Pulchra Animo
Platinum Member
- Jun 16, 2016
- 6,828
- 10,460
Wakuu zipo sababu kibao ambazo tukizitaja zinaweza kuwa mwiba mchungu sana lakini itabidi tuzitaje ili kuuboresha mji wa Dodoma ambao umepewa hadhi ya jiji ikiwa kimuonekano baado sana
1. Geografia ya mji wa Dodoma
Mkoa huu ni miongoni mwa mikoa mikame na yenye asili ya jangwa kwa maana hauna mvua za kutosha ikiwa wastani wa mvua zake ni miezi mitatu au minne kasoro. Hivyo uoto wa asili muda wote ni ukame. Najiuliza sana serikali yetu imetenga bajeti kuwekeza katika eneo lenye ukame na kulifanya liwe la kuvutia au wamekurupuka tu.
Tukiangalia miji ya Dubai, Misri yenye hali kama hii ya ukame wametumia gharama kubwa kufanya miji ipendeze.pia ukiacha ukame kuna bonde la ufa limepita pale ambalo kitaalamu linakufanya usijenge majengo marefu kwenda juu.
2. Mzunguko wa pesa
Kwa sasa mkoa huu umekuwa na mzunguko wa pesa kwakuwa kuna uuzwaji mkubwa wa viwanja lakini baada ya hapo sidhani kama kutakuja kuwa na mzunguko wa pesa. Pia uwekezaji unaofanyika hauendani na ungezeko la watu.
Yaani unajenga majengo ya gharama mbali na miji ya watu halafu watu waje wajae kama maji ya bahari ni kitu kigumu sana.
Hii itatokea kwa miaka ya mbele kama 40 au zaidi. Kinachofanyika sasa ni kuharibu pesa za walipa kodi ambazo kurudi kwake itatugharimu miaka mingi.
3. Ni mji wa kisiasa (Makao makuu ya CCM)
Kwa mitazamo ya kawaida tunajua huu mji Nyerere na serikali waliufanya uwe makao makuu ya Chama cha Mapinduzi. Kimsingi sio wazo baya ila Nyerere mwenyewe alishtuka kuufanya katika kuufanyia maendeleo kwa kuwa kisiasa watu watajitambua na CCM itapoteza taswira. Serikali hii imevunja kanuni ya huu mji haukutakiwa kuendelezwa ili CCM itawale.
Yapo mengi ya kuelezea kwangu mimi. Wadau kama mnayo kuhusiana na mji huu mnaweza kutiririka.
Taifa lenye watu million 50+ halitarajiwi kuwa na mawazo yanayofanana. Kama ambavyo wewe hujaridhika na uamuzi wa kuhamia Dodoma, wapo wengi ambao watayaona mawazo yako kuwa hayana mashiko hata kidogo.
Mjadala kama huu kwa sasa hauna tija sana. Ungekuwa na maana kama uamuzi wa kuhamia Dodoma ungekuwa haujafanyika. Subiri watafiti wafanye tathimini ya huo uamuzi miaka 30-50 baadaye.
Kushindwa au kufanikiwa kwa mambo mengi ni matokeo ya self-fulfilling prophecies. On the one hand, if you’re overly pessimistic about a given project, you aren’t likely to give it your all, thereby guaranteeing the potential project failure. On the other hand, if you’re very optimistic about the project, your actions will (most of the time) be a positive (rather than a negative) contributory factor!