Bachelor Degree in Shipping Economics and Logistics hii kozi inahusiana na nini?

Sheehan

Member
Apr 19, 2022
71
57
Habari za muda huu wanandugu wa JF,

Pale DMI kuna kozi inaitwa Bachelor degree in shipping economics and logistics hii kozi inahusiana na nini? then kwenye suala la fursa zake ipoje (Au ni kozi za watoto wa vigogo?)
 
Hii Kozi itakuwezesha kufahamu maswala ya usafirishaji wa njia za maji,Anga na Nchi kavu, namna ya kupanga mipango ya kutoa mizigo kutoka Sehemu Moja kwenda nyingine Kwa Kutumia njia ambazo ni gharama nafuu na haraka.

Ukimaliza Sehemu ambazo unaweza kupata kazi ni hapo hapo chuoni kuwa Tutorial Assistant, Kwenye kampuni za Shipping Line, Logistics Company,Inland Container Depot (ICD), ukijiongeza kujua baadhi ya vitu Kwenye Clearing and Fowarding unafanya na Bandari au wakitangaza post za kuhitaji taaluma hiyo
 
Asante sana mkuu, biala shaka umempa mwongozo mzuri kijana wetu. Wakati wowote huwa nakutegemea kwa positive input kwenye masuala haya ya majini.

Nje ya mada kidogo:
1. Nasikia TASAC wamepunguziwa baadhi ya majukumu na kuyakasimisha majukumu hayo kwa private sector ?

2. Offshore Seaman ni mkufunzi kwenye moja ya taasisi zetu za elimu ?
 
1. Ndio saizi majukumu ya Ship Agency, Cargo Tallying na Documents control for shipping agency. Watabaki na Kazi za kufanya clearing and Fowarding Kwenye nyara za serikali, wanyama pori, silaha na makinikia.

2. Mimi sio mkufunzi, nipo na harakati zangu za umachinga wa vifaa vya Majini
 
Back
Top Bottom