Kugoma kula ni suicide mission, kwanini asishitakiwe?

Kugoma kula ni suicide mission, kwanini asishitakiwe?

Je wakimfungulia shitaka hilo mnaamini ndio ataogopa ale?? Jaribu kusema mengine hayo kwa anayejiona kuwa mwanaharakati huwa hayawasumbui. Unaweza mpachika kesi 100 wala haogopi. Kumbuka kuwa hawa ni watu wanaotafuta kuandikwa kwenye historia. Iwe ya wapuuzi waliowahi kuishi chini ya jua au wapambanaji waliowahi kuishi chini ya jua. Kwao kuandikwa ndio kiu yao.
Mwanaharakati wa kitu gani?
 
Hivi haya maneno "To be under protest" na "intention to" yanafanana maana hii kesi atashinda asubuhi ni Mawazo yangu tu lakini
Nashukuru kuwa umeleta Hiyo tafsiri kwani itasaidia hao polisi kujua kuwa hakuna kesi hapo. Huyu angekuwa nyumbani kwake halafu akagoma kula kwa nia ya kujiua (na kudhibitisha nia hiyo kwa mdomo wake) hapo wangeweza kumshitaki. This guy is protesting against police brutality and violation of his rights. So, police are the one to be blamed. He wants his rights- mpeni atakula it's simple like that !
 
Wanakamatwa hovyo hawa ni magaidi?
Mbona wanaosema matamko ya kupiga watu kama makonda vile hawawakamati?
 
Wanawapotezea muda wao TU...
Nashukuru kuwa umeleta Hiyo tafsiri kwani itasaidia hao polisi kujua kuwa hakuna kesi hapo. Huyu angekuwa nyumbani kwake halafu akagoma kula kwa nia ya kujiua (na kudhibitisha nia hiyo kwa mdomo wake) hapo wangeweza kumshitaki. This guy is protesting against police brutality and violation of his rights. So, police are the one to be blamed. He wants his rights- mpeni atakula it's simple like that !
 
Kwani ni lazima kula? Wangekuwa na nia njema wangesikiliza shauri wa Meya wa Jiji la Arusha Kalisti Lazaro jana kumpatia dhamana na jumatatu angeenda mahakamani .Watu wengi hawajui udhalilishaji ambayo amefanyiwa mbunge Godbless Lema ndo maana wanaandika ujinga humu JF.
 
Aendelee kugomea kula, naomba Lema asibembelezwe, tuone kama hatokula
 
Kwani ni lazima kula? Wangekuwa na nia njema wangesikiliza shauri wa Meya wa Jiji la Arusha Kalisti Lazaro jana kumpatia dhamana na jumatatu angeenda mahakamani .Watu wengi hawajui udhalilishaji ambayo amefanyiwa mbunge Godbless Lema ndo maana wanaandika ujinga humu JF.
Nenda zako... Dhamana asipewe tuone kama atokula, tuna hamu na uchaguzi mdogo
 
Jeshi la polisi mkoani Arusha limesema kama mbunge wa Arusha mjini amegomea kula bila sababu ya msingi watamfungulia kesi ya kutaka kujiua.
Kwa mujibu wa meya wa Arusha mjini leo ni siku ya tatu toka mbunge huyo agome kula akiwa gerezani kupinga kukamatwa kwako.
Kuna tofauti kati ya kugoma kula na kujaribu kujiua.hizo ni boyoyo tu, sheria ndiyo inayofanya uchambuzi wanamtisha asiwasumbue kutunza!
 
Kwani mpaka wakasema " ikithibitika"
Kuna muda walimwachilia akaenda mtaani kidogo kwamba huenda alikula huko, na kwa nini watoe Maneno yasiyo na chanzo eti amegoma kula halafu waseme ikithibitika, waliyaota ndotoni hayo ya kutokula?
 
Jeshi letu sijui ni la namna gani. Mandela alipokuwa mfungwa, aliweza kujisomea na hata kupata shahada yake ya pili ya sheria akiwa gerezani. Najaribu kufikiria, hivi kuna uwezekano wa mfungwa wa Tanzania kupata japo certificate tu akiwa gerezani chini ya hawa askari wetu?

Tunapenda sana kujionesha kuwa ni nchi ya kidemokrasia na inayowajali watu wake lakini kiuhalisia tupo mbali sana kutoka uliko mwanga.
 
Natambua hii nchi haina Hati Miliki, kwa hiyo IPO siku Tu!
 
Kama ni haki yake ya kikatiba kwa nini asipewe dhamana? kwani police hawajui katiba ya nchi hii? hata communist countries wana raia wao hupewa dhamana. Sijui nchi yetu iko upande upi, maana police katika nchi ambazo tunajidanganya kufuata eti sisi ni wa communist hawapigi raia wao,mimi nimewahi kamatwa mara nyingi tu katika nchi zile ,tena nikiwa ndani ya gari la police nimekunywa nilikuwa natukana sana police katika nchi ile hakunigusa, na kesho yake walimu wa chuo nilichokuwa nasoma wakaja asubuhi wakanitoa, police very friendly tena wanacheka na kunikumbusha jinsi nilivyokuwa naongea na kutukana usiku ule, Tanzania kitu ambacho tunamisss kama waafrika wengine ni kutokuwa na uelewa, upendo na kutofuata sheria, tunapenda sana kukomoana, mtu binafsi mmoja au wawili ndo wanasheria ,ndo wakisema basi hakuna cha kufuta utaratibu wa sheria hapa, tunapenda sana mambo ya mheshimiwa, haya mambo yalikuwa zamani, dunia imebadilika. Hata Kenya kwa sasa inatuzidi, maana sheria ya Kenya inasema mtu ukimkamata leo, kama hakuna shida mmalizane nae leo leo, ikishindikana baada ya masaa 24 apandishwe mahakamani, kule akifika wataangalia je anastahili kupewa dhamana? kama yes hapo hapo anapewa dhamana, na kesi itapangia tarehe kuanza kusikilizwa. Unakaaa na mtu kituo cha police siku tatu hizo zote za nini? hiyo ni gharama kubwa, upotezaji muda, unampotezea mtu muda pia unaliingizia taifa hasara ya kumlaza na kumuangalia muda wote huo, bure kabisa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom