Kufungwa kwa Jukwaa la DINI

Asante sana Mkuu invisible kwa mabadiliko haya. Pia tunashukuru wengine tutapata access ya jukwaa la dini, na kuwa kutakuwa na taratibu general na specific kwa jukwaa hilo. Ni ukweli usiopingika kuwa masuala ya dini ni sensitive sana. Kwa mantiki hii wachangiaji ni lazima wawe na mipaka ya maneno (abusive words kwa dini). Sasa hapa kama ni kufungiwa naamini namba ya lockups itaongezeka (that is my prediction). Kwa upande wa mambo ya kikubwa naomba libakie private tu ila kule nako kuwe na mambo ambayo siyo yanayozidi mipaka ya binadamu. Yaani let us make our JF forum na majukwaa yake user friendly i.e palatable to majority. Binafsi sijaingia majukwa yote mawili (Dini na mambo ya kikubwa) ila I believe kulikuwa na hot debates!!!

Nawapongeza Next Level na Maxishimba kuwa mods wa awali kwa jukwa hili. Pia itapendeza kama mods watakuwa wa pande zote tatu tunazoamini i.e majority believers(muslims, christians and pagans), hii itasaidia moderation ya threads and posts kwani mods watakuwa kama wataalam katika filtering (hili ni wazo langu tu).

Nitafurahi kama our JF itaendelea kuwa jukwa la jamii na amani kama ilivyokuwa kabla ya jukwaa la dini kuwa public.All the best with the changes/modifications!!!!
 
Sasa wewe invisible aka robot uliitisha kura ya nini? huwezi kutufanya watu wazima hamnazo....tumepiga kura kumbe wewe tayari una matokeo......
"ati nafunga jukwaa la dini" si ungefunga tu bila kutupigisha kura......
jukwaa lilikuwa private na anaeingia kule anajua anafata nini.......hivi unafikiri mimi utanishawishi nikubaliane na ukristo au uislamu wakati najua hawanifikishi popote?

......nimesikitika sana.....kumbe ina maana hata kule siasani ni watu wanapiga mayowe tu hamna la maana,kwa sababu kitu mnachopigia kelele nyie wenyewe ndio wakwanza kuvunja........

....watu wanasema ccm iliiba kura....inabaka demokrasia...sijui mafisadi.....sisi wenyewe hatui practise demokrasia.......sisi ndio mafisadi....

....anyway this is ur forums....siku nyingine usituitishe kura za kifisadi tena kama hii amua uonavyo....

yanayojadiliwa jukwaa la kikubwa mmeyapa baraka zoote.....dini ilikuwa inaleta mijadala ambayo ambayo inapigania kwenda mbinguni....jukwaa la kikubwa lina faida gani? zaidi ya kuweka picha watu wakifanya mapenzi kinyume na maumbile.......kesho mtakuja kuanzisha thread ati maadili kwa watoto wetu yameshuka.......
 
Katika sehemu ambayo Invisible kapata upizani wa kweli ni hapa...yaani watu wanapiga mawe balaaaaaaaa....wana hasira...yaani ukijitokeza tu mzee wanakuzima.
 
Mkuu Next Level,
Kuna wakati flani ubabe hutumika kwa manufaa ya wengi... Kuitisha kura kule ni kutekeleza wajibu lakini just imagine ndani ya kura yenyewe ukaingia mhadhara!

Mkuu Invisible,

SASA naanza kuelewa kwa nini CCM inawachagulia viongozi ndugu zetu kule Zanzibar....Lol!
 
Yananikumbusha ya Kivuitu Kenya. Yani jukwaa la Dini kufungwa kunapunguza raha hapa JF.
 
Mkuu Mchukia Fisadi,
Mambo ya Kikubwa sijapata lawama hata kidogo... Kama linakusumbua basi mkuu wacha nikuondoshee access haraka kabla hujakosa exit door!
Sio lazima yaletwe malalamiko wewe unajua kuwa jukwaa lile liko kinyume na mila zetu watanzania....na JF ni kioo cha jamii..wewe kama una mtoto ukimkuta kule anaangalia mapicha yale utafurahi?
....maana unatoa access hujui unaempa ni mtoto au vipi......
 
Nionavyo tunakoelekea tutafika mahali jukwaa la siasa nalo litakuwa Categorized kwa vyama vya siasa ili mtu wa cuf azungumzie masuala ya cuf na sisi m azungumzie ya sisi m na wa chadema azungumzie ya chadema.
Kwa sasa jukwaa hilo limesheheni criticism sana na naogopa kama tutakwenda kwa mwendo wa kuogopa kila mapenzi ya watu hapa patabana. Nategemea siku moja kuona watu wa sisi mafisadi wakija na utetezi wa ufisadi kwa kasi ya ajabu na tusiwashangae. Tuwa challenge kwa hoja hadi wakimbie.
Hakuna haja ya kuwa na jukwaa lililo na mipaka kidhehebu! We acha tu watu waseme wanavyoona imani za watu wengine zilivyo na kasoro na uenda hiyo ikawaponya na jehanamu wengi.
Uislamu na Ukristo usingeenea bila kuzisema dini zilizoitwa za kijima na kuwashawishi watu kuziacha. Nakwambia watu wangekuwa bado wanafanya ibada zao kwenye mibuyu ya Dodoma na majabali ya Singida hadi sasa hivi. Je makuhani wao nao walalamike?
Naomba tusifike huko ingawa imani zetu zinatuumiza. Tujifunze kuvumilia. Hapo ndipo tutaonyesha hata huo tunaoita ukomavu wa kisiasa. Mbona huku mitaani watu wanaendeleza hiyo mijadala live na wengine wanaumia na wengine wanacheka na hakuna kupigana? Najua kuna dini moja tu ambayo haina uvumilivu wa kuambiwa ukweli maana ukishawasema tu, pasiwepo mawe au majambia karibu, maana umekwisha. Na hili ndilo lililo hapa jf sasa. Poleni wapenzi wa jukwaa la dini. Ni afadhali kwamba imesemekana litakuwa open:)
 
Mimi nadhani jukwaa la dini lingebakia private. Watoane ngeu humo humo bila kutuhusisha wengine. Pamoja na kukutakia kila la heri kwenye hili lakini nina shaka kama utaweza kuwadhibiti hawa jamaa. Watukuumiza kichwa bure! Lazima watatukanana maana ndivyo walivyozoea.

Amandla............
 
Na sasa wameondolewa jukwaa lao watakuja kuleta tabu kwenye fora nyingine huku.
 
Na sasa wameondolewa jukwaa lao watakuja kuleta tabu kwenye fora nyingine huku.
Kwani wanaoshiriki jukwaa la Dini si wako hata katika majukwaa mengine nayo wanashiriki. Ama unataka sema wao walikuwa kule tu. Yani sijui itamchukua siku ngapi Invisible na timu yake kumaliza kulikarabati jukwaa lile ADHIMU, manake raha ya JF inapungua bila kutoa kuwaidhisha yaleyatokayo kwa Mola.
 
Ok, Nashukuru kwa taarifa Invisible, maana nilishituka nilipofungua na kulikosa Jukwaa pekee ambalo linanivutia kuingia hapa.

Kitu kimoja watu wafahamu hata Jukwaa la Dini litakaporudi na kuwekwa wazi kwa kila mmoja kuchangia ni kwamba, Dini ni Imani, na Imani ni ya mtu binafsi, hivyo wachangiaji wake wawe makini na kulazimisha Imani yake ni bora kuliko Imani ya mwenzake, na pindi mwenye imani tofauti ya kwake anapokataa kukubaliana na anachosema, ndio pale huanza maneno ya kashfa juu ya dini ya mwenzake.

Naamini kitu kimoja, Dini zote zinawaongoza watu wkenda kwake yeye aliye mmoja, anayepaswa kuabudiwa (MUNGU) bila kujali wanatumia njia gani. Hivyo, shime kwa wachangiaji wote wa Jukwaa la Dini kutoa maoni na michago itakayosaidia kuwajenga watu kiimani na sio kuponda na kuikandia imani ya mwenzako, iwe unaijua au huijui.

Tutalisubiri jukwaa litakapofunguliwa ili tuweze kuendelea kumtukuza yeye anayetupigania.

Mbarikiwe.
 
Wakuu,

Nasikitika kutangaza kufungwa kwa Jukwaa la Dini.

Malalamiko dhidi ya jukwaa hili yamekuwa mengi na moderators hawataweza kuvumilia kero zinazotokana na malalamiko haya.

Ukweli ni kwamba malalamiko yote yako sahihi na pia LILIKUWA NA MATATIZO ambayo dawa yake ni kulipitia upya na kuchukua hatua muhimu kwa manufaa ya wote wanaolitumia.

Izingatiwe kuwa, sheria zitazingatiwa katika kulipitia upya na lugha yoyote itakayoonekana kuwa CHAFU ama kejeli zisizo za lazima zitafutiliwa mbali na wahusika watafahamishwa.

Baada ya kulipitia jukwaa hili, litakuwa public na litakuwa chini ya uangalizi wangu na moderators wengine wawili wapya watakaotambulishwa kwenu.

Nasikitika kwa usumbufu utakaojitokeza kwa YEYOTE. Ni hatua ambayo kwa sasa haikwepeki na ni LAZIMA iwe ilivyo sasa.

Ahsanteni
Miaka 15 imepita sasa, lirudisheni jukwaa la dini liwe public na malalamiko yote yashugulikiwe kama mnavyofanya katika majukwaa mengine yote.

Ninaamini hata jukwaa la siasa mnapata malalamiko mengi ila hamlifungii.
 
Back
Top Bottom