Kufanya masters, phd ni uoga wa maisha.

Kufanya masters, phd ni uoga wa maisha.

LIKUD

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
19,899
Reaction score
37,699
Kuna watu wanapenda sana maisha ya uanafunzi, utafikiri walizaliwa ili wasome.

Shule ya msingi ========= 7 years.

O-Level ========== 4 years.

A- Level =========== 2 years.

Degree ya kwanza =========3 au 4 years.

Jumla : Miaka 16 au 17.

Umekaa shuleni kwa muda wa miaka kumi na saba lakini bado hauna uwezo wa kutumia elimu na maarifa uliyo yapata shuleni kukabiliana na changamoto za maisha? Still unataka kwenda kufanya masters, miaka miwili, after masters, unataka tena PHD miaka 3, we vipi wewe?

Ukiniambia nimuelezee mtu wa namna hii kwa maneno machache , nitasema ' MUOGA WA MAISHA ". Anaogopa ugumu wa maisha, anashindwa kuzi face changamoto za maisha ( e.g ukosfu wa ajira ). Anataka aendelee kuonekana mwanafunzi ili kuutumia uanafunzi wake kama excuse ya kuwa broke. Let me tell you brother, the only excuse of being broke is to be in jail.

Achana na hizo bla blah za masters na PHD, piga kazi mjomba tujenge taifa letu. GPA yenyewe ya 2.1, masters mpaka ukafanye post graduate kwanza, dah watu wanajua kuua muda. Ukomboe wakati bro, siku ya mwisho utahukumiwa kwa kosa la ku ua muda. Nyambaff, unasoma hadi PHD halafu ukimaliza unaanza kutembea kwenye ofisi za watu na bahasha za kaki.
 
kula 5 mkuu,kama unataka kuwa academician au researcher it's ok kuendelea kusoma hadi elimu za juu zaidi,ila kiukweli digrii inatosha sana kukabiliana na changamoto nyingi za lyf nashangaa mijitu mingi kufuata mikumbo tu
 
Tanzania haitakaa ikombolewe unless watu wake kama hawa wakombolewe kwanza.

Kwa akili zake kidogo anadhani masters zote lazima usome miaka miwili.

Kwamba ukiwa na GPA ya 2.1 lazima ukafanye post graduate kwanza ili usome masters.

Sijui hata kama anajua maana ya post graduate.

Kwamba huwezi kufanya kazi huku ukiwa unasoma.

Hata hivyo mtu akiamua kusoma ni hiari yake, sijui kwa nini ikuwashie wewe?

Probably, hapo ulipo cheo chako kipo mashakani baada ya mwezio kwenda kupiga shule.

We vipi! Sasa wote tukiwa kama wewe tutapata wapi maprofesa vyuoni na wataalam wa fani mbalimbali? Hata mameneja wa bank wana masters pia

waacheni macadeicians waliopo vyuoni wakafanye hizo masters na p.h.d, sio wewe mwenzangu na mimi, G.P.A yenyewe 2.1, umekaa mtaani mwaka mmoja, miwili umeshindwa kupambana, unanyanyua mikono, unazuga kutafuta masters, qualifications zenyewe za kusoma masters, hauna, inabidi ufanye post graduate kwanza, mwaka mmoja na miezi minane , nyambaff, after post graduate, unaomba masters, hela huna unaanza kusumbua wanaume wakuchangie..nyambaff. Mbona vitu vya kufanya vipo vingi sana! Elimu ni ufunguo wa maisha, na kazi ya ufunguo ni kufungua milango na madirisha yaliyo fungwa, kama degree yako imeshindwa kukusaidia kufungua milango ya changamoto za maisha, masters and p.h.d will neva do anything for you. Utabika kulaumu wachawi bure, kumbe aliyekuroga wewe, ni mwanga yuleyule, aliyekataa kukupeleka SHULE YA KITAA, ndo hii nayo kupa, hakika itakufaa kwenye shida na raha, shauri yako ukiikataa, utakuja kupatwa na mabalaa weye...Shahada ya uzamivu, umekuwa kaboneke wewe!
 
Tanzania haitakaa ikombolewe unless watu wake kama hawa wakombolewe kwanza.

Kwa akili zake kidogo anadhani masters zote lazima usome miaka miwili.

Kwamba ukiwa na GPA ya 2.1 lazima ukafanye post graduate kwanza ili usome masters.

Sijui hata kama anajua maana ya post graduate.

Kwamba huwezi kufanya kazi huku ukiwa unasoma.

Hata hivyo mtu akiamua kusoma ni hiari yake, sijui kwa nini ikuwashie wewe?

Probably, hapo ulipo cheo chako kipo mashakani baada ya mwezio kwenda kupiga shule.

Wewe ndio unayehitaji kukombolewa, unadhani kila mtu ameajiriwa kama wewe. Hayo mambo ya vyeo, huwa yanazungumzwa na watu walio ajiriwa kama wewe au wanao amini katika kuajiriwa kama wewe.. It's a great thing when you can show that you've been successful and that you've made a lot of money and that you've employed a lot of people.
 
Mtoa mada bado haujui elimu kubwa Masters na PhD zina mchango gani kwa maendeleo ya taifa kwa ujumla, wewe umeegemea kwa mtu mmoja mmoja..!!
 
kula 5 mkuu,kama unataka kuwa academician au researcher it's ok kuendelea kusoma hadi elimu za juu zaidi,ila kiukweli digrii inatosha sana kukabiliana na changamoto nyingi za lyf nashangaa mijitu mingi kufuata mikumbo tu

Asante kwa kunielewa kaka.
 
Mtoa mada bado haujui elimu kubwa Masters na PhD zina mchango gani kwa maendeleo ya taifa kwa ujumla, wewe umeegemea kwa mtu mmoja mmoja..!!

Sina tatizo na waalimu wa vyuo vikuu, kwa sababu inabidi wasome hizo masters na phds, hapa nawazungumzia hawa weenzangu na mimi, G.P.A haisomi, yupo mtaani, haajariwa na taasisi yote ya kitaaluma, ameshindwa kupambana na changamoto za maisha, then anakuja na proposal ya kufanya masters and all that.
 
Hao hao baadae wanakuwa kina Mulongo, Maghembe, Mungai yaani hadi ukianza na title ya Prof unasikia kinyaa.
 
Back
Top Bottom