Fahamu jinsi ya kumiliki mgodi wa madini nchini Tanzania

george aloyce

JF-Expert Member
Aug 22, 2017
1,177
1,827
JINSI YA KUMILIKI MGODI WAKO KISHERIA NCHINI TANZANIA.

KISHERIA:madini yote ni mali (nyara) ya serikali KUU na serikali hiyo ndio yenye mamlaka ya kumpatia mtu leseni ya uchimbaji pale inapotokea mtu huyo kaomba leseni yakuchimba madini hayo yaliyopo katika eneo flani. Serikali hii humpatia mtu flani leseni ili aweze mchimbaji madini hayo ili yenyewe ikusanye KODI kutokana na madini yanayo chimbwa na mtu huyo.

LESENI HII YA UCHIMBAJI MDOGO (PRIMARY MINING LICENCE-PML): hutolewa kwa kipindi cha miaka saba (7), na miaka 7 inapoisha mwenye leseni anaweza kutuma tena maombi ili aweze kupiwa tena leseni UPYA. ila sasa kama mtu huyu alishindwa KUENDELEZA eneo lake kwa miaka 7 ya mwanzo (yaani hakufanya shughuri za uchimbaji) basi serikali haita mruhusu mtu huyu tena kumiliki eneo hilo na badala yake atapewa mtu mwingine akatie leseni eneo hilo ili aweze KULIENDELEZA.

SERIKALI KUPITIA WAZIRI WAKE WA MADINI ANAYO MAMLAKA YAKUIFUTA LESENI YEYOTE YA UCHIMBAJI NCHINI TANZANIA KWA MASLAHI MAPANA YA NCHI.

SERIKALI HAITOI LESENI ZA UCHIMBAJI WA MADINI KWA MTU YEYOTE KATIKA MAENEO YAFUATAYO HATA KAMA YAKIWA NA MADINI.

1. maeneo ya HIFADHI

2.maeneo ya mbuga za wanyama

3.maeneo ya utawala.

4.maeneo ya vyazo vya maji.

maeneo tajwa hapo juu hatakama ukikuta yana madini kiasi gani basi ukiomba leseni ya kumiliki maeneo hayo ili uchimbe hautakubaliwa.

ZINGATIA HILI: kama nilivyokwisha tangulia kusema hapo juu kuwa MADINI YOTE NI MALI YA SERIKALI NA SIO MALI YA MTU BINAFSI WALA MWENYESHAMBA LINALOTOKA HAYO MADINI, maana kuna tabia siku hizi mtu shamba lake linatoka madini ila yeye hana mpango nayo kabisa ila ikitokea mtu katoka zake mbali huko akawahi kukatia leseni yale madini ya kwenye shamba lake basi anahisi kazulumiwa hapana sheria ndivyo ilivyo kwani wewe lako ni shamba yale madini yalikuwa sio yako haimani madini kutoka shambani kwako basi madini yale ni yako sheria HAISEMI HIVYO. ukitaka mwenye shamba eneo lako linatoka madini basi wewe wahi wizarani kaombe leseni ya eneo lako hilo hapo utakuwa umeshinda ila ukichelewa wajanja akawahi IMEKULA KWAKO KWANI leseni anaewahi kuomba leseni ndio atakaepewa leseni na ww ukija nyuma yake umechelewa.

HATUA ZA KUKATIA ENEO LAKO LESENI:

1. nikupata eneo ambalo unauhakika kuwa madini yapo na umejirizisha kuwa eneo hilo halina leseni ya mtu mwingine ulishawahi kata na yupo mbioni kufanya kazi za uchimbaji. kwani eneo kama lina leseni wewe hautakubaliwa kukatia eneo hilo hilo leseni labda ukate pembeni mwa iyo leseni iliyopo.

2.HATUA INAYOFATA, ni kuchukua mpimaji/SURVEYOR mwenye GPS na kumpeleka katika eneo hilo ili akakuchukulie coordinate/points za eneo lako ( kama unayo GPS na unajuwa kuitumia unaweza chukua coordinate zako mwenyewe ili kupunguza garama za kumlipa pesa SURVEYOR).

3.HATUA INAYOFATA, ni kupeleka coordinate zako hizi za eneo katika ofisi za madini zilizopo katika mkoa wako.

4.HATUA INAYOFATA, afisa madini atachukua coordinate zako na kuziingiza katika system ili kuangalia kama eneo hilo tayali lina leseni ya mtu au halina, kama kuna leseni ya mtu kashakatia pale ataona na kama bado halina leseni LIPO WAZI ATAONA, kama lina leseni ya mtu imekula kwako rudi nyumbani katulie tuu ila kama lipo wazi atakwambia uendelee na hatua zinazofata.

5.HATUA INAYOFATA, utafanya maombi la leseni ya eneo hilo na garama yake utalipia TSH 50,000/=, na PIA UTALIPIA GARAMA NYINGINE YA tsh 50,000/= hii ni kwa ajili ya maandalizi ya leseni yako ( wanaiita ada ya maandalizi ya leseni) na baada yahapo utarudi nyumbani kusubiria leseni itoke na haitazidi mwezi 1 leseni yako itakuwa imetoka.

6.HATUA INAYOFATA, leseni yako ikitoka utapewa taarifa kuwa leseni yako imetoka uje kuilipia, HAPA KWENYE KULIPIA inategemea eneo lako ulilokata leseni lina ukubwa wa HEKTA NGAPI kwani kila hekta moja utalipia TSH 90,000/= kila mwaka.

NOTE: HEKTA 1 NI SAWA NA HEKARI 2.5

MFANO: eneo lako ulilolikatia leseni lina ukubwa wa HEKTA 4 ambazo ni sawa na HEKARI (4X2.5= 10), HAPA LESENI HII UTALIPIA KILA MWAKA 90,000/= X4 = 360,000/= NDANI YA MIAKA 7 YAKO YA LESENI ULIYOPEWA.

SASA kwa leseni yako hii yenye eneo la hekta 4 ukipigiwa simu leseni yako imetoka wewe weka pesa ya serikali tsh 360,000/= kwenye mfuko wa shati njoo nayo wizarani lipia unapewa LESENI YAKO. kumbuka hiii tsh 360,000/= unayolipia ni YA MWAKA HUU WA KWANZA, MWAKANI UNALIPIA KAMA HII TENA, MWAKA UNAOFUATA UNALIPIA TENA MPAKA MIAKA 7 YAKO YA LESENI IISHE, ukisikia leseni ya mtu flani inadaiwa ujue ndio hizi hapa pesa za kila mwaka hajalipia.

HAPA UMEPEWA LESENI TUU, ILA BADO SERIKALI ITAKWAMBIA, TUMEKUPA LESENI ILA HATUKUTUHUSU KUANZA UCHIMBAJI WAKO MPAKA UTULETEE OFISINI KWETU VITU VIFUATAVYO:

1. barua ya maandishi kutoka kwa mmiliki wa shamba ulilolikatia leseni ( mwenyeshamba akuandikie ww barua kuwa nimemruhusu mtu flani akatie leseni shamba langu, yaani kifupi barua ya mariziano kati ya ww uliekatia leseni na mwenye shamba lake linalotoa hayo madini): HAPA mtajuana kama utamlipa fidia au vipi shauri zako mradi akuandikie barua upeleke wizarani.

2.mukhtasari wa kijiji husika unapotaka kuanzisha huo mradi wako. KIJIJI KILIZIE

3.mpango wa utunzaji wa mazingira. hapa utamuita mtalamu aliesomea mambo ya mazingira akuandikie ripoti.

4.kiapo cha uadilifu, hii ni form maalimu unapewa pale wizarani unaenda kuijaza na kuhongewa mhuri na mwanasheria, hiki ni kiapo kwamba hutaenda kinyume na sheria za madini katika UCHIMAJI wako kama KUTOROSHA madini n.k

5. mpango wa uwajibikaji wa mwenye leseni kwa jamiii, yaani jamiii inayozunguuka mradi wako itanufaikaVIPI na ww, kama utawajengea shule au zahanati n.k haya utayaahidi kwa maandishi.

6.mpango wa manunuzi katika kazi zako za uchimbaji, hapa wanataka kama eneo la mradi wako kuna watu wa wanauza vyakula inatakiwa ununue mahitaji yako eneo hilo sio unafata vitu mbali wakati pale vipo.

UKISHAFATILIA VYOTE HIVI UKAWA NAVYO SASA NDIO KWA PAMOJA UNAVIKUSHANYA UNAVIPEKEKA OFISI YA MADINI NA HAPA SASA NDIO MGODI WAKO UPO HURU KUANZA KAZI, NA SIO TUU UPO HURU BALI WAO NDIO WATAKUPA BARUA KUWA SASA UMEKIZI VIGEZO ANZA KAZI..

CHAKUZINGATIA NA CHA MUHIMU, sio tuu ukiona visampo vya madini flani unakimbilia wizarani kukatia leseni kwa vigezo kuwa NAWAHI ILI NISIJE WAHIWA hapana, kwanza hatua ya kwanza kabla hujaenda kufanya mpango wa leseni hakikisha madini unayokatia leseni HAPO KATIKA ENEO HILO YAPO KWA KIWANGO/WINGI AMBACHO KAMA UTAFANYA UCJIMBAJI UTAPATA FAIDA ila ukiona ni kinyume chake hushauriwi kukatia leseni,HAPA NDIPO LINAKUJA SWALA LA KULETU MTALAMU MWENYE UELEWA WA MADINI ILI ATIZAME ENEO LAKO NA AKUSHAURI, HATAKA ASIWE MTALAMU SANA WALAU BASI AWE NA UFAHAMU JAPO KIDOGO WA MADINI HAYO ILI AZUNGUUKIE ENEO HILO NA AKUSHAURI JAPO MTU HUYU NAE UWE NA UHAKIKA NAE MAANA ASIJE KUWA MTU WA TAMAAA AKAKUZUNGUUKA AKASEMA ENEO LAKO HALIFAI KUMBE ANAENDA KUKATIA YEYE LESENI KWA JINA LAKE kwenye madini watu wa hivi wapo wengi sana kuweni nao makini.

USHAURI WANGU KWA JAMII: kama eneo lako au shamba umeona lina madini na umeona yanatoka kwa wingi WAHI KATIA LESENI KABLA HUJAWAHIWA, ILA kumbuka kukatia leseni ni mchakato mrefu hivyo unahitaji pesa za kutosha mizunguuko yake kwani leseni mpaka ikamilike mara nyingi garama yake andaa pesa kati ya MILIONI 1 MPAKA MILIONI 3, Japo itategemea na ukubwa wa eneo ila hela hii iwepo, HIVYO HII NI GARAMA WENGI HAWEZI NA UKIONA HUWEZI TAFUTA MTU MSHIRIKIANE WOTE KWA PAMOJA KUKATIA LESENI MGODI NA WOTE MUWE SHEA YAANI MAJINA YENU WOTE YAMEMO KWENYE LESENI KWANI SIKU ZOTE NI VIGUMU SANA KUMILIKI MGODI PEKEAKO...

KWA USHAURI WA KITALAMU JUU YA MAMBO YAHUSUYO MADINI HUSUSANI BIASHARA ZA MADINI NA UTAFITI WA ENEO LAKO LENYE MADINI UNAWEZA KUNITAFUTA

BY GEORGE
1707239681539.jpg
 
Kabla ya kufanya vipimo kubaini kama kuna madini kwenye eneo unalohisi kuwa kuna madini, utapaswa kupata kibali cha Serikali?
 
Back
Top Bottom