Kufuatia kibano cha DC (Igunga): Wabunge wa CHADEMA wakamatwa

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,886
6,883
WABUNGE wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Susan Kiwanga (Viti Maalum) na Sylivester Kasulumbai (Maswa Mashariki), wamehojiwa na Jeshi la Polisi Mkoani Tabora wakituhumiwa kushiriki kumvamia na kumpiga Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Fatma Kimario.

Akizungumza na waandishi wa habari wilayani Igunga, jana, Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Makao Makuu ya Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi Issaya Mungulu, alisema wabunge hao walikamatwa na kuhojiwa kwa saa kadhaa kabla ya kuachiwa.

Akizungumzia kile kilichotokea, Mngulu alisema mkuu huyo wa wilaya alikwenda katika kijiji cha Isakamaliwa kufanya mkutano wa ndani na watendaji wa kijiji hali iliyowafanya wafuasi na viongozi wa CHADEMA kuchukizwa kwa madai kuwa wameingiliwa. "Mkutano wa CHADEMA katika kijiji cha Isakamaliwa ulikuwa ufanyike kati ya saa nne na saa sita. Kikao cha mkuu wa wilaya kilifanyika kati ya saa 7:30 na saa 9:00 alasiri muda ambao CHADEMA hawakuwa na mkutano," alisema.

Hata hivyo, kamanda huyo wa polisi alikiri kuwepo kwa malalamiko ya CHADEMA kuhusiana na kuingiliwa katika maeneo waliyotengewa kufanya kampeni na ukiukwaji wa maadili unaodaiwa kufanywa na mkuu huyo wa wilaya lakini akadai msemaji wa mambo hayo ni msimamizi wa maadili ambaye ni mkurugenzi wa uchaguzi.

Aidha alikiri kwamba askari wake walikuta hali ya amani na utulivu katika kijiji hicho, ndipo walipolazimika kuanza upelelezi kujua ukweli wa tukio hilo. Aliongeza kuwa tuhuma zinazochunguzwa dhidi ya wabunge hao na wafuasi wengine watatu wa CHADEMA, ni kuvamia kikao cha mkuu wa wilaya. Taarifa hizo zinadai kwamba katika tukio hilo mkuu wa wilaya alivuliwa hijabu, viatu, kukatiwa mkufu ambao thamani yake haijajulikana.
"Anadai kuwa simu yake ya mkononi aina ya Samsung yenye thamani ya sh 400,000 ilipotea na kumtukana matusi ya nguoni," alisema na kuongeza kuwa Jeshi la Polisi lilipokea taarifa za tukio hilo kutoka kwa Ofisa Tawala wa Wilaya, Sumera Manoti.

Taarifa zimebainisha kuwa mkuu huyo wa wilaya amefungua jalada la shambulio la aibu namba IR/1115/2011, wakati CHADEMA wamefungua jalada namba IR/1115/2011 linalohusu kuingilia mkutano wa kampeni kwa mujibu wa ratiba ya msimamizi wa uchaguzi. Kwa sasa jeshi hilo linaendelea kukusanya ushahidi kuhusiana na kesi hizo. Hata hivyo, Kamanda Mngulu alitoa wito kwa vyama, viongozi, wanachama, wapenzi na wafuasi wa vyama vya siasa kuacha tabia ya kujichukulia sheria mikononi hususan kipindi hiki cha uchaguzi.

Juzi mkuu wa wilaya hiyo akiwa katika kijiji cha Isakamaliwa, tarafa ya Igunga alivamiwa na viongozi, wafuasi na mashabiki wa CHADEMA muda mfupi baada ya kumaliza kikao cha ndani na watendaji wa vijiji.

Tanzania daima
 
Pande zote zimepeleka malalamiko polisi kukosewa haki, nani atashinda kesi?
 
Taarifa zimebainisha kuwa mkuu huyo wa wilaya amefungua jalada la shambulio la aibu namba IR/1115/2011 wakati CHADEMA wamefungua jalada namba IR/1115/2011 linalohusu kuingilia mkutano wa kampeni kwa mujibu wa ratiba ya msimamizi wa uchaguzi. Kwa sasa jeshi hilo linaendelea kukusanya ushahidi kuhusiana na kesi hizo. Hata hivyo, Kamanda Mngulu alitoa wito kwa vyama, viongozi, wanachama, wapenzi na wafuasi wa vyama vya siasa kuacha tabia ya kujichukulia sheria mikononi hususan kipindi hiki cha uchaguzi.
Hapo kwenye red mbona namba za majalada zinafanana??
 
Hapo kwenye red mbona namba za majalada zinafanana??

Mwandishi wa habari au uhariri wa Gazeti la Tanzania daima ndio waliofanya makosa labda maana hii ni nukuu kutoka gazetini bila kuhariri chochote kuanzia kichwa cha habari na na habari nzima.

Kilichopunguzwa toka kwenye habari hiyo ni nyongeza ambayo inahusu Kamanda Mbowe na Dr Slaa kuzunguka nchi nzima kuhamasisha wanachi wasiichague CCM.
 
Alyepaswa kukamatwa alikuwa ni mkuu wa wilaya aliyehendesha mkutano batili wakati wa uchaguzi na pia kwa kitendo chake cha kukutwa na fomu za maombi ya usimamizi wa uchaguzi wakati yeye hausiki. Madai mengine yote yaliyobaki ni hasira za kuhumbuliwa na wananchi.

Mtu alyepigwa na kukatiwa cheni aombi kwenda kwenye mkutano kuonana na slaa ili amwombe msamaha bali anakwenda hospitalini kutibiwa na madai mengine yanafuata baadaye.
 
they took this long kuwakamata? i was wondering what was nt happening...at last!

Imechukua muda mrefu kutokana na polisi kupata kigugumizi cha nani asikilizwe kwanza kwa vile wote Chadema na Mkuu wa Wilaya wamepeleka malalamiko polisi.
 
mkuu wa wilaya akiwa na cheni yake kifuani kabla ya kukaa kwenye kiti na kuojiwa na waandishi bila kuoji ilipo simu yake wala madai ya kupigwa hakuyasema wala hakwenda hospitali alichodai ni kuomba aonane na DR.SLAA .

MKUU WA WILAYA AKIWA NA CHENI YAKE KIFUANI MBELE YA WAANDISHI WA HABARI WAKICHUKUA PICHA. ITABIDI POLISI WAMFUNGULIE
YA KUFAILI FALSE STATEMENT KWA POLISI.

attachment.php
 
yaani bado najiuliza ,ina maana mkuu wa wilaya hakwenda mkutanoni hata na afisa usalama wa wilaya?basi huo mkutano ulikuwa wa kimagumashi acha wamtie adabu kwa sababu hakuheshimu cheo chake in the first place.
 
Kwa hili CCM hawana la kujitetea, wamelikoroga lazima walinywe wenyewe, Huyo mkuu wa wilaya alistahili hiyo aibu. Na nashangaa kwa nini hawakuumpa kisago, kwakweli vijana wa CHADEMA wameonesha ustaarabu sana kwa hilo!
 
Kwa hili CCM hawana la kujitetea, wamelikoroga lazima walinywe wenyewe, Huyo mkuu wa wilaya alistahili hiyo aibu. Na nashangaa kwa nini hawakuumpa kisago, kwakweli vijana wa CHADEMA wameonesha ustaarabu sana!
 
huyu mama alistahili kupata kichapo maana wanatumiwa sana na ccm ndio maana anajifanya kanyanyaswa kumbe ni uongo
 
Mzee Mwanakijiji juzi juzi hapa katoa mada kuhusu siri ya CCM. Ni siri gani Mkuu wa Wilaya akaenda peke yake bila ulinzi stahiki hata wa mgambo tu kama polisi na makachero walikuwa na shughuli za ulinzi wa Kampeni? Kuna mambo ya siri aliyokuwa anafanya huku.
 
Mzee Mwanakijiji juzi juzi hapa katoa mada kuhusu siri ya CCM. Ni siri gani Mkuu wa Wilaya akaenda peke yake bila ulinzi stahiki hata wa mgambo tu kama polisi na makachero walikuwa na shughuli za ulinzi wa Kampeni? Kuna mambo ya siri aliyokuwa anafanya huku.
Alikuwa anaenda kuwanga.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom