Kufahamu kuhusu Bachelor Degrees za Economics

Kufahamu kuhusu Bachelor Degrees za Economics

ngoja wataalamu waje ila mmi nakushauli achana na mambo hayo ya uchumi hayana ishuu wwe kama kwenu mshiko upo wa kutosha kasome chuo cha kodi masuala ya Tax and customs
Hii unakua nani pia ajira vp??
 
Wakati wa kujitayarisha ni sasa-angalia options na uzielewe. Kama untaka kuwa mfanya biashara inabidi pia uangalie program za business management na hizo za uchumi. Lakini kwanza ingia mtandaoni ugoogle hizo programs upate maelezo yake. Bahati mbaya ukiangalia prospectus zetu hazielezi kwa kina hivyo itabidi ucheck vyuo vingine hata vya nje.
Jiulize umechukua kombi ipi. HGE au EGM, nafikiri pia kuna ECA (masomo ya biashara zaidi). Economics & Statistics-UDSM na UDOM nafikiri wote wanataka in addition to Economics uwe na ADVANCE Maths, Wenye BAM naamini hawachukuliwi. BA in Economics (UDSM, UDOM, SAUT, JUCO , ARDHI) au BSc in Economics (Mzumbe) hawa wanachukua wote wa EGM na HGE. Halafu kuna Uchumi kilimo na Biashara (SUA) na Uchumi Kilimo, Mazingira na Biashara (UDSM)nao nafikiri wanachukua wote EGM na HGE. Somo moja lapo ambalo mtu wa uchumi hufanya ni Econometrics ambayo msingi wake huwa statistics na mathematics. Hivyo utakapolifikia kama umejenga msingi wake utaliweza au siyo kama mkuu mmoja alivyosema alilijua baada ya kula supp (lakini haya ndio maisha ya vyuo).
Ukisha jua kipi ni kipi unaweza kuangalia prospectus a vyuo tofauti. Karibu vyuo vyote vimeanzia na ile UDSM na kubadilisha machache. Ya SUA na UDSM kilimo zinautofauti wa kutosha kwani ni za kilimo +
Samahan mkuu ss hiyo bsc economics ya mzumbe na BA economics ya udsm ni tofauti ? Na utafauti wake upo WAP?
 
Wadau na Mimi naomba kujua kama mtu alie soma HGE anaweza soma kozi zinazo husika a na Madini ? Kama Ni ndiyo , Ni zipi na wapi pazuri? Natanguliza shukrani kwa ushirikiano mtakaonipa!
 
Samahan mkuu ss hiyo bsc economics ya mzumbe na BA economics ya udsm ni tofauti ? Na utafauti wake upo WAP?
Ukiangalia masomo wanaochukua yanafanana kwa asilimia kubwa kama 80% au zaidi. Ni vizuri u download prospectuses zote mbili mtandaoni za 2014/15 ulinganishe wewe mwenyewe.
 
Back
Top Bottom