Kufanya kosa si kosa, kosa kurudia kosa. CHADEMA inakaribia kufa, hii ndio njia yenu pekee ya kujinasua

CHADEMA wala haifi karibuni. Unashangilia kitendo hiki kwa sababu kinainufaisha zaidi ccm na Magufuli kuliko CHADEMA yenyewe. Wizi na ubabaishaji vina mwisho wake hata hivyo
 
Mara kadhaa nimekuwa nikisema humu chadema imeshakufa., Kitendo cha Tundu Lissu kuhama nchi kwa style ile bila mapambano ndani ya nchi kwanza akishirikiana na wananchi imewafanya kina hawa halima mdee nao wakate tamaa kabisa kabisa inasikitisha sana.

Niliposema chadema imekufa humu JF walinitukana na kunikebehi. Chadema hawakuwa na plan B baada ccm kupora majimbo nchi nzima, yaonekana hawakuwa na mpango kabambe walioupanga kabla, sasa itabaki kuonekana maalim seif peke yake ndie amefaulu kuonyesha uaminifu wake siku zote kwa wananchi. Hakuwahi kuwakimbia wala kuwasaliti wananchi anaanguka nao akisimama nao kila siku.

Wabongo hela wanaindekeza sana, hawana utu kwenye hela. Njaa bado ni tatizo
 
Alafu jumapili unakaa viti vya mbele kanisani...Mbona huongelei wizi wa kura ambao haujawahi kutokea Afrika..kweli mjini maisha bila ya unafiki hayaendi.
 
Leo umenywea sana kama kaukau....uko chamani huna sauti nini,

Matamko ya mitandaoni leo kwisha#

Nimenywea kwa kipi labda? Naona unatamani ninywee, mimi sina maamuzi yoyote kwenye hicho chama, bali nina ushawishi wa kutosha.
 
Umeleta huu uzi kujihami coz unajua nini Chadema wanaweza kufanya, na mimi ndicho nachotaka wakifanye, wacha kuwatisha watu, Chadema lazima wawatimue hao wanawake ikithibitika kukiuka maamuzi ya Kamati Kuu.

Walifukuzwa kina Zitto Chadema bado ipo mpaka leo kwanini hao wanawake ndio wawe untouchables!, waondolewe, vinginevyo kubaki kwao ndani ya chama ndio kutawaondoa wapenda mabadiliko wa kweli.
 
Kila uchao Paschal unaelekea shimoni.Kaburi lako umechimba kwa mikono yako mwenyewe. Tukafikiri mwili ni dhaifu. Sasa hata nafsi yako si radhi. Kilichobaki ni roho kulihama jumba mwili. This is sooner than later. Kiingereza kinakupa shida mpaka mambo elementary kama third person singular. Hujui s inatumikaje kwenye nouns na verbs kiasi inatia kichefuchefu.

Kila uchao unaelekea level ya directions, font page, can't reach you! Hili jambo linaonekana kama dogo. Utawezaje makubwa wakati dogo limekataa? Limeathiri hadi upeo wako wa uchambuzi! Upande huo unaelekea level ya Jingalao, Magonjwa Mtambuka, Jmco6, na nungunungu wengine kiuchambuzi. Umeishamreach Wakudadavua. Tunaona zaidi demise ya Paschal kuliko ya Chadema!
 
Kuna wanasiasa wako kwenye siasa, na wametafuta uongozi wa siasa kwa kusaka madaraka tuu, uongozi as a means of livelihoods, lakini kiukweli siasa hawaziwezi, hawazijui wala hawajui uongozi wa umma sio utumishi wa chama ni utumishi wa watu.
Wewe ndio mwanasiasa wa hovyo ndiyo maana bwana yule alikuanika wazi kwa Njaa yako ndio maana amekubania kukupa shavu wewe ni Nuksi
 
Back
Top Bottom