Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,890
- 6,898
WABUNGE wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Susan Kiwanga (Viti Maalum) na Sylivester Kasulumbai (Maswa Mashariki), wamehojiwa na Jeshi la Polisi Mkoani Tabora wakituhumiwa kushiriki kumvamia na kumpiga Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Fatma Kimario.
Akizungumza na waandishi wa habari wilayani Igunga, jana, Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Makao Makuu ya Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi Issaya Mungulu, alisema wabunge hao walikamatwa na kuhojiwa kwa saa kadhaa kabla ya kuachiwa.
Akizungumzia kile kilichotokea, Mngulu alisema mkuu huyo wa wilaya alikwenda katika kijiji cha Isakamaliwa kufanya mkutano wa ndani na watendaji wa kijiji hali iliyowafanya wafuasi na viongozi wa CHADEMA kuchukizwa kwa madai kuwa wameingiliwa. "Mkutano wa CHADEMA katika kijiji cha Isakamaliwa ulikuwa ufanyike kati ya saa nne na saa sita. Kikao cha mkuu wa wilaya kilifanyika kati ya saa 7:30 na saa 9:00 alasiri muda ambao CHADEMA hawakuwa na mkutano," alisema.
Hata hivyo, kamanda huyo wa polisi alikiri kuwepo kwa malalamiko ya CHADEMA kuhusiana na kuingiliwa katika maeneo waliyotengewa kufanya kampeni na ukiukwaji wa maadili unaodaiwa kufanywa na mkuu huyo wa wilaya lakini akadai msemaji wa mambo hayo ni msimamizi wa maadili ambaye ni mkurugenzi wa uchaguzi.
Aidha alikiri kwamba askari wake walikuta hali ya amani na utulivu katika kijiji hicho, ndipo walipolazimika kuanza upelelezi kujua ukweli wa tukio hilo. Aliongeza kuwa tuhuma zinazochunguzwa dhidi ya wabunge hao na wafuasi wengine watatu wa CHADEMA, ni kuvamia kikao cha mkuu wa wilaya. Taarifa hizo zinadai kwamba katika tukio hilo mkuu wa wilaya alivuliwa hijabu, viatu, kukatiwa mkufu ambao thamani yake haijajulikana.
"Anadai kuwa simu yake ya mkononi aina ya Samsung yenye thamani ya sh 400,000 ilipotea na kumtukana matusi ya nguoni," alisema na kuongeza kuwa Jeshi la Polisi lilipokea taarifa za tukio hilo kutoka kwa Ofisa Tawala wa Wilaya, Sumera Manoti.
Taarifa zimebainisha kuwa mkuu huyo wa wilaya amefungua jalada la shambulio la aibu namba IR/1115/2011, wakati CHADEMA wamefungua jalada namba IR/1115/2011 linalohusu kuingilia mkutano wa kampeni kwa mujibu wa ratiba ya msimamizi wa uchaguzi. Kwa sasa jeshi hilo linaendelea kukusanya ushahidi kuhusiana na kesi hizo. Hata hivyo, Kamanda Mngulu alitoa wito kwa vyama, viongozi, wanachama, wapenzi na wafuasi wa vyama vya siasa kuacha tabia ya kujichukulia sheria mikononi hususan kipindi hiki cha uchaguzi.
Juzi mkuu wa wilaya hiyo akiwa katika kijiji cha Isakamaliwa, tarafa ya Igunga alivamiwa na viongozi, wafuasi na mashabiki wa CHADEMA muda mfupi baada ya kumaliza kikao cha ndani na watendaji wa vijiji.
Tanzania daima