Kufahamu kuhusu Bachelor Degrees za Economics

cabo

JF-Expert Member
Jun 15, 2016
4,751
5,224
Habari za kwenu,
Wana uzi mimi ni kijana nimemaliza form 6 na ninatarajia kujiunga na Chuo kikuu Mungu akinijaalia, ila kuna tatizo linanitatiza hasa katika program za kusoma.

Mimi binafsi napendelea kuchukua au kusomea maswala ya uchumi ila napata mkanganyiko kwenye akili yangu maaana kila nikifuatilia na kuchambuachambua kuhusu suala hilo naona kuna Bachelor degree in Economics, BA of arts in economics, BA in Economics & Statistics na nyingine.

Kwakweli mimi hata sizielewi zinahusiana na nini, naomben msaada wetu kunielewesha vizuri na jinsi ukizisoma baadae unakuwa nani.

Natumaini mtanielewesha vizuri na mtanipa ushauri mzuri kipi nikakisomee. Asanteni. HATIMAE MUNGU AMEJIBU MAOMBI
 
ngoja wataalamu waje ila mmi nakushauli achana na mambo hayo ya uchumi hayana ishuu wwe kama kwenu mshiko upo wa kutosha kasome chuo cha kodi masuala ya Tax and customs
 
Kasome B.A Economics ndugu.. ni kozi nzuri sana kama utaifikiria nje ya box. Usisome kitu kwa nia ya kupata ajira. Soma kitu kama umekipenda kutoka moyoni na utaifurahia elimu. Issue za ajira zitakuja baadae. Wala huwezi jua Mungu kakupangia mambo gani. Kila la heri
 
Nimekupata ila shida inakuja kwamba siifaham kabisa yan may b unifahamishe zaid kuhusu iyo BA
 
Back
Top Bottom