Kufeli kwa Serikali kuhamia Dodoma

Kufeli kwa Serikali kuhamia Dodoma

Wakuu zipo sababu kibao ambazo tukizitaja zinaweza kuwa mwiba mchungu sana lakini itabidi tuzitaje ili kuuboresha mji wa Dodoma ambao umepewa hadhi ya jiji ikiwa kimuonekano baado sana

1. Geografia ya mji wa Dodoma
Mkoa huu ni miongoni mwa mikoa mikame na yenye asili ya jangwa kwa maana hauna mvua za kutosha ikiwa wastani wa mvua zake ni miezi mitatu au minne kasoro. Hivyo uoto wa asili muda wote ni ukame. Najiuliza sana serikali yetu imetenga bajeti kuwekeza katika eneo lenye ukame na kulifanya liwe la kuvutia au wamekurupuka tu.

Tukiangalia miji ya Dubai, Misri yenye hali kama hii ya ukame wametumia gharama kubwa kufanya miji ipendeze.pia ukiacha ukame kuna bonde la ufa limepita pale ambalo kitaalamu linakufanya usijenge majengo marefu kwenda juu.

2. Mzunguko wa pesa
Kwa sasa mkoa huu umekuwa na mzunguko wa pesa kwakuwa kuna uuzwaji mkubwa wa viwanja lakini baada ya hapo sidhani kama kutakuja kuwa na mzunguko wa pesa. Pia uwekezaji unaofanyika hauendani na ungezeko la watu.

Yaani unajenga majengo ya gharama mbali na miji ya watu halafu watu waje wajae kama maji ya bahari ni kitu kigumu sana.

Hii itatokea kwa miaka ya mbele kama 40 au zaidi. Kinachofanyika sasa ni kuharibu pesa za walipa kodi ambazo kurudi kwake itatugharimu miaka mingi.

3. Ni mji wa kisiasa (Makao makuu ya CCM)
Kwa mitazamo ya kawaida tunajua huu mji Nyerere na serikali waliufanya uwe makao makuu ya Chama cha Mapinduzi. Kimsingi sio wazo baya ila Nyerere mwenyewe alishtuka kuufanya katika kuufanyia maendeleo kwa kuwa kisiasa watu watajitambua na CCM itapoteza taswira. Serikali hii imevunja kanuni ya huu mji haukutakiwa kuendelezwa ili CCM itawale.

Yapo mengi ya kuelezea kwangu mimi. Wadau kama mnayo kuhusiana na mji huu mnaweza kutiririka.
Sababu kuu hapo ni hiyo 1 tu hizo zinginr porojo tu.
 
Hoja zako ni dhaifu sana ndugu. Hivi hujui hata hiyo miji kama Dubai, Tripoli na mingineyo kufikia hapo ilipo kuna hatua za awali kabisa walianza nayo?
Halafu kamwe usijidanganye kuwa eti kuwekeza kwenye kuendeleza mji wowote ule kwenye nchi hii kwamba ni kupotezza fedha. Ikiwa unajua jinsi ambayo mzunguko wa fedha ulivyo utaelewa. Ndg nasema hivi kwa kuwa Nia ipo acha tufanye kwani wenzetu walianza vipi sisi tushindwe?
 
Sawa kwann iwe 2015-2020 nakwann isingekuwa 1973 -2019 acha kuamini katika siasa ipo siku uwekezaji huu utakuja kubakia magofu yasiyokuwa na kazi mkuu
Ref. Mobito sseseko alijenga ikulu kwao limebaki gofu
 
ndoo maana utawala wangu makao makuu yatakuwa mtwara ujinga huu sasa
 
Mungu anakuona wewe
Viwanda vya maji kama Kilimanjaro, Dasani nk wawekeze kwa wingi Dodoma maana maji yao mabalozi watanunua kwa wingi sio kwa akili ya kunywa tuu bali hata kuogea ili wasipauke kwa chumvi!
Hakika mzee wetu ni mbunifu wa kuendeleza viwanda, pongezi kwake!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom