Kugoma kula ni suicide mission, kwanini asishitakiwe?

Kugoma kula ni suicide mission, kwanini asishitakiwe?

Jeshi la polisi mkoani Arusha limesema kama mbunge wa Arusha mjini amegomea kula bila sababu ya msingi watamfungulia kesi ya kutaka kujiua.
Kwa mujibu wa meya wa Arusha mjini leo ni siku ya tatu toka mbunge huyo agome kula akiwa gerezani kupinga kukamatwa kwako.
 
Wana Jf wasalaam.

Baada ya Bwana Lema kukamatwa juzi na kuswekwa rumande kwa uchochezi amekuwa akigoma kula kwa kile anacho dai hakuyendewa wakati ana kamatwa.

Bwana Lema amesema atagoma kula hadi atakapo achiliwa huru jambo ambalo si hoja..

Kamanda wapolisi mkoani Arusha amesema kama ikithibitika Bwana Lema amegoma kula kwa sababu zisizo za msingi basi atafunguliwa shitaka la kujaribu kujiua ambalo ni kinyume na sheria...

Njia pekee ya Lema kukwepa mashitaka hayo ya kutaka kujiua ni kula..

Ni vyema chadema wakamshauri Lema kula chakula kwani kutokula kwake hakutofanya kuepuka mashitaka.. Ni wazi viongozi wa chadema wanaunga mkono kitendo cha Lema kugoma kula.

Karibuni wanajamvi..
Hizi kauli za wakubwa wetu bwana huwasiwaelewielewi ukizifanyia analyisisi una ambiwa mchochezi,kama alizalilishwa wakati wa kukamatwa mbona hsemi wahusika watafanywa nini.?
 
Je wakimfungulia shitaka hilo mnaamini ndio ataogopa ale?? Jaribu kusema mengine hayo kwa anayejiona kuwa mwanaharakati huwa hayawasumbui. Unaweza mpachika kesi 100 wala haogopi. Kumbuka kuwa hawa ni watu wanaotafuta kuandikwa kwenye historia. Iwe ya wapuuzi waliowahi kuishi chini ya jua au wapambanaji waliowahi kuishi chini ya jua. Kwao kuandikwa ndio kiu yao.
 
Sheria ya kip.umbavu kabisa hiyo.

Utamshitakije mtu aliyetaka kujiua mwenyewe?
 
Lema amefanya uchochezi upi?

Hebu thibitisha hapa jinsi alivyotoa kauli ya uchochezi au kuandika chochote cha uchochezi.
 
Hatofunguliwa Mashitaka ya kujaribu kujiua kwa kuwa hagomi kula isipokuwa ni maigizo tu ya kutafuta Kick ndio Maana RPC kasema ikithibitika kwa kuwa anajua haitothibitika!
 
Wana Jf wasalaam.

Baada ya Bwana Lema kukamatwa juzi na kuswekwa rumande kwa uchochezi amekuwa akigoma kula kwa kile anacho dai hakuyendewa wakati ana kamatwa.

Bwana Lema amesema atagoma kula hadi atakapo achiliwa huru jambo ambalo si hoja..

Kamanda wapolisi mkoani Arusha amesema kama ikithibitika Bwana Lema amegoma kula kwa sababu zisizo za msingi basi atafunguliwa shitaka la kujaribu kujiua ambalo ni kinyume na sheria...

Njia pekee ya Lema kukwepa mashitaka hayo ya kutaka kujiua ni kula..

Ni vyema chadema wakamshauri Lema kula chakula kwani kutokula kwake hakutofanya kuepuka mashitaka.. Ni wazi viongozi wa chadema wanaunga mkono kitendo cha Lema kugoma kula.

Karibuni wanajamvi..
Hivi haya maneno "To be under protest" na "intention to" yanafanana maana hii kesi atashinda asubuhi ni Mawazo yangu tu lakini
 
Lema alishasema yupo tayari kutetea anachokiamini hata kama ni kwa damu yake ,Sasa nimeamini maneno yake
 
Mwiguluu angalia chuki wanazozitengeneza askari kwa wananchi hivi wapiga kura wa lema watakuwa na mapenzi na askari, angalia hili bro. Waambie watende haki ni jambo jema kwa yeyote kumheshimu mwenzake
 
Mtu ikithibitika kuwa anataka kujiua........
Mtu ikithibitika kuwa anataka kuishi (wanaonyongwa) sheria inawataka wafanywe nini?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom