Kufuru katika msiba wa bilionea Sambeke Arusha

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,073
Reaction score
34,844
ajali_sembeke.jpg

Ndege aina ya Cessna 5H-QTT ikiwa imeanguka eneo la Kisongo, karibu na Uwanja wa Ndege Arusha juzi jioni, baada ya kugonga mti wakati ikijiandaa kutua na kusababisha kifo cha mmiliki wake na aliyekuwa rubani, Bob Sambeke(katika picha ndogo juu). Picha na Filbert Rweyemamu.

KWA UFUPI
Meneja wa Uwanja wa Ndege Arusha, Ester Dede alisema uchunguzi wa ajali hiyo unaendelea kufanywa na wataalamu wawili wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga kutoka Dar es Salaam.

Arusha. Wakati mazishi ya mfanyabiashara bilionea wa Moshi, Ernest Babu ‘Sambeke' yakiwa yamepangwa kufanyika keshokutwa, msiba wake umekuwa wa kitajiri kutokana vyakula na vinywaji kumwagwa kwa wingi nyumbani kwa marehemu.

Msiba wa mfanyabiashara huyo uko nyumbani kwake, Njiro – Themi nje kidogo wa Mji wa Arusha ambako habari zinasema mamia ya watu wamekuwa wakifurika kuhani.

Matajiri wa Mikoa ya Kilimanjaro na Arusha wakiwa na magari ya kifahari wamefurika katika msiba huo na habari zaidi zinasema mamilioni ya shilingi yamechangwa kwa ajili ya kufanikisha mazishi ya bilionea huyo aliyefariki dunia, Jumamosi iliyopita kwenye ajali ya ndege.

Ajali hiyo ilitokana na ndege aina ya MT 7- yenye namba 5H-QTT ambayo alikuwa akiiendesha mwenyewe kuanguka kwenye Uwanja wa Ndege wa Arusha, baada ya bawa lake kugonga mti katika eneo la Magereza linalopakana na uwanja huo.

Alifariki dunia wakati askari magereza waliompa msaada walipokuwa wakimkimbiza hosipitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu kutokana na majeraha makubwa aliyoyapata kichwani.

Magari makubwa yaliyosheheni vyakula na vinywaji yamekuwa yakiingia na kutoka katika makazi ya Sambeke ambako waombelezaji wote wameandaliwa maeneo maalumu ya kuketi yaliyofunikwa na mahema ambako vinywaji na vyakula vinatolewa.

Msemaji wa familia, Dk Richard Masika alisema marehemu atazikwa katika eneo la Karanga mjini Moshi ilipo nyumba yake na kwamba misa itaanza saa 7.00 mchana katika Kanisa Katoliki mjini Moshi na mazishi kufanyika saa 10.00 jioni.

Habari zaidi zilizopatikana zinaeleza kuwa marehemu atazikwa akiwa amevalia sare za marubani kutokana na kupenda kwake kurusha ndege.

Habari zaidi zinasema familia ya marehemu imekuwa ikifuatilia mali alizokuwa nazo marehemu zikiwemo fedha wakati akipatwa na mauti.
Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari alisema, Babu Sambeke alikuwa ni rafiki wa watu wengi, wakiwapo wanasiasa wa vyama vyote.

"Binafsi baada ya kupata taarifa za kufariki kwa Babu Sambeke, niliwapigia baadhi ya wabunge na mawaziri, wote walishtushwa sana na msiba huu," alisema Nassari.

Babu Sambeke ni mmoja wa wafanyabiashara wa kwanza katika kanda ya Kaskazini kumiliki ndege, na hadi anafariki alikuwa akitumia ndege mbili.Jina lake lilianza kuwa maarufu 1985 akionekana kama mtoto wa mjini `mission town' na baadaye alijiimarisha kibiashara na kuwa na utajiri mkubwa.Kufuru katika msiba wa bilionea Sambeke Arusha - Kitaifa - mwananchi.co.tz

alaf hii address ya u-bilionea, napata shida sana kuielewa

Ndio kaka lazima upate shida kuelewa.

Huo u-bilionea unaoongelewa hapo ni mahesabu ya shilingi za kitanzania, sio British pound au US dollar.

Ukiwa bilionea Tanzania unaweza kununua kadege kama hiko cha bilionea Sambeke. Umeona picha ya "ndege" ya bilionea Sembeke? Ni haki yake kuitwa bilionea kama alimiliki shilingi bilioni na ushee za kitanzania.

Ukiwa milionea wa US dollar unaweza kununua Private jet kama hii.

Last edited by a moderator:

All in all marehemu alikua bilionea.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
alaf hii address ya u-bilionea, napata shida sana kuielewa
Ni kwa sababu hukumjua au hukuwahi kuishi karibu na mtu huyo ndio maana unapata shaka.
Kwa tuliomjua kwa karibu tunajua jinsi mwanaume yule alivyokuwa na uwezo wa kutisha wa senti, ikiwa ni pamoja na vision za hali ya juu za maendeleo.
Yeye alikuwa akiongelea kuhusu kuanzisha Flying School, kitu ambacho hata serikali haijawahi kuwaza hilo.
 
Sasa kama hela ipo watu wasile??
Namna ya uandishi huu wa habari inaonesha namna mwandishi wa habari alivyo na fikra za kimaskini.
Mtu kafariki lakini pesa haijafariki...
 
ajali_sembeke.jpg

Ndege aina ya Cessna 5H-QTT ikiwa imeanguka eneo la Kisongo, karibu na Uwanja wa Ndege Arusha juzi jioni, baada ya kugonga mti wakati ikijiandaa kutua na kusababisha kifo cha mmiliki wake na aliyekuwa rubani, Bob Sambeke(katika picha ndogo juu). Picha na Filbert Rweyemamu.

KWA UFUPI
Meneja wa Uwanja wa Ndege Arusha, Ester Dede alisema uchunguzi wa ajali hiyo unaendelea kufanywa na wataalamu wawili wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga kutoka Dar es Salaam.

Arusha. Wakati mazishi ya mfanyabiashara bilionea wa Moshi, Ernest Babu ‘Sambeke' yakiwa yamepangwa kufanyika keshokutwa, msiba wake umekuwa wa kitajiri kutokana vyakula na vinywaji kumwagwa kwa wingi nyumbani kwa marehemu.

Msiba wa mfanyabiashara huyo uko nyumbani kwake, Njiro – Themi nje kidogo wa Mji wa Arusha ambako habari zinasema mamia ya watu wamekuwa wakifurika kuhani.

Matajiri wa Mikoa ya Kilimanjaro na Arusha wakiwa na magari ya kifahari wamefurika katika msiba huo na habari zaidi zinasema mamilioni ya shilingi yamechangwa kwa ajili ya kufanikisha mazishi ya bilionea huyo aliyefariki dunia, Jumamosi iliyopita kwenye ajali ya ndege.

Ajali hiyo ilitokana na ndege aina ya MT 7- yenye namba 5H-QTT ambayo alikuwa akiiendesha mwenyewe kuanguka kwenye Uwanja wa Ndege wa Arusha, baada ya bawa lake kugonga mti katika eneo la Magereza linalopakana na uwanja huo.

Alifariki dunia wakati askari magereza waliompa msaada walipokuwa wakimkimbiza hosipitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu kutokana na majeraha makubwa aliyoyapata kichwani.

Meneja wa Uwanja wa Ndege Arusha, Ester Dede alisema uchunguzi wa ajali hiyo unaendelea kufanywa na wataalamu wawili wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga kutoka Dar es Salaam.

Magari makubwa yaliyosheheni vyakula na vinywaji yamekuwa yakiingia na kutoka katika makazi ya Sambeke ambako waombelezaji wote wameandaliwa maeneo maalumu ya kuketi yaliyofunikwa na mahema ambako vinywaji na vyakula vinatolewa.

Msemaji wa familia, Dk Richard Masika alisema marehemu atazikwa katika eneo la Karanga mjini Moshi ilipo nyumba yake na kwamba misa itaanza saa 7.00 mchana katika Kanisa Katoliki mjini Moshi na mazishi kufanyika saa 10.00 jioni.

Habari zaidi zilizopatikana zinaeleza kuwa marehemu atazikwa akiwa amevalia sare za marubani kutokana na kupenda kwake kurusha ndege.

Habari zaidi zinasema familia ya marehemu imekuwa ikifuatilia mali alizokuwa nazo marehemu zikiwemo fedha wakati akipatwa na mauti.
Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari alisema, Babu Sambeke alikuwa ni rafiki wa watu wengi, wakiwapo wanasiasa wa vyama vyote.

"Binafsi baada ya kupata taarifa za kufariki kwa Babu Sambeke, niliwapigia baadhi ya wabunge na mawaziri, wote walishtushwa sana na msiba huu," alisema Nassari.

Babu Sambeke ni mmoja wa wafanyabiashara wa kwanza katika kanda ya Kaskazini kumiliki ndege, na hadi anafariki alikuwa akitumia ndege mbili.Jina lake lilianza kuwa maarufu 1985 akionekana kama mtoto wa mjini `mission town' na baadaye alijiimarisha kibiashara na kuwa na utajiri mkubwa.Kufuru katika msiba wa bilionea Sambeke Arusha - Kitaifa - mwananchi.co.tz

Msiba ni msiba tu ndugu yangu. Roho imeshatoka haya mengine ni kujiridhisha.
 
Ndio kaka lazima upate shida kuelewa.

Huo u-bilionea unaoongelewa hapo ni mahesabu ya shilingi za kitanzania, sio British pound au US dollar.

Ukiwa bilionea Tanzania unaweza kununua kadege kama hiko cha bilionea Sambeke. Umeona picha ya "ndege" ya bilionea Sembeke? Ni haki yake kuitwa bilionea kama alimiliki shilingi bilioni na ushee za kitanzania.

Ukiwa milionea wa US dollar unaweza kununua Private jet kama hii.

Safi sana mkuu,umefafanua vizuri sana!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom