Kuhamishwa kituo cha kazi na kuachishwa kazi

Wadau naomba kusaidiwa nimekua na mgogoro wa kazi na mwajiri wangu kuniachisha kazi baada ya kunihamisha kituo bila kufuata taratibu.
kwasasa tupo CMA mwajiri katika mgogoro wa kazi anasema kituo changu cha kazi Tanzania.
wakati barua ya tangazo la kazi ni tanga port .
Na hata makubaliano yetu ni kua kabla ya mkataba natakiwa nikubali kusain barua ya tangazo la ajira.baada ya miezi mitano kutumikia probation alinipa mkataba wa kudumu ukuonesha sehem ya kazi tanzania badala ya kituo cha kazi husika.
Sasa baada ya kwenda cma kwenye usuluhisho alisema nimeajiriwa mtwara baada ya kuona kesi imeenda mbele kwa maamuzi anasema nimekuajiri tanzania hivyo anamamlaka yakunipeleka popote huku mkataba ukiwa hausemi hivyo.
Msaada kabla ya kwenda mahakamani .
je kama mwajiri amekuajiri anamamlaka ya kukuhamisha bila barua na baada ya mda kukuachisha kazi kazi kisa mkataba umesema tz

Keneth,

Natumaini sijachelewa sana kukushauri kuhusiana na shauri lako ambalo kwa sasa lipo CMA. Sehemu ambapo nadhani wengi humu ndani umewachanganya nadhani ni sehemu ya kusema kwamba ulitakiwa kukubai kusaini barua ya tangazo ka ajira; sidhani kama hiyo barua inatambulika katika sheria zetu za kazi na naamini ni utaratibu ambao muajiri wako kajiwekea mwenyewe.

Mwajiri wako anaposemaa ya kwamba umeajiriwa Tanzania na ana mamlaka ya kukupeleka kokote anakuwa amekosea na yupo sahihi pia. Kosa ni kwamba hawezi kusema amekuajiri na kituo chako cha kazi ni Tanzania; Tanzania ni nchi yenye mikoa na wilaya na nchi haiwezi kuwa kituo cha kazi. Katika Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya mwaka 2004 Sehemu ya 15 imeainisha vitu ambavyo mwajiri anatakiwa mjulisha mwajiri au kuviweka katika mkataba wa ajira na moja kati ya vitu hivyo ni Kituo cha Kazi na majukumu yake. Sehemu ya kazi itakuwa ndani ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na sio Tanzania yote. Ninaposema Mwajiri anakuwa sahihi ni kutokana na uliposema:

...anasema nimekuajiri Tanzania hivyo ana mamlaka ya kunipeleka popote huku mkataba ukiwa hausemi hivyo.

Ni kweli kwamba anaweza kukupeleka sehemu yoyote ambapo ana shughuli zake lakini itakuwa ni jukumu lake kugharamia uhamisho wako mpaka kituo chako kipya cha kazi na pia atakuwa na jukumu la kukusafirisha wewe ni mizigo yako kwenda kituo kipya cha kazi; ikitokea kwamba mkataba wa ajira utasitishwa, mwajiri atakuwa na jukumu la kukusafirisha wewe na mizigo yako yote kukurudisha kituo cha kazi ambapo uliajiriwa ulipojiunga na kampuni yake (ELRA 2004 Section 43(1)).

Suala la kukuhamisha kituo cha kazi mwajiri anatakiwa kukaa na muajiriwa na kuainisha sababu za kumuamisha kutoka kituo cha kazi; katika hilo pia mwajiri anatakiwa kutoa muda kwa mwajiriwa utakaomtosha kwa ajili ya maandalizi ya uhamisho. Pia mwajiri atatakiwa kutoa posho ya kujikimu kwa majiriwa katika kipindi cha uhamisho. (ELRA 2004 Section 43(1)).

Katika suala la kumwachisha mwajiriwa kazi, mwajiri anatakiwa fuata sheria mama ya Ajira na Mahusiano Kazini na hatua zote zinazotakiwa kufuata kumwachisha mwajiriwa kazi. Kilichoandikwa kwenye mkataba tu hakitoshelezi kufikia maamuzi hayo; ,mwajiri anatakiwa ainishe hatua alizochukua katika kujaribu kunusuru ajira ya mwajiriwa na pia athibitishe kwamba kusitisha mkataba wa ajira ndio ilikuwa suluhu pekee ya mahusiano kati yake na mwajiriwa. Hatua hizi zimeainishwa vizuri kwenye Code of Good Practise, 2007.

USHAURI:

Endelea na shauri lenu CMA usikate tamaa na utapata haki yako stahili. Mwajiri atafanya kila awezalo kupoteza muda lakini usikate tamaa.
 
Mwajiri ana haki ya kumhamisha mwajiriwa wake kituo chochote cha kazi mahali ambapo shughuli za mwajiri huyo zipo, acho paswa ni kuzingatia sheria na kanuni zinavyoelekeza. Kitendo chakutoripoti kituo chako kipya cha kazi bila sababu itachukuliwa kama utovu wa kinidhamu na mwajiri anaweza kuchukua hatua za kukuadhibu kwa kufuata utaratibu uliowekwa kwamujibu wa sheria na kanuni.
 
Back
Top Bottom