Kufeli kwa Serikali kuhamia Dodoma

Tatizo watu hawajapenda Dodoma kupewa hadhi yake,wanataka kila kitu kiwe Dar kwa kigezo cha bahari na starehe nyinginezo.Mungu akipenda inawezekana Dodoma ikawa chanzo cha mafanikio ya mikoa ambayo iliachwa na wakoloni pasipo maendeleo yoyote
 
Una matatizo.
Fika dodoma uone mji unavyo shamiri.
 
Wakati Nyerere alipoamua Dodoma iwe makao makuu ya nchi sababu kuu zilikuwa za kiusalama kwani nchi yetu ilikuwa kinara wa kusaidia ukombozi barani Afrika. So maadui wakubwa, makaburu that time walikuwa tishio sana kuushambulia, from Dar. Sababu hizo kwa sasa hazipo, kwani sasa hivi watu wanaangalia zaidi economic reasons lakini pia na mazingira mazuri ya investment. Nimesikia rais akigusia kwamba Dodoma sasa ndiyo makao makuu na hata akimaliza muda wake hakuna kurudi Dar. Hii kauli inaashiria wasiwasi uliopo kwamba maamuzi haya one day yanaweza kuwa reversed....


Aisee sasa kipi ni kipi maana mengi yanasemwa kuhusu Makao Makuu Dodoma.
 
MARA MIA MJI UNGEJENGWA MOROGORO KWA KUIKATA KATIKATI UKATENGENGWA MKOA MMOJA UKAITWA MAKAO MAKUU
KWASABABU NI KARIBU NA DAR ES SALAAM
Well said [emoji120] [emoji120] [emoji120] [emoji106] [emoji106] [emoji106]
 
Udogo wa Dar siyo issue kwani wangepanga vizuri Kibaha, mpaka Mlandizi, pugu, mkuranga yote ingekuwa part ya Dar.
 
Una matatizo.
Fika dodoma uone mji unavyo shamiri.
Swali moja kwako mkuu nitajie vivutio vitatu tu vya kiuchumi ambavyo vilikuepo dodoma kabla ya serikali kutangaza kuhamia huko.na ikibidi uvitolee ufafanuzi katika ufanisi wake na je serikali imeviendelezaje?? Isije kua tuna anza halafu tunapongezana bila ya kuwa na saababu za msingi.
 
Udogo wa Dar siyo issue kwani wangepanga vizuri Kibaha, mpaka Mlandizi, pugu, mkuranga yote ingekuwa part ya Dar.
Yes ingekuwa ni wilaya hata tano kiuchumi ilikua na faida sana yaani ingekusanya mlandizi kibaha ni wilaya za jirani halafu makao makuu yawe morogoro ungeona mji unavyokua kwa kasi ; maghorofa unayoyaona posta yangefika mpaka chalinze tena kwa masta plan yakueleweka na fly over za kimkakati zingejengwa
 
Dodoma ndipo panastahili kuwa makao makuu,
1. Ni karibu kufikika kwa watu wa mikoa mbali mbali. Dodoma ina barabara kuu 4, watu kufata huduma ni rahisi kuliko Dar

2. kuondoa tatizo la "centralization" haiwesekani nchi kubwa hivi kila kitu kiwe Dar, kuanzia Elimu vyuo vingi kurundikana Dar, mahospitali makubwa yote Dar, Majengo Marefu yote Dar, viwanja vya mpira Dar, kila kitu Dar

3. kupunguza foleni, population Dar,

4. pakiwa mji mkuu kamili ,hivo vilivyopo Dar vitajengwa na Dodoma pia kutokana na mahitaji
NB😀odoma waiplan vizuri isiye kuwa kama miji yetu mingine
 
Anahamasisha wahamie Dodoma lakini yeye muda mwingi kama si wote yupo Dar. Hameni na wake zenu. Mnaopewa ubalozi mwende na wake zenu.
 
Nakubaliana na maamuzi ya kuhamishia makao makuu ya nchi kuwa Dodoma ila kitu ambacho hakijanifurahisha ni kuharakisha uamuzi na kutowahusisha wataalamu ktk maamuzi
Wangefanya kama UAE, Mfalme alichukua vijana 10 akawapeleka katika 5 Big Cities(2@ in every city) in the World kazi yao kubwa ni kufanya Observation kwa miaka 2 mtawalio jinsi gani miji hiyo inatunzwa na kuendeshwa na kupeleka report kwa Mfalme hatimae ndio hii miji tuionayo sasa
Mimi ni muumini mzuri wa kitu kinaitwa " simulation" yaani kama unaamua kuhamia Dodoma unajipangia a number of steps za kuhama kulingana na mahitaji ya kuhama, na hiki kitu kiliishaanza kufanyika tena hamuwezi kuamini Wizara ya Kwanza kuhamia Dodoma ilikuwa ni Wizara ya Maji chini ya Edward Lowassa nina hakika it was a good strategy Wizara ya Maji kuhamia kule na kuweka sawa Infrastructure za Maji toka Ziwa Victoria ambapo kungekuwa na malengo ya lets say miaka 15 ijayo ambapo kwa wakati ule hivi sasa ingeishafika miaka 15
Kulikuwa na Wizara nyingine iliyokuwa chini ya Mizengo Pinda nayo ilikwishahamia kule nayo ingefanya mambo yake then hivyo hivyo mpaka Wizara zote zinaisha
 
Labda wayavute ya Ziwa victoria toka tabora.itasaidia
 
Hama acha maneno maneno..najua unapo angalia ulichowekeza Dar roho inakuuma.
 
Dodoma kuna mawe mengi sana.
Hiyo ni fursa ya kiuchumi!
 
ni mara yangu ya kwanza kukaa ddm angalau kwa wiki mbili sasa, ukweli bado safari ni ndefu sana sana kuifikisha ddm kwenye hadhi ya jiji, ddm bado mno
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…