Huduma yake ina angalia zaidi nani anatoa hela kiasi gani. Nadhani ukitaka kumuona sio chini ya laki 3 akisisitiza anajenga kanisa hivyo michango ni lazima. Huwa waumini wapo wanaosaidiwa na kinachowaponya ni imani yao na utayari kwa yesu na si nguvu ya mchungaji.
 
Nilienda kwa mwamposa napia nikajaribu kwa kuwani musaa Ana kibwagizo chake bwana yesu kristo atukuzweee"
Sas nimerud kkkt kimara ingawa sikuhama Wal nilikuwa nikipata muda naenda kwenye maombi Bila sababu zzote nikaona siwaelewi nikarudi zangu korogwe kwa master wangu mastai bingwa San Yule mbuluu nafurahishwa sna na jinsi anavyolipeka kanisa mbele na wahumini kuwa na kititi ingwa anawapenda San wachaga ila Kuna mungu aisee achen kbsa pale hakuna drama

Note sijawadharu hao kina musa na mwamposa wapike Kaz Kaz iendeleee
 
Back
Top Bottom