Kufuatia kibano cha DC (Igunga): Wabunge wa CHADEMA wakamatwa

SERIKALI imesikitishwa na udhalilishaji uliofanywa na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa Mkuu wa Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Fatma Kimario juzi.

Imesema kwa kuwa nchi inafuata utawala wa sheria, inaviachia vyombo vya Dola vifanye uchunguzi wake.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Mkuchika, alipozungumza na gazeti hili akiwa Newala mkoani
Mtwara.

“Serikali imesikitishwa na udhalilishaji uliofanywa kwa DC wa Igunga. Nchi ina taratibu, kanuni na sheria kwa hiyo unaviachia vyombo vya Dola kufanya kazi yake. “Lakini tumesikitishwa na tukio lile kwa sababu DC alikuwa tayari kusema nao, alikuwa eneo lake la utawala akifanya kazi. Kwa nini wamkamate na kumtoa nje kwa udhalilishaji ule,” alisema Mkuchika.

Alisema haikuwa vyema kwa wahusika kufanya udhalilishaji huo hasa baada ya Mkuu huyo wa wilaya kuwa tayari kuzungumza nao; hivyo wangeweza kuzungumza naye ofisini katika mazingira ya ustaarabu.

DC Kimario alifanyiwa vurugu na vijana wa Chadema juzi akiwa katika shughuli zake za kikazi.

Vijana hao walidai DC alikuwa akifanya kampeni za kisiasa katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Igunga utakaofanyika Oktoba 2, mwaka huu.

Katika taarifa yake jana, Polisi ilisema DC huyo amefanyiwa shambulio la kudhalilisha kinyume cha maadili, ikiwemo kuvuliwa vazi lake la hijab ambalo humsitiri mwanamke wa Kiislamu hasa kichwani.

Akizungumza jana wilayani Igunga, Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathimini wa Polisi, Makao Makuu ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP), Isaya Mngulu, alisema mbali na kuvuliwa hijab, pia DC alidai alivuliwa viatu na kukatiwa mkufu.

"Pia simu yake ya mkononi aina ya Samsung ilipotea na alitukanwa matusi ya nguoni ya kumdhalilisha …(hatuwezi kuyaandika hapa)," alisema Mngulu akielezea madai hayo ya DC Kimario.

Alisema wakati Mkuu huyo wa Wilaya akifanyiwa vitendo hivyo na vijana hao wa Chadema, Ofisa Tawala wa Wilaya ya Igunga, Sunera Manoti, alikwenda Polisi kutoa taarifa.

Hata hivyo, baada ya Polisi kupata taarifa hiyo, kwa mujibu wa Mngulu, walikwenda eneo la tukio na kukuta hali ni shwari na kuanza upelelezi baada ya majalada ya tuhuma; la kwanza la DC akilalamika kufanyiwa shambulio la aibu na la pili la Chadema wakilalamikia kuingiliwa katika mkutano wa kampeni.

Kwa mujibu wa taarifa za Chadema, Mbunge wa Viti Maalumu, Suzan Kiwanga, Mbunge wa Maswa Mashariki, Kasulumba Sylvester pamoja na shabiki wao ambaye jina lake halikupatikana waliitwa Polisi na kuhojiwa saa moja na kuachiwa kwa dhamana.

Madai ya Chadema Awali, kabla ya Polisi kuzungumzia hilo, Chadema iliitisha mkutano na waandishi wa habari na kuelezea makosa 15 ya DC huyo, likiwemo la kuitisha mkutano waliodai kuwa ni wa hadhara na kinyume cha sheria.

Akifafanua madai hayo, Mkurugenzi wa Chadema wa Oganaizesheni na Mafunzo, Benson Singo, alidai kuwa mtu ye yote akitaka kufanya mkutano, lazima atoe taarifa kwa Polisi na kwa kuwa polisi walikuwa wakifahamu kuwepo kwa mkutano wa Chadema, wasingemruhusu DC kufanya wa kwake.

Hata hivyo, Mngulu alisema DC Kimario alikuwa katika kikao cha ndani na sio mkutano wa hadhara kama Chadema walivyodai, ambacho kisingehitilafiana na mkutano huo wa Chadema, lakini hata muda wa tukio la kushambuliwa Mkuu huyo wa Wilaya na mkutano wa Chadema vilikuwa tofauti.

Kwa mujibu wa ratiba ya mikutano ya hadhara ya kampeni iliyooneshwa na Mngulu, Chadema ilipaswa kufanya mkutano wao wa hadhara katika eneo hilo la Kijiji cha Isakamaliwa saa 4 asubuhi hadi saa 6 mchana na tukio hilo, lilitokea kati ya saa 8:30 na saa 9.

Mngulu alisema hata polisi walikwenda eneo la mkutano huo kulinda amani saa 4 mpaka saa 6, lakini waliondoka kwa kuwa Chadema hawakwenda katika mkutano huo kwa mujibu wa ratiba.

Chadema pia walilalamika kuwa katika kikao hicho, DC huyo alikusanya na kujadili barua za maombi ya wasimamizi wa vituo vya kupigia kura na waelekezaji wa vituo kinyume cha sheria.

Hata hivyo, DC Kimario alipozungumza na waandishi na kuhojiwa kuhusu kukutwa na baadhi ya barua za maombi ya wasimamizi wa vituo vya kupiga kura, alisema alipewa na wasimamizi wa uchaguzi vijijini ili awasaidie kuzipeleka kwa msimamizi wa uchaguzi.

DC katika maelezo hayo, alisema anajua Chadema watasema kuwa alikuwa na hizo barua, lakini kwa maelezo yake ni kwamba yeye alitoa msaada tu wa kuzifikisha kwa msimamizi wa uchaguzi.

Waandishi wagawanyika Katika tukio lingine, waandishi wa habari waliokutana Kituo cha Polisi muda mfupi baada ya kumalizika kikao cha Chadema na waandishi, waligawanyika, baadhi wakimtuhumu DC kuwa ndiye mwenye makosa; wengine wakiituhumu Chadema ndiyo chenye makosa.

Waliomtuhumu DC Kimario kuwa ndiye mwenye makosa, walidai ameitisha mkutano huo kinyume cha sheria na walipopewa sheria hiyo na kutakiwa kuisoma, walibadilika huku wakisahihishana kuwa, hakukiuka sheria, bali maadili ya uchaguzi.

Waliokuwa wakituhumu kuwa Chadema ina makosa; walitaka kujua Polisi imechukua hatua gani; kama inawashikilia watuhumiwa ni wangapi, akina nani na lini watapelekwa mahakamani.

Akijibu hoja hizo, Mngulu alisema suala la kukiuka maadili ya uchaguzi ni la Msimamizi wa Uchaguzi, Protas Magayane, lakini suala la shambulio ni la Polisi.

Alisema mpaka sasa wameshawahoji watu watatu, lakini akakataa kuwataja majina kwa maelezo kuwa uchunguzi bado unaendelea. Hata hivyo katika mkutano na waandishi wa habari na Chadema, Mkurugenzi wa Chadema wa Oganaizesheni na Mafunzo, Singo alisema waliohojiwa ni pamoja na wabunge hao wa Chadema.

Gazeti hili liliwasiliana na Msimamizi wa Uchaguzi, Magayane kwa simu ambaye alijibu kuwa yupo Dar es Salaam akishughulikia picha za wagombea.

Kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Igunga tayari zimekumbwa na matukio ya vurugu huku yakihusishwa na Chadema ikiwemo mtu mmoja kumwagiwa tindikali na wengine kukatwa mapanga.

GAZETI LA HABARI LEO, Septemba 17, 2011

of course hili ni kama gazeti la uhuru ilikuwa inategemewa wao kusema hivyo kwani ni mwenzao ningeshangaa kama wangesema the opposite, kuhusu swala la kuvuliwa hijabu ni picha ndizo zinawasuta kwa maana mama huyu kipindi chake chote alikuwa na hijabu kichwani.kuhusu cheni bado ameivaa kifuani mwake wakati anahojiwa na waandishi wa habari ni aibu tupu angalieni picha jamani. kuhusu kukutwa na fomu jamani hilo alikubaliki kwani siyo kazi ya DC kushugulikia maombi ya wasimamizi wa uchaguzi ni kazi ya tume hapo inaonyesha wazi kuna watu walitaka kupandikizwa ili wawe wasimamizi wavuruge uchaguzi. kuhusu wengine kupigwa mapanga, ni ajabu hata matukio ya kihalifu sasa ni chadema ndiyo wamefanya kwahiyo ktk kipindi hiki cha uchaguzi wezi na majambazi wote wamekwenda likizo ndivyo CCM inavyotaka tuamini.
 
Tuwe wakweli chadema ni wavunjaji wa sheria, hapa wamefanya kosa kubwa kuchukua sheria mkononi na kumdharirisha mteule wa rais ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani
aliyeanza kujidhalilisha ni yeye kwa kwenda mkutanoni bila ulinzi !
 
Huyo DC alipenda mwenyewe kudhalilishwa! Sasa kama anafanya mambo ya kijinga alitaka makamanda wamchekee!
 
Nimeangalia sana picha za huyu kwangu anaonekana kama ni Mama Kada na wala si mkuu wa wilaya .Muonekano wake unanitia shaka sana kwamba anaweza kuwa na msimamo wa maendeleo ya Nchi badala ya uswahili na Chama .Huyu mama kweli anapewa madaraka makubwa namna hii ?Mtu analia na mkufu sijui chain na simu ya mchina ya laki 4 ? Uteuzi wa JK na wanavyo gawana ulaji una mashaka sana hata mtu kuingia mtaani bila ulinzi wowote kama kweli alikuwa kazini kihalali .Vinginevyo siri zao zitawaumbua kila mara.
 
Huyo DC alipenda mwenyewe kudhalilishwa! Sasa kama anafanya mambo ya kijinga alitaka makamanda wamchekee!
Take care!
Dola linaweza sana kujitetea, sitashangaa kama hao vijana mnaowashangilia wakila mvua kadhaa "kuonyesha mfano kwa wengine".
 
LAZIMA TUKUBALINE KWAMBA; KAMA WEWE SI MSTAARABU THEN AKUNA ATAKAYEKUFANYIA USTAARABU!! KAMA LILE NI ENEO LA UTAWALAWA HUYO DC KWA NINI ASIJUE UWEPOWA HUO MKUTANO WA CHADEMA? [Kauli yake "sikujua kama mnamkutano hapa"]
CCM wasitufanye tu wajinga kiasi hicho!!

SERIKALI imesikitishwa na udhalilishaji uliofanywa na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa Mkuu wa Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Fatma Kimario juzi.

Imesema kwa kuwa nchi inafuata utawala wa sheria, inaviachia vyombo vya Dola vifanye uchunguzi wake.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Mkuchika, alipozungumza na gazeti hili akiwa Newala mkoani
Mtwara.

"Serikali imesikitishwa na udhalilishaji uliofanywa kwa DC wa Igunga. Nchi ina taratibu, kanuni na sheria kwa hiyo unaviachia vyombo vya Dola kufanya kazi yake. "Lakini tumesikitishwa na tukio lile kwa sababu DC alikuwa tayari kusema nao, alikuwa eneo lake la utawala akifanya kazi. Kwa nini wamkamate na kumtoa nje kwa udhalilishaji ule," alisema Mkuchika.

Alisema haikuwa vyema kwa wahusika kufanya udhalilishaji huo hasa baada ya Mkuu huyo wa wilaya kuwa tayari kuzungumza nao; hivyo wangeweza kuzungumza naye ofisini katika mazingira ya ustaarabu.

DC Kimario alifanyiwa vurugu na vijana wa Chadema juzi akiwa katika shughuli zake za kikazi.

Vijana hao walidai DC alikuwa akifanya kampeni za kisiasa katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Igunga utakaofanyika Oktoba 2, mwaka huu.

Katika taarifa yake jana, Polisi ilisema DC huyo amefanyiwa shambulio la kudhalilisha kinyume cha maadili, ikiwemo kuvuliwa vazi lake la hijab ambalo humsitiri mwanamke wa Kiislamu hasa kichwani.

Akizungumza jana wilayani Igunga, Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathimini wa Polisi, Makao Makuu ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP), Isaya Mngulu, alisema mbali na kuvuliwa hijab, pia DC alidai alivuliwa viatu na kukatiwa mkufu.

"Pia simu yake ya mkononi aina ya Samsung ilipotea na alitukanwa matusi ya nguoni ya kumdhalilisha …(hatuwezi kuyaandika hapa)," alisema Mngulu akielezea madai hayo ya DC Kimario.

Alisema wakati Mkuu huyo wa Wilaya akifanyiwa vitendo hivyo na vijana hao wa Chadema, Ofisa Tawala wa Wilaya ya Igunga, Sunera Manoti, alikwenda Polisi kutoa taarifa.

Hata hivyo, baada ya Polisi kupata taarifa hiyo, kwa mujibu wa Mngulu, walikwenda eneo la tukio na kukuta hali ni shwari na kuanza upelelezi baada ya majalada ya tuhuma; la kwanza la DC akilalamika kufanyiwa shambulio la aibu na la pili la Chadema wakilalamikia kuingiliwa katika mkutano wa kampeni.

Kwa mujibu wa taarifa za Chadema, Mbunge wa Viti Maalumu, Suzan Kiwanga, Mbunge wa Maswa Mashariki, Kasulumba Sylvester pamoja na shabiki wao ambaye jina lake halikupatikana waliitwa Polisi na kuhojiwa saa moja na kuachiwa kwa dhamana.

Madai ya Chadema Awali, kabla ya Polisi kuzungumzia hilo, Chadema iliitisha mkutano na waandishi wa habari na kuelezea makosa 15 ya DC huyo, likiwemo la kuitisha mkutano waliodai kuwa ni wa hadhara na kinyume cha sheria.

Akifafanua madai hayo, Mkurugenzi wa Chadema wa Oganaizesheni na Mafunzo, Benson Singo, alidai kuwa mtu ye yote akitaka kufanya mkutano, lazima atoe taarifa kwa Polisi na kwa kuwa polisi walikuwa wakifahamu kuwepo kwa mkutano wa Chadema, wasingemruhusu DC kufanya wa kwake.

Hata hivyo, Mngulu alisema DC Kimario alikuwa katika kikao cha ndani na sio mkutano wa hadhara kama Chadema walivyodai, ambacho kisingehitilafiana na mkutano huo wa Chadema, lakini hata muda wa tukio la kushambuliwa Mkuu huyo wa Wilaya na mkutano wa Chadema vilikuwa tofauti.

Kwa mujibu wa ratiba ya mikutano ya hadhara ya kampeni iliyooneshwa na Mngulu, Chadema ilipaswa kufanya mkutano wao wa hadhara katika eneo hilo la Kijiji cha Isakamaliwa saa 4 asubuhi hadi saa 6 mchana na tukio hilo, lilitokea kati ya saa 8:30 na saa 9.

Mngulu alisema hata polisi walikwenda eneo la mkutano huo kulinda amani saa 4 mpaka saa 6, lakini waliondoka kwa kuwa Chadema hawakwenda katika mkutano huo kwa mujibu wa ratiba.

Chadema pia walilalamika kuwa katika kikao hicho, DC huyo alikusanya na kujadili barua za maombi ya wasimamizi wa vituo vya kupigia kura na waelekezaji wa vituo kinyume cha sheria.

Hata hivyo, DC Kimario alipozungumza na waandishi na kuhojiwa kuhusu kukutwa na baadhi ya barua za maombi ya wasimamizi wa vituo vya kupiga kura, alisema alipewa na wasimamizi wa uchaguzi vijijini ili awasaidie kuzipeleka kwa msimamizi wa uchaguzi.

DC katika maelezo hayo, alisema anajua Chadema watasema kuwa alikuwa na hizo barua, lakini kwa maelezo yake ni kwamba yeye alitoa msaada tu wa kuzifikisha kwa msimamizi wa uchaguzi.

Waandishi wagawanyika Katika tukio lingine, waandishi wa habari waliokutana Kituo cha Polisi muda mfupi baada ya kumalizika kikao cha Chadema na waandishi, waligawanyika, baadhi wakimtuhumu DC kuwa ndiye mwenye makosa; wengine wakiituhumu Chadema ndiyo chenye makosa.

Waliomtuhumu DC Kimario kuwa ndiye mwenye makosa, walidai ameitisha mkutano huo kinyume cha sheria na walipopewa sheria hiyo na kutakiwa kuisoma, walibadilika huku wakisahihishana kuwa, hakukiuka sheria, bali maadili ya uchaguzi.

Waliokuwa wakituhumu kuwa Chadema ina makosa; walitaka kujua Polisi imechukua hatua gani; kama inawashikilia watuhumiwa ni wangapi, akina nani na lini watapelekwa mahakamani.

Akijibu hoja hizo, Mngulu alisema suala la kukiuka maadili ya uchaguzi ni la Msimamizi wa Uchaguzi, Protas Magayane, lakini suala la shambulio ni la Polisi.

Alisema mpaka sasa wameshawahoji watu watatu, lakini akakataa kuwataja majina kwa maelezo kuwa uchunguzi bado unaendelea. Hata hivyo katika mkutano na waandishi wa habari na Chadema, Mkurugenzi wa Chadema wa Oganaizesheni na Mafunzo, Singo alisema waliohojiwa ni pamoja na wabunge hao wa Chadema.

Gazeti hili liliwasiliana na Msimamizi wa Uchaguzi, Magayane kwa simu ambaye alijibu kuwa yupo Dar es Salaam akishughulikia picha za wagombea.

Kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Igunga tayari zimekumbwa na matukio ya vurugu huku yakihusishwa na Chadema ikiwemo mtu mmoja kumwagiwa tindikali na wengine kukatwa mapanga.

GAZETI LA HABARI LEO, Septemba 17, 2011
 
Formula ni moja tu!
Kama hauchukui hatua, inakula kwako, ndicho walichikifanya makamanda.
If you let these janjaweed do what they are good at, then you are setting your failure route.

hit them when they are real hot!
Bravo guys
 
huyu mama sijawahi kuona nywele zakejifunika kichwa siku zote kumvua mwanamke wa imani hiyo hijab ni udhalilishaji wa hali ya juu!nawashangaa wanawake wanaoshangilia udhalilishaji huo!

Imani yenyewe ya majini matupu
 
Chochote watakachoamua dhidi ya wafuasi wa cdm na kiwe lakini nguvu ya uma imefanya kazi
na itaendelea kufanya kazi
 
katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania inampa jukumu kila raia wa tanzania analo jukumu la kuzuia uhalifu au kosa lisifanyike.kwa hatua hiyo ni kwamba vijana wa chadema walikuwa najukumu la kuzuia mkutano wao usiingiliwe na mtu awaye yote.
 
@Kila mtu anajua DC alikuwa anafanya kikao haramu tena na watendaji wa CCM kuwekana sawa namna ya kuharibu demokrasia katika uchaguzi wa Igunga. Ndio maana DC alihamaki sana&kutoa maelezo tata baada ya kufumaniwa. Bahati nzuri tukio zima lilitokea mchana kila mtu akiona na hata waandishi wa habari wakipiga picha na kuchukua video. @Vyombo vya dola kuwakamata wabunge wa Chadema pekee ni kugeuza kibao ili kufunika kombe nia kuficha aibu ya DC. @Na huu ndio uongo na unafiki wa jeshi la polisi&Serikali yetu; 1/Inashangaza kuona mwanzo mpaka mwisho wa tukio zima polisi hawakuwepo (Wakati askari na vifaa vya kutosha vimepelekwa Igunga kuhakikisha usalama) 2/DC bado hajakamatwa na kuhojiwa kama walivyofanyiwa wabunge wa Chadema (Kumbuka wote walifungua majalada polisi) 3/Mkuchika nae anamtetea DC badala ya kumuonya DC aache kuvuruga demokrasia. 4/Ni vipi polisi walishindwa kuzuia mkutano wa Chadema kama haukupaswa kufanyika kwa wakati huo au Walishindwa vipi kuzuia kikao cha DC ktk eneo ambalo Chadema walikuwa wanafanyia mkutano?
 
Mwaka jana wakati wa campaign huko Shinyanga mgombea ubunge kwa tikect ya ccm alimtwanga mateke mkuu wa kituo cha polisi lakini issue yote iliwekwa chini ya carpet, hakukuwa na kauli ya serikali au polisi. Leo hii serikali hiyo hiyo inaonekana kupaza sauti kwa sababu ni CHADEMA ndio wamemshughulikia mpambe wao. Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo, ccm wamezoea kupiga/kudhalilisha wengine sasa CHADEMA are doing what ccm knows best.
 
huyo jamaa anayemvuta dc magamba lazima wazae nae watamtafuta popote alipo wampe hata kesi ya kichwaa
 
Back
Top Bottom