Kufungua tawi la chadema udom | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kufungua tawi la chadema udom

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by miradibubu, Dec 11, 2010.

 1. m

  miradibubu JF-Expert Member

  #1
  Dec 11, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 313
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Salaam kwenu nyote wapenda maendeleo wa dhati hapa Tanzania. Ninayo furaha kubwa kuwataarifu kwamba sisi wanajumuiya ya Chuo Kikuu Cha Dodoma ambao ni wafuasi wa dhati wa CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO- CHADEMA, tumeamua kufungua tawi letu ambalo litaendelea kutuunganisha na kuweka pamoja nguvu zetu ili kuleta mabadiliko ya kweli.

  Tawi hili linakusudiwa kuwa hapo maeneo ya mjini ambapo tutapangisha ofisi nzuri na tutawajibika kuilipia pango kwa muda wote. Litafunguliwa mwanzoni mwa mwezi januari 2011.

  CHADEMA ina wafuasi wengi sana katika hiki chuo tofauti sana na wengine wanavyodhani.

  Ninaomba kutoa uthibitisho wa hili kama ifuatavyo:

  1. Wakati wa kampeni uongozi wa Chuo uliamua kutoa mabasi yanayotumiwa na wafanyakazi ili yawapeleke wafanyakazi kuhudhuria mkutano wa Kikwete uliofanyika hapa Dodoma.Tofauti na uongozi wa chuo ulivyotarajia mabasi yale hayakupata watu katika njia zote yalikotumwa.

  Kwa mfano, katika eneo la Kisasa wanakoishi walimu mabasi mawili yale makubwa hayakuambulia hata mwalimu mmoja, njia ya Nkuhungu basi la watu 65, lilipata watu wawili tu na njia ya Mipango basi lilipata mtu mmoja tu.

  2. Katika chaguzi zote za uongozi hapa chuoni ni kosa kubwa sana kwa mgombea kubainika kwamba yeye ni mwa CCM.

  Kwani kitakachompata ni kukosa kura, mifano ni hii hapa kuna kijana anaitwa Tery yule alisoma risala ya kipuuzi siku Kikwete amaetangazwa kuwa mgombea wa CCM.

  Risala hiyo ilipewa jina la risala ya wanafunzi wa elimu ya juu, huyu Tery aligombea nafasi ya uraisi wa serikali ya wanafunzi, kamuulizeni kilichompata ni nini, kwani kura hazikutosha.
  Mfano wa piili unawahusu Wahadhiri walioenda kugombea kwa tiketi ya CCM, katika majimbo ya Manyoni mashariki na mwingine katika jimbo lililokuwa la Samwel Chitalilo, wote hawa waligombea uongozi wa UDOMASA - CHAMA CHA WANATAALUMA UDOM, walikosa kura si kwa kukosa uwezo bali tu kule kufungamana na CCM.

  3. Serikali ya wanafunzi kushikiriwa na vijana machachari wa Chadema.

  4. Mijadala mikali katika mabasi na maeneo ya ofisi inayowahusisha wafanyakazi wa chuo yote imekuwa ikiipinga CCM kwa kiwango kikubwa na kuifagilia CHADEMA.

  5. Kipindi cha kampeni wafanyakazi wengi na kwa uwazi waliiunga mkono CHADEMA, kutokana na hali hii hakuna mwana CCM aliyekuwa tayari kuitetea ccm hata kwa wale walioenda kugombea kwa tiketi ya CCM hawakuweza kukabiliana na nguvu kubwa ya Chadema.

  6.Kauli ya kikwete kuwaasa wana UDOM wasitumiwe na wanasiaasa baada ya kubaini kwamba CHADEMA ina nguvu kubwa sana hapa mpaka imefikia hali ya kuhitaji kufanya mkakati madhubuti wa kudhibiti halii hii kupitia uongozi wa juu wa chuo na kuleta makada wa CCM kuja kunusuru hali.

  7. UDOM kuwa ndani ya kata iliyochukuliwa na CHADEMA- kata ya Dodoma Makulu, kuna mchango mkubwa sana wa wana UDOM katika kufanikisha hili.

  8. Wafanyakazi wa UDOM kusafiri kwenda mlimani yaani UDSM kumpigia kura mnyika hili ni kundi kubwa sana la vijana waliomaliza chuo hivi karibuni ambao wameajiliwa hapa UDOM, ilikuwa ni uzalendo wa hali ya juu sana kufanikisha hili na pasipo malipo yoyote zaidi ya kupigania haki ya WATANZANIA.

  Hivyo basi kutokana na hoja hizo nane tumebaini kabisa ya kwamba Wana CHAADEMA tupo wengi sana na hivyo tunahitaji sehemu yetu itakayotuunganisha na kutupatia nafasi ya kujadiliana mambo yetu, tawi hili litakuwa kiungo muhimu kati ya Walimu, wanafunzi na wafanyakazi wengine waendeshaji.​

  RAI YETU
  Rai yetu kwenu ni juu ya kuhitaji kuungwa mkono katika mchakato huu, si uhitaji wa mali bali hasa mchango wa mawazo na ushauri kwani ni suala nyeti na ambalo halitawafurahisha wengi lakini tumeamua kufanya haya si kwa kushawishiwa na uongozi wa juu au wa mkoa wa CHADEMA.​

  Pia kwa Wana CHADEMA wenzetu tunaomba tusaidiane klupambana na propaganda mbaya inayojaribu kuaminisha watanzania wote kwamba wafanyakazi na wanafunzi wote wa Udom ni CCM, ninajua wengine mnafanya hivyo kwa hasira baada ya kuzidiwa na nguvu ya propaganda na wengine ni kutokana na kukosa taarifa sahihi.​

  Tunatambua kwamba CCM wanawagawia kadi wanafunzi hadi mabwenini tena kwa kuwaandika majina pasipo ridhaa yao na kuwaomba wawape picha passport size wawaletee kadi.
  Pia wameweka viongozi wao wa matawi katika mabweni, licha ya jitihada hizi wanazozifanya bado upinzani una nguvu kubwa kwani wanafunzi wanaelewa nini ccm inafanya, na wale wachache wanaojiunga na ccm hapa chuoni ni kutokana na mtazamo potofu wa kudhani kwamba mtu hawezi kuajiriwa mpaka uwe na kadi ya CCM.​

  Mtazamo huu tumepambana nao sana tena kwa kutoa mifano tukionesha watu walioamini hivyo huku mpaka wakati huu hali zao bado ni mbaya sana. ​

  Kimsingi huu ni mtazamo potofu amabao unawatafuna baadhi ya wasomi wetu katika vyuo vingi na hao ndio wanakuja kuwa watu kama Benson Bana kwani hata anavyoongea amejaa kujipendekeza zaidi ili akumbukwe, nadhani mlimuona jana kwenye kipima joto ITV,alivyokuwa anajikanyaga kuonesha namna ambavyo watanzania wana hali nzuri mpaka kufikia uwezo wa kuendesha magari.​

  Ninaomba msitishwe na matamko yanayotolewa na baadhi ya watu yakihusisha sisi UDOM, mengine ni propaganda za ccm, mengine ni ya kutungwa na vijana wa CCM ambao wanasoma hapa na hata makao makuu CCM wanafahamu kwamba wapo hapa, hivyo basi ni lazima waoneshe kwamba wanafanya kazi kubwa.​

  CHADEMA itaendelea kustawi hapa Udom hata kama viongozi wa ngazi ya juu wangefanya nini.​

  Mungu ibariki CHADEMA , Mungu ibariki Tanzania na Viongozi wote wa CHADEMA​
   
 2. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #2
  Dec 11, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Heshima kwako Miradibubu,

  Mkuu hongera kaza buti tunataka wasomi wengi vijana waisaidie Tanzania sasa na siku zijazo.Vijana ni taifa la leo na kesho.
   
 3. bwegebwege

  bwegebwege JF-Expert Member

  #3
  Dec 11, 2010
  Joined: Jul 30, 2010
  Messages: 1,031
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Hongereni lakini mkumbuke kufuata taratibui zilizowekwa na Chuo na mhakikishe hamkiuki sheria za nchi wakati wa mchakato mzima wa ufunguzi na uendeshaji wa tawi lenu! Ushauri mwingine ninaowapiatia ni kuhakikisha mnaweka msisistyizo na kipaumbele kwenye elimu, ndiyo iliyowapeleka chuoni!! ELIMU KWANZA!!
  Kila la kheri
   
 4. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #4
  Dec 11, 2010
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Umenena vizuri. Ongezeni vitendo ili hiyo taa imulike TZ nzima.
   
 5. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #5
  Dec 11, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  wewe kweli *****, kwa maandishi hayo hapo juu unaona kuna mtu wa kukurupuka? wape moyo bwana acha kuwatisha vijana wameamua kujikomboa.
   
 6. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #6
  Dec 11, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  Tunatambua kwamba CCM wanawagawia kadi wanafunzi hadi mabwenini tena kwa kuwaandika majina pasipo ridhaa yao na kuwaomba wawape picha passport size wawaletee kadi.
  Pia wameweka viongozi wao wa matawi katika mabweni, licha ya jitihada hizi wanazozifanya bado upinzani una nguvu kubwa kwani wanafunzi wanaelewa nini ccm inafanya, na wale wachache wanaojiunga na ccm hapa chuoni ni kutokana na mtazamo potofu wa kudhani kwamba mtu hawezi kuajiriwa mpaka uwe na kadi ya CCM.


  hata nje ya nchi pia hii imekuwa kama defensive mechanism fulani hivi, mfano mgaya wa TUCTA walipodai anatumiwa na chadema alisema kuwa yeye ni mwana ccm nakuitaja namba ya kadi ya ccm, mengi alifanya hivyo, mwandishi Francis Godwin naye alifanya hivyo.
  sasa hivi kuna vijana wamepewa kazi hiyo na vitendea kazi vya kisasa digital camera,printer kutekeleza hilo tena wanasumbua kweli kweli kuwapigia watu simu. Rafiki yake na rafiki wangu anafaya hiyo kazi anadai kuwa akishapata wanachama wengi kuna mapande mbeleni
   
 7. Mtumiabusara

  Mtumiabusara JF-Expert Member

  #7
  Dec 11, 2010
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 473
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Hilo nalo neno. Nafikiri nyinyi anzisheni tu hilo tawi kama utaratibu unaruhusu. Nguvu ya Umma kama ipo itajithihirisha, otherwise kama kuna ukweli mwingine kuhusu mtazamo wa wanafunzi UDOM nalo litakuwa wazi tu with time.
   
 8. w

  wamlaga Member

  #8
  Dec 11, 2010
  Joined: Jun 19, 2010
  Messages: 22
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Naamini umetujibu kwa nia njema kabisa asante kwa ushauri wako. labda haukuona vema eneo ambalo hili tawi linafunguliwa si katika eneo la chuo kwani ni mjini kabisa. pia wanofungua ni wafanyakazi na wanafunzi hivyo usihofu wanafunzi hatapewa majukumu mazito yatakayo sababisha kushuka ufanisi katika masomo yao, asante tena
   
 9. F

  Froida JF-Expert Member

  #9
  Dec 11, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Hongereni sana ,kumbukeni nchi hii itajengwa na sisi wenyewe nyie ni vijana wasomi wenye uwezo wa kupambanua mambo mengi ya mustakabali wa taifa letu mutakapokuwa kwenye taasisi za kisiasa na kuongeza nguvu ya uelewa wenu mutasaidia sana kueneza elimu ya urai na haki za watu katika nyanja mbalimbali ni jambo zuri na huo ndio uzalendo mahala pengi duniani wanafunzi wa vyuo vikuu wana michango mikubwa sana ya kisiasa katika nchi zao,masomo mema
   
 10. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #10
  Dec 11, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Itabidi sasa wajenge(ccm na waarabu wao) chuo kingine. Udom imekombolewa

  kazeni buti vijana.
   
 11. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #11
  Dec 11, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hii safi sana ...
   
 12. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #12
  Dec 11, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Safi sana,atleast naanza kuhisi udom sio wasaliti wa democracy
   
 13. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #13
  Dec 11, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hahaha this is good for UDOM. Sasa tunawa-upgrade kwenda "Middle School". Mtakuwa chini ya uangalizi kabla ya kupewa status ya wasomi. Mifano yote ni mizuri ila tunataka kusikia JK anaogopa kujigawia degree hapo.
   
 14. B

  Bull JF-Expert Member

  #14
  Dec 11, 2010
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kufungua matawi siyo issue, Nyie walokole mkumbuke CCM, CUF vilisha kuwa na matawi mengi mpaka nje ya nchi, sasa nyie mnaanza kujigamba na kita cha UDOM


  Mnatikiwa kuleta democrasia ndani ya chama chenu cha mtandao, badala ya kupeana madaraka, ubunge kikabilakabila na udiniudini!!


  Kinachochosha hapa jf, chadema wakifanya utumbo wowote imekuwa News, huu ni ulimbukeni na kutokomaa kisiasa kwa chama hiki na wafuasi wake
   
 15. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #15
  Dec 11, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  hizo rasharasha tu
   
 16. w

  wamlaga Member

  #16
  Dec 11, 2010
  Joined: Jun 19, 2010
  Messages: 22
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  sawa yetu macho
   
 17. k

  kiche JF-Expert Member

  #17
  Dec 11, 2010
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mimi uwa nashangaa jinsi watu wanapodanganywa kirahisi,na ningeomba mnaochangia humu muondoe mawazo eti ccm ina nguvu vyuoni,huo ni uongo wa kishetani,na ni punguani tu anayeweza kutekwa na propaganda hizo,ukweli wa mambo ccm haina bao vyuo vikuu,ni watu wanajipendekeza na kutoa maneno ya kiuendawazimu kuonyesha kuwa ccm wapo,mfano chuo cha ifm uchaguzi wa ifmso uliopita kuna mgombea anaitwa kigoda alitumia uccm licha ya kuwa anatoka kozi yenye watu karibu ya nusu ya wanafunzi wa chuo,alibwagwa chini kwenye uraisi na mwanafunzi toka kozi ya Taxi ya wanafunzi 80 tu,kosa lilikuwa uccm,naomba msidanganyike,mtaji wa ccm ni umaskini wetu siyo wasomi.
   
 18. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #18
  Dec 11, 2010
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  Unadhani kwa sababu nyie Waislamu mlilala na sisi tutalala??? Imekula kwenu
   
 19. Jeremiah

  Jeremiah JF-Expert Member

  #19
  Dec 11, 2010
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 642
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Mkuu hongera kaza buti tunataka wasomi wengi vijana waisaidie Tanzania sasa na siku zijazo.Vijana ni taifa la leo na kesho.

  Tanzania bila CCM na kikwete Inawezekana.
   
 20. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #20
  Dec 11, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Very brilliant. Naombeni tu msijifunze ufisadi kwenye kuuza vyumba na vitanda kwa bei za juu kwa wanafunzi wenzenu kama ilivyo pale mlimani na vyuo vingine vya dar!
   
Loading...