DOKEZO Changamoto UDOM (College ya Informatics)

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Wanafunzi wa UDOM college ya informatics wamekua na changamoto kadha wa kadha.

1. Ubovu wa miundombinu hasa choo kwa baadhi ya blocks(1 and 3) hali inayopelekea kushindwa kujisaidia na kupata huduma vizuri hasa block 3 Lina wanafunzi zaidi ya 450 lakini matundu ya vyoo vinayofanya kazi ni 3 tu vingine vyote vimeziba huu ni mwaka wa 3 kumekua na hali hii.

2. Changamoto ya hostel: Kumekuwa na wimbi kubwa la wanafunzi waliodahiliwa mwaka huu wa masomo hali inayopelekea wanafunzi kukosa makazi ili hali wamelipia hostel kwa kukumbana na Changamoto ya kupangiwa chumba kimoja watu zaidi ya 8.

3. Kuhamishwa chumba ulichopangiwa na kupelekwa kingine(ili aje mtu mwingine)ambacho pia kimepangiwa mtu mwingine na endapo utabaki unapokaa wataletwa walinzi wachukue magodoro hali inayopelekea wanafunzi kulala sakafuni.
 
Yudom kutakuwa nashida sana
1) kwa wanafunzi hususani utunzaji wa miundombinu.
2)uongozi wa wanafunzi katika uwasilishaji wa changamoto za aanafunzi
3)uongozi wa juu hususani namna ya uendeshaji na utatuaji wa masuala mbalimbali
 
UDOM ni chuo ambacho inaonekana dhahiri,kina shida ya uongozi makini,kuanzia UDOSO hadi juu kabisa.Kuna kipindi kulikua na shida ya maji,wanafunzi wakawa wanahangaika kinoma,mwaka uliofuata tena kukawa na shida ya maji pia,nikashangaa sana,kwamba kwanini chuo kikubwa hivi,kinakosa ufumbuzi wa kudumu wa tatizo la maji,nikatafakari nikabaini kua tatizo lipo kwa UDOSO na uongozi wa juu wa chuo,kwani ilikua ukifuatilia inasemekana eti mabomba huwa yanapasuka,hivyo kupelekea shida ya maji.Sasa kweli chuo kikubwa hivyo,kinaingiza mapato kila leo,kinashindwa kununua mabomba imara,na kuondoa tatizo dogo kama hilo,linalopelekea wanachuo kuhangaika?
Nyie wanafunzi wa informatics,hebu thubutuni hata kuandamana muondoe serikali ya UDOSO,na ikiwezekana alikeni vyombo vya habari vikubwavikubwa,maana wameshindwa kutatua matatizo madogo kama hayo na mengineyo,ilhali mnakatwa pesa za kuwalipa wao,no wonder Jenerali Ulimwengu anasema baadhi ya vyuo vyasasa vimekua ni extended high schools.
 
Nipo UDOM pia niseme tu ukweli sisi wanafunzi ndio source ya haya matatizo.Tabia ya sisi wanafunzi kujihesabia haki na kuonesha kama tunaonewa wakati kiuhalisia sisi ndio wenye makosa hatutunzi miundombinu yetu pia sio wastaarabu.

Unakuta mtu anaenda chooni na kopo moja tu wakati chini maji yapo mengi ila mwanafunzi huyu anaona uvivu kwenda kuchota maji ya kuflashia mwisho wa siku choo kinaziba na kesho unakuja kulalamika vyoo vichafu.

Hii tabia ya kuchafua chuo na uongozi tuache haifai....Acha tabia za kichawi kijana.

Kuhusu hostel Udom hostel zipo kibao ila inajulikana kama hujalipa ada na kumaliza usajili huwezi kupewa makazi.
 
UDOM ni chuo ambacho inaonekana dhahiri,kina shida ya uongozi makini,kuanzia UDOSO hadi juu kabisa.Kuna kipindi kulikua na shida ya maji,wanafunzi wakawa wanahangaika kinoma,mwaka uliofuata tena kukawa na shida ya maji pia,nikashangaa sana,kwamba kwanini chuo kikubwa hivi,kinakosa ufumbuzi wa kudumu wa tatizo la maji,nikatafakari nikabaini kua tatizo lipo kwa UDOSO na uongozi wa juu wa chuo,kwani ilikua ukifuatilia inasemekana eti mabomba huwa yanapasuka,hivyo kupelekea shida ya maji.Sasa kweli chuo kikubwa hivyo,kinaingiza mapato kila leo,kinashindwa kununua mabomba imara,na kuondoa tatizo dogo kama hilo,linalopelekea wanachuo kuhangaika?
Nyie wanafunzi wa informatics,hebu thubutuni hata kuandamana muondoe serikali ya UDOSO,na ikiwezekana alikeni vyombo vya habari vikubwavikubwa,maana wameshindwa kutatua matatizo madogo kama hayo na mengineyo,ilhali mnakatwa pesa za kuwalipa wao,no wonder Jenerali Ulimwengu anasema baadhi ya vyuo vyasasa vimekua ni extended high schools.
Kuandamana haijawahi kuwa solution ya kusolve changamoto.
 
Miaka ya nyuma,ambapo vyuo vilikua vyuo kweli na siyo extended high schools,maandamano yakikua ni moja ya suluhu.Kama wewe ni current University student wa hapo UDOM,sikushangai,may be hujui protest ninini na aina za protests ni zipi.
Zama zinabadilika.
 
Back
Top Bottom