miradibubu
JF-Expert Member
- Sep 21, 2010
- 312
- 84
Salaam kwenu nyote wapenda maendeleo wa dhati hapa Tanzania. Ninayo furaha kubwa kuwataarifu kwamba sisi wanajumuiya ya Chuo Kikuu Cha Dodoma ambao ni wafuasi wa dhati wa CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO- CHADEMA, tumeamua kufungua tawi letu ambalo litaendelea kutuunganisha na kuweka pamoja nguvu zetu ili kuleta mabadiliko ya kweli.
Tawi hili linakusudiwa kuwa hapo maeneo ya mjini ambapo tutapangisha ofisi nzuri na tutawajibika kuilipia pango kwa muda wote. Litafunguliwa mwanzoni mwa mwezi januari 2011.
CHADEMA ina wafuasi wengi sana katika hiki chuo tofauti sana na wengine wanavyodhani.
Ninaomba kutoa uthibitisho wa hili kama ifuatavyo:
1. Wakati wa kampeni uongozi wa Chuo uliamua kutoa mabasi yanayotumiwa na wafanyakazi ili yawapeleke wafanyakazi kuhudhuria mkutano wa Kikwete uliofanyika hapa Dodoma.Tofauti na uongozi wa chuo ulivyotarajia mabasi yale hayakupata watu katika njia zote yalikotumwa.
Kwa mfano, katika eneo la Kisasa wanakoishi walimu mabasi mawili yale makubwa hayakuambulia hata mwalimu mmoja, njia ya Nkuhungu basi la watu 65, lilipata watu wawili tu na njia ya Mipango basi lilipata mtu mmoja tu.
2. Katika chaguzi zote za uongozi hapa chuoni ni kosa kubwa sana kwa mgombea kubainika kwamba yeye ni mwa CCM.
Kwani kitakachompata ni kukosa kura, mifano ni hii hapa kuna kijana anaitwa Tery yule alisoma risala ya kipuuzi siku Kikwete amaetangazwa kuwa mgombea wa CCM.
Risala hiyo ilipewa jina la risala ya wanafunzi wa elimu ya juu, huyu Tery aligombea nafasi ya uraisi wa serikali ya wanafunzi, kamuulizeni kilichompata ni nini, kwani kura hazikutosha.
Mfano wa piili unawahusu Wahadhiri walioenda kugombea kwa tiketi ya CCM, katika majimbo ya Manyoni mashariki na mwingine katika jimbo lililokuwa la Samwel Chitalilo, wote hawa waligombea uongozi wa UDOMASA - CHAMA CHA WANATAALUMA UDOM, walikosa kura si kwa kukosa uwezo bali tu kule kufungamana na CCM.
Mfano wa piili unawahusu Wahadhiri walioenda kugombea kwa tiketi ya CCM, katika majimbo ya Manyoni mashariki na mwingine katika jimbo lililokuwa la Samwel Chitalilo, wote hawa waligombea uongozi wa UDOMASA - CHAMA CHA WANATAALUMA UDOM, walikosa kura si kwa kukosa uwezo bali tu kule kufungamana na CCM.
3. Serikali ya wanafunzi kushikiriwa na vijana machachari wa Chadema.
4. Mijadala mikali katika mabasi na maeneo ya ofisi inayowahusisha wafanyakazi wa chuo yote imekuwa ikiipinga CCM kwa kiwango kikubwa na kuifagilia CHADEMA.
5. Kipindi cha kampeni wafanyakazi wengi na kwa uwazi waliiunga mkono CHADEMA, kutokana na hali hii hakuna mwana CCM aliyekuwa tayari kuitetea ccm hata kwa wale walioenda kugombea kwa tiketi ya CCM hawakuweza kukabiliana na nguvu kubwa ya Chadema.
6.Kauli ya kikwete kuwaasa wana UDOM wasitumiwe na wanasiaasa baada ya kubaini kwamba CHADEMA ina nguvu kubwa sana hapa mpaka imefikia hali ya kuhitaji kufanya mkakati madhubuti wa kudhibiti halii hii kupitia uongozi wa juu wa chuo na kuleta makada wa CCM kuja kunusuru hali.
7. UDOM kuwa ndani ya kata iliyochukuliwa na CHADEMA- kata ya Dodoma Makulu, kuna mchango mkubwa sana wa wana UDOM katika kufanikisha hili.
8. Wafanyakazi wa UDOM kusafiri kwenda mlimani yaani UDSM kumpigia kura mnyika hili ni kundi kubwa sana la vijana waliomaliza chuo hivi karibuni ambao wameajiliwa hapa UDOM, ilikuwa ni uzalendo wa hali ya juu sana kufanikisha hili na pasipo malipo yoyote zaidi ya kupigania haki ya WATANZANIA.
Hivyo basi kutokana na hoja hizo nane tumebaini kabisa ya kwamba Wana CHAADEMA tupo wengi sana na hivyo tunahitaji sehemu yetu itakayotuunganisha na kutupatia nafasi ya kujadiliana mambo yetu, tawi hili litakuwa kiungo muhimu kati ya Walimu, wanafunzi na wafanyakazi wengine waendeshaji.
RAI YETU
Rai yetu kwenu ni juu ya kuhitaji kuungwa mkono katika mchakato huu, si uhitaji wa mali bali hasa mchango wa mawazo na ushauri kwani ni suala nyeti na ambalo halitawafurahisha wengi lakini tumeamua kufanya haya si kwa kushawishiwa na uongozi wa juu au wa mkoa wa CHADEMA.
Rai yetu kwenu ni juu ya kuhitaji kuungwa mkono katika mchakato huu, si uhitaji wa mali bali hasa mchango wa mawazo na ushauri kwani ni suala nyeti na ambalo halitawafurahisha wengi lakini tumeamua kufanya haya si kwa kushawishiwa na uongozi wa juu au wa mkoa wa CHADEMA.
Pia kwa Wana CHADEMA wenzetu tunaomba tusaidiane klupambana na propaganda mbaya inayojaribu kuaminisha watanzania wote kwamba wafanyakazi na wanafunzi wote wa Udom ni CCM, ninajua wengine mnafanya hivyo kwa hasira baada ya kuzidiwa na nguvu ya propaganda na wengine ni kutokana na kukosa taarifa sahihi.
Tunatambua kwamba CCM wanawagawia kadi wanafunzi hadi mabwenini tena kwa kuwaandika majina pasipo ridhaa yao na kuwaomba wawape picha passport size wawaletee kadi.
Pia wameweka viongozi wao wa matawi katika mabweni, licha ya jitihada hizi wanazozifanya bado upinzani una nguvu kubwa kwani wanafunzi wanaelewa nini ccm inafanya, na wale wachache wanaojiunga na ccm hapa chuoni ni kutokana na mtazamo potofu wa kudhani kwamba mtu hawezi kuajiriwa mpaka uwe na kadi ya CCM.
Pia wameweka viongozi wao wa matawi katika mabweni, licha ya jitihada hizi wanazozifanya bado upinzani una nguvu kubwa kwani wanafunzi wanaelewa nini ccm inafanya, na wale wachache wanaojiunga na ccm hapa chuoni ni kutokana na mtazamo potofu wa kudhani kwamba mtu hawezi kuajiriwa mpaka uwe na kadi ya CCM.
Mtazamo huu tumepambana nao sana tena kwa kutoa mifano tukionesha watu walioamini hivyo huku mpaka wakati huu hali zao bado ni mbaya sana.
Kimsingi huu ni mtazamo potofu amabao unawatafuna baadhi ya wasomi wetu katika vyuo vingi na hao ndio wanakuja kuwa watu kama Benson Bana kwani hata anavyoongea amejaa kujipendekeza zaidi ili akumbukwe, nadhani mlimuona jana kwenye kipima joto ITV,alivyokuwa anajikanyaga kuonesha namna ambavyo watanzania wana hali nzuri mpaka kufikia uwezo wa kuendesha magari.
Ninaomba msitishwe na matamko yanayotolewa na baadhi ya watu yakihusisha sisi UDOM, mengine ni propaganda za ccm, mengine ni ya kutungwa na vijana wa CCM ambao wanasoma hapa na hata makao makuu CCM wanafahamu kwamba wapo hapa, hivyo basi ni lazima waoneshe kwamba wanafanya kazi kubwa.
CHADEMA itaendelea kustawi hapa Udom hata kama viongozi wa ngazi ya juu wangefanya nini.
Mungu ibariki CHADEMA , Mungu ibariki Tanzania na Viongozi wote wa CHADEMA