Kuhamishwa kituo cha kazi na kuachishwa kazi

Keneth

Senior Member
Sep 29, 2011
195
47
Wadau naomba kusaidiwa nimekua na mgogoro wa kazi na mwajiri wangu kuniachisha kazi baada ya kunihamisha kituo bila kufuata taratibu.
kwasasa tupo CMA mwajiri katika mgogoro wa kazi anasema kituo changu cha kazi Tanzania.
wakati barua ya tangazo la kazi ni tanga port .
Na hata makubaliano yetu ni kua kabla ya mkataba natakiwa nikubali kusain barua ya tangazo la ajira.baada ya miezi mitano kutumikia probation alinipa mkataba wa kudumu ukuonesha sehem ya kazi tanzania badala ya kituo cha kazi husika.
Sasa baada ya kwenda cma kwenye usuluhisho alisema nimeajiriwa mtwara baada ya kuona kesi imeenda mbele kwa maamuzi anasema nimekuajiri tanzania hivyo anamamlaka yakunipeleka popote huku mkataba ukiwa hausemi hivyo.
Msaada kabla ya kwenda mahakamani .
je kama mwajiri amekuajiri anamamlaka ya kukuhamisha bila barua na baada ya mda kukuachisha kazi kazi kisa mkataba umesema tz
 
Wadao naomba kusaidiwa nimekua na mgogoro wa kazi na mwajiri wangu .kwasasa tupo CMA mwajiri anasema kituo chankazi Tanzania wakati barua ya tangazo la kazi ni mtwara port .na hivyo ili kukubari ajirabilikua lazima niisaini kukubaliana kabla ya mkataba.
Sasa baada ya kwenda cma alisema nimeajiriwa mtwara baada ya kuona kesi imeenda mbele anasema nimekuajiri tanzania
Msaada kabla ya kwenda mahakamani jumatatu
Pia je kama mwajiri amekuajiri anamamlaka ya kukuhamisha na kukufukuza kazi kisa mkataba umesema tz
Jaribu kupitia maandiko yako hayo kama wewe mwenyewe utayaelewa.
 
kituo cha kazi lazima kitambulike...

mf. polisi ameajiriwa na JMT, lakini lazma awe amepangiwa kituo chake cha kazi mahali fulani.
 
kituo cha kazi lazima kitambulike...

mf. polisi ameajiriwa na JMT, lakini lazma awe amepangiwa kituo chake cha kazi mahali fulani.
Asante nipe mwanga haijarishi nimekosea lakini content imeeleweka kinachotakiwa namna ya kudefend hiyo hoja
 
Kama kuna kosa la kimantiki ina maana kuna kosa kubwa sana ambalo mantiki ya andiko haitaeleweka.
Asante mkuu, inashangaza mtu ana adimit kosa tena la kimantiki lakini anashindwa kutambua kuwa bilashaka mantiki ya andiko lote haitaeleweka kabisa lisiposahihishwa kosa hilo.
 
Hueleweki kabisa mkuu. Hebu tulia na ulete ufafanuzi ulionyooka. Kwanza inaonekana bado upo kwenye probation period, katika kipindi hiki hutakiwi kuwa jeuri maana mwajiri anaweza kukufukuza kazi bila fidia kama hajaridhishwa nawe kiutendaji au kwasababu yoyote ile. Mkataba wako nadhani una masharti, mojawapo likiwa kutumikia kituo chochote cha kazi ambacho mwajiri wako ataona inafaa.

Swali,
Unataka kumshtaki bosi wako jambo gani, uzi wako umeandika kireno haueleweki!
 
Back
Top Bottom