Kufuru katika msiba wa bilionea Sambeke Arusha

Kufuru katika msiba wa bilionea Sambeke Arusha

Sasa kama hela ipo watu wasile??
Namna ya uandishi huu wa habari inaonesha namna mwandishi wa habari alivyo na fikra za kimaskini.
Mtu kafariki lakini pesa haijafariki...
Teh teh teh!umenichekesha sana mkuu!
 
Ni kwa sababu hukumjua au hukuwahi kuishi karibu na mtu huyo ndio maana unapata shaka.
Kwa tuliomjua kwa karibu tunajua jinsi mwanaume yule alivyokuwa na uwezo wa kutisha wa senti, ikiwa ni pamoja na vision za hali ya juu za maendeleo.
Yeye alikuwa akiongelea kuhusu kuanzisha Flying School, kitu ambacho hata serikali haijawahi kuwaza hilo.

Mkuu PakaJimmy huyu jamaa alikuwa anajishugulisha na biashara gani?

Flying school inafaida gani kwa jamii masikini ya kitanzania?
 
Last edited by a moderator:
All in all,mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi!
 
Kumbukumbu yangu huyu jamaa alikuwa tishio ila kwa sababu ya U-bilionea basi anaonekana wa maana.Mwenyezi mungu ailaze roho ya mbabe huyo mahali pema peponi.AMEN
 
Kumbukumbu yangu huyu jamaa alikuwa tishio ila kwa sababu ya U-bilionea basi anaonekana wa maana.Mwenyezi mungu ailaze roho ya mbabe huyo mahali pema peponi.AMEN
Alikuwa tishio kivipi?kisiasa,kiusalama au kimazingira?
 
Mwananchi sasa hivi limeanza kuwa la Udaku. Hivi hizi ni habari za kuandikwa na Mwananchi.
 
Kama kweli ni kufuru, basi waanzishe kwa kugawa japo burger msibani.


Nataka pia kujua, nani atachinja?
 
Tena wamesema bilionea wa moshi na sio billionea wa Tanzania, so nadhani huko Moshi alikuwa mtu fulani kwani binafsi simjui......yote ya yote namtakia kila la kheri na familia yake ipokee pole nyingi Mungu atawatia nguvu, huko alipo kwa sasa natumaini amepata mapokezi yake kulingana na matendo yake hapa duniani.
 



Babu Sambeke ni mmoja wa wafanyabiashara wa kwanza katika kanda ya Kaskazini kumiliki ndege, na hadi anafariki alikuwa akitumia ndege mbili.Jina lake lilianza kuwa maarufu 1985 akionekana kama mtoto wa mjini `mission town’ na baadaye alijiimarisha kibiashara na kuwa na utajiri mkubwa.Kufuru katika msiba wa bilionea Sambeke Arusha - Kitaifa - mwananchi.co.tz





Sepetu ni sepetu sio kijiko ikubwa. mtoto wa mjini misheni town inamaanisha nini... tapeli, mwizi??
 
Kwani watu huwa wanaitwa bilionaires kwasababu gani?

Kutokana na mali anazozimiliki huyu bilionea gani anamiliki ndege ya kizamani kama hiyo hakuna bilionea ambaye anakubali kupanda ndege kama hiyo ambayo si salama. Au nikuwekee ndege za mabilionea.
 
Back
Top Bottom